Anaandika Mo Mlimwengu.
Ni hali ya simanzi na majonzi inaendelea ndani ya wilaya ya Muleba na nje ya Muleba. Haki ya kuishi iko wapi? Vyombo vya ulinzi na usalama kazi yake ni ipi? Tumefikia wapi mpaka kufanya Muleba kuifanya kuwa kama machinjio ya binadamu? Hofu inaendelea kutanda kila mahala baada ya kuona vijana watafutaji wanapigwa risasi za moto kwenye vifua vyao kama wawindaji haramu ambavyo huwa wanavyatua tembo.
Kwanini hofu? Hofu inatanda pale ambapo tunakaa kimya na huku ndugu zetu wanazidi kufariki na ambao tulishukuru kuona majeruhi na wao wanazidi kupukutika. Na taarifa inayosambaa ni kwamba wamepigwa kwa sababu shughuli yao kubwa ni kuuza mkaa.
Tuweke bayana tujue mkaa ni haramu, lakini mbona mkaa unauzwa kote na watu wanapata vibali je kama huna kibali adhabu yake ni risasi za moto? Kwanini ukimya unashamiri kwa wale ambao tulitegemea mtueleze kilichotokea. Ni kipi ambacho kipo nyuma ya ukimya wa mauji haya ya kikatili?
Raia zaidi ya saba wamepigwa risasi za moto. Je yalikuwa majibizano ya risasi na kama ni majibizano hao askari kwanini hawajitokezi kuelezea hilo jambo. Na je labda waliuwawa ni majambazi kama ni majambazi porini walikuwa wanafanya ujambazi gani?. Kama ni suala la mkaa kwanini watu wauwawe kwa pamoja kiasi hicho na wengine wadhuriwe kwa majeruhi ya aina hiyo?
Kuna matukio tumeyashuhudia ikaonekana ni katika hali ya kutuliza amani. Je hawa waliuwawa porini kulikