Ni kweli waliouawa Mwanza walitoka Kibiti?

Ni kweli waliouawa Mwanza walitoka Kibiti?

Polisi wakishika watuhumiwa hufanyiwa mahojiano ambayo upelekea kupata watuhumiwa.zaidi hivyo kulink na mwanza ni taarifa za awali kwa watuhumiwa wa kibiti simple as it.

Mobile Traveller
 
MUNGU NIPE HEKIMA NIONGEE KIDOGO KUHUSU WAUWAJI WA KIBITI.

Zipo taarifa kwamba kwamba wauwaji wa KIBITI wameuwawa Mwanza baada ya majibizano ya risasi na askari wetu.

Pia ziko taarifa kwamba akipatikana mtu mgeni kwenye eneo fulani kwa maana ya kwamba serikali ya eneo Hilo kutokumtambua basi atauwawa.

Kama taarifa hizi ndivyo zilivyo basi tunazo sababu za kujiuliza maswali mengi.

Kwamba, kama wauwaji wa KIBITI wameuwawa Mwanza kwenye majibizano ya risasi na askari, ni nani alitoa taarifa za uwepo wa watu hao Mwanza wakitokea KIBITI?

Je, aliyetoa taarifa ya watu hao kuwa wametoka KIBITI alizithibitihaje taarifa hizo na yuko wapi mpaka sasa?

Jeshi la Polisi linasema nini juu ya mtoa taarifa huyo ambaye kimsingi atalisaidia sana Jeshi letu la Polisi kufanya upelelezi?

Je, ni sahihi kwamba mtu yeyote mgeni kwenye eneo fulani anatakiwa kuuwawa? Na kama ndivyo mbona serikali yetu imekuwa na uoga wa kiwango hiki kwa wahalifu?

Je, hakuna namna nyingine ya kushughulika na wanaodaiwa kuwa ni wageni kwenye maeneo fulani zaidi ya kuwauwa?

Hii ni Tanzania ile ile tunayoisifia kwamba inaongozwa kwa misingi ya sheria?

KIBITI KIBITI KIBITI
MCHEZO WA SINEMA USIOTABIRIKA.
Haya ni mawazo tu lakini ya mjinga mmoja.
Uhalifu wa kutumia silaha haujaanza leo na haukuanzia Kibiti.
Uko pote nchini.
 
"Ujambazi haulipi"-by kamanda Sirro

Sent from my Infinix_X521 using JamiiForums mobile app
 
Police wetu wamegeuka kuwa killers sasa.

Sent from my SM-N920V using JamiiForums mobile app
 
we kiharusi, waliouwawa mwanza ni majambazi sio magaidi wa kibiti, nimeuona uzi umletwa na mlumumba mwenzako jingalao, kaelezea vizuuri kuwa ni igoma mashariki na msangi kakiri ni majambazi, leo gazeti lenu linasema kibiti,

nitakuumnga mkono pale utakapoacha chuki, ubaguzi na visasi
msome vizuri huyu mama; ameumizwa sana kwa mauaji ya hawa jamaa ; mtu yeyote mwenye weledi atajiuliza kwanini?? akamatwe ahojiwe. atatusaidia kupambana na hawa wauwaji.
 
Sijui ninawaza vibaya. Huyu kamanda Sabasi si alikuwaga Mz?? Sasa Kibiti kaenda huko wakamkimbia na kurudi Mz?? Kaaz kweli kweli
 
leo nilikuwa Kivule (sikuwahi kufika tangu nizaliwe) kumtembelea ndugu yangu wakati nasubiri mlo wa mchana nikaenda baa ya karibu 'kutoa loki' ila nilikuwa nahofu tupu.

Sent from my SM-A500F using JamiiForums mobile app
 
Hii indiscriminate killings inahitaji international attention! Upinzani achana na kusemea ndani, paza sauti UN, AU, EU etc, vinginevyo tunakwisha.
Hata mimi napata kigugumizi, huyo mtoa taarifa ambae kwa mujibu wa taarifa za Polisi wa mwanza amewezaje kujua hao wahalifu ndio waliohusika na mauaji ya Kibitii?? au wanatoka kibitii??, au pengine hao wahalifu aliwatambua kwa kuwa walikuwa na alama za kibiti usoni au alitoka nao kibiti! Naona umma unahitaji majibu sahihi vinginevyo polisi wasijisumbue sana kuzungusha mada wasema tu wameua majambazi, uma uelewe.

Sent from my IM-A860L using JamiiForums mobile app
 
kama majambazi waliouawa ni ndugu zako unakaribishwa katika postmortem halafu ukawazike kwa heshima.

Polisi ikishatangaza vita maana yake hakuna majadiliano ni action tu.

Hapa mtaani kwangu kuna wageni kibao sijaona wakiuawa na Polisi.

Wanaouawa ni Majambazi...na waendelee kuawa tu.
Kama una uhakika kuwa wanaouawa ni majambazi, basi usikike. Lakini kama huna uhakika wewe au ndugu yako kufa na mfe, maana imeandikwa ' usihukumu usije ukahukumiwa' na "auae kwa upanga nae ataangamia kwa huo"

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
Kwa sasa hata wewe wakikutaka wanakucharaza risasi halafu wanasema ni wa Kibiti.

Nani atabisha?
 
MUNGU NIPE HEKIMA NIONGEE KIDOGO KUHUSU WAUWAJI WA KIBITI.

Zipo taarifa kwamba kwamba wauwaji wa KIBITI wameuwawa Mwanza baada ya majibizano ya risasi na askari wetu.

Pia ziko taarifa kwamba akipatikana mtu mgeni kwenye eneo fulani kwa maana ya kwamba serikali ya eneo Hilo kutokumtambua basi atauwawa.

Kama taarifa hizi ndivyo zilivyo basi tunazo sababu za kujiuliza maswali mengi.

Kwamba, kama wauwaji wa KIBITI wameuwawa Mwanza kwenye majibizano ya risasi na askari, ni nani alitoa taarifa za uwepo wa watu hao Mwanza wakitokea KIBITI?

Je, aliyetoa taarifa ya watu hao kuwa wametoka KIBITI alizithibitihaje taarifa hizo na yuko wapi mpaka sasa?

Jeshi la Polisi linasema nini juu ya mtoa taarifa huyo ambaye kimsingi atalisaidia sana Jeshi letu la Polisi kufanya upelelezi?

Je, ni sahihi kwamba mtu yeyote mgeni kwenye eneo fulani anatakiwa kuuwawa? Na kama ndivyo mbona serikali yetu imekuwa na uoga wa kiwango hiki kwa wahalifu?

Je, hakuna namna nyingine ya kushughulika na wanaodaiwa kuwa ni wageni kwenye maeneo fulani zaidi ya kuwauwa?

Hii ni Tanzania ile ile tunayoisifia kwamba inaongozwa kwa misingi ya sheria?

KIBITI KIBITI KIBITI
MCHEZO WA SINEMA USIOTABIRIKA.
Haya ni mawazo tu lakini ya mjinga mmoja.
una unasaba na wahanga? vifo vya raia wenzako havikuumi? utamkamataje mtu mwenye silaha ya moto? si bure. una ukoo nao.

Sent from my TECNO P5 using JamiiForums mobile app
 
kama majambazi waliouawa ni ndugu zako unakaribishwa katika postmortem halafu ukawazike kwa heshima.

Polisi ikishatangaza vita maana yake hakuna majadiliano ni action tu.

Hapa mtaani kwangu kuna wageni kibao sijaona wakiuawa na Polisi.

Wanaouawa ni Majambazi...na waendelee kuawa tu.
Kweli we jinga lao.
Mjumbe Rose ni wazi kuwa hujui usemalo. Mwulize mtu yeyote hata mtoto atakwambia kuwa mambo kama hayo hayaulizwi wala kujibiwa hazarani labda kama unanusanusa upate fununu uwasaidie wahusika. Endelea kuamini unachoamini, kuwaliwaza magaidi na maadui wa Taifa hili. Uyakapojazinduka utakuta meli ilishaondoka zamani.
 
Hii indiscriminate killings inahitaji international attention! Upinzani achana na kusemea ndani, paza sauti UN, AU, EU etc, vinginevyo tunakwisha.
mbona wale viongozi wanaouawa kibiti hamuwasemei huko UN, AU, na kwa waume zenu EU.

Sent from my TECNO P5 using JamiiForums mobile app
 
Sidhani Kama kuna agizo la kuua mgeni kwenye eneo Fulani huo ni upotoshaji na pili taifa lina intelijensia hivo kuwa trace Hao watu kuwa wametoka kibiti ni kazi ya intelijensia
Na ukiwa mgeni mahali sidhani Kama utapigwa risasi tu hapana utasimamishwa utahojiwa na kuulizwa vitambulisho Ndio utaratibu ila wewe ukisimamishwa ukaanza kukimbia na kurusha risasi lazima utauawa
Watu wanauwawa kila siku....hio intelijensia inakua wap?
 
Mjumbe Rose ni wazi kuwa hujui usemalo. Mwulize mtu yeyote hata mtoto atakwambia kuwa mambo kama hayo hayaulizwi wala kujibiwa hazarani labda kama unanusanusa upate fununu uwasaidie wahusika. Endelea kuamini unachoamini, kuwaliwaza magaidi na maadui wa Taifa hili. Uyakapojazinduka utakuta meli ilishaondoka zamani.

No way, watu lazima wahoji.... tuhoji ndugu !!

Kwa sbb, kwa mfano, hivi mbona kila wanapokabiliana na hawa wahalifu, wanawaua wote si hawa wa Mwanza wala huko Kibiti ??

Sasa watatatuaje tatizo iwapo kila wanayemdhania kuwa ndiye haramia wa Kibiti anakula shaba ??

Kwa, mfano. Kwa hawa wa Mwanza, wangewaua wanne na wawili kati ya wale sita wakawatia mikononi mwao wakiwa hai, wangeeleweka kidogo !!

Lakini kwa mtindo huu wanavyoshughulikia uhalifu wa ujambazi, yeyote mwenye akili huru lazima ajiulize weledi wa vyombo vyetu vya usalama....

Na hii argument ya kwamba, majambazi ndiyo yaliyoanza kuwarushia polisi risasi na kwa hiyo kuamua kujilinda na mwisho wa siku kuua wahalifu wooote kwa kila tukio, ndiyo kabiiiiisa inatia mashaka !!!!
 
Huyu kamanda msangi ana kimbele mbele sana ,natamani apelekwe kibiti atacheza na media mpaka wauaji waishe kabisa,kila anachofanya media anao mkononi.
Ile ya ya magaidi wa mapango ya amboni tanga. KAMANDA MSANGI yeye alikuja na yake ya mwanza , Mizinga ya kuvunjia mawe na mahandaki kuuwa majambazi mwanza(polisi tangu lini watumie mizinga ). advertisement yake tu mtu unajua leo ama zetu ama zao.
naamini akipelekwa kibiti urafiki wake na vyombo vya habari utawamaliza nguvu magaidi.
Haahaa nimecheka mpaka basiiii[emoji23] [emoji23]

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
 
Rose Mayemba wewe binti una matatizo, peleka mgeni nyumbani kwako basi uone kama atapigwa risasi ?
Mmeishiwa hoja hadi mpo radhi kutetea wauaji, hivi kuna raia mwema yoyote anayeweza kurushia polisi risasi kama si jambazi ?

Majambazi wakiua watu Kibiti mnafurahia na kuanzisha nyuzi za kejeli, polisi wakiua majambazi mnaleta nyuzi za maswali ya kijinga kijinga, nyie ni binadamu wa aina gani mnaofurahia mauaji ?
Ni kweli siasa imewatoa hata utu tu wa kuheshimu uhai wa wengine ? Inaonekana amekosekana mtu wa kuwapa muongozo huko ndio maana mnaropoka ovyo ovyo.
Hiili swala la Kibiiti inaonekana ni comedian show zaidi kulliko uhalisia wenyewe!

Kuna kamchezo kanachezwa hapa kati ya Jeshi la Police, CCM na Serkali na pengine kwaa vile Watz ni wavivu wa kufkiri tunaendelea kushabikia huku watu wakiuawa na Jeshii la Policcm! Just ask the Police,TISS and rulling party the following questions:
  1. Kama hawa waliouawa Mwanza ni magaidi tlka Kibiti(Mkoa wa Kipolisi) wametorokaje toka Kibiti na kwa usafirii ganii na njia ipi?
  2. Je, kwa sasa kazi ya Jeshi la Polisi siku hizi ni KUUA tu billa kumkamata mhalifu na kumpeleka Mahakamani?
  3. Je, hawa waliouawa Mwanza ni Majambazi au Magaidi? Je huko Kibiiti Polisi wannapambana na Magaidi au Majambazi???????
  4. Inasemekana walikuuwa na sare za Jeshi, Je, kuna uhsiiano wowote wa sare za Jeshii alizokutwa nazo Manji?ii
  5. Je, nini mtazamo wa Magufuli kuuhsiana na hayo mauajii in conecction wiith KIIBITI as well as UPINZANI?
 
Sidhani Kama kuna agizo la kuua mgeni kwenye eneo Fulani huo ni upotoshaji na pili taifa lina intelijensia hivo kuwa trace Hao watu kuwa wametoka kibiti ni kazi ya intelijensia
Na ukiwa mgeni mahali sidhani Kama utapigwa risasi tu hapana utasimamishwa utahojiwa na kuulizwa vitambulisho Ndio utaratibu ila wewe ukisimamishwa ukaanza kukimbia na kurusha risasi lazima utauawa
MKUU, hawa walisema mwanaume kuvaa hijabu si kosa. wanajua kinachoendelea ndo maana wanawatetea wahalifu. viongozi wasio na hatia wanauawa, hawaona kama ni tatizo. ila wakiuawa wanaume waliovaa hijabu na kukataa kutii amri ya polisi, utawasikia wanalalamika. NI AJABU!!

Sent from my TECNO P5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom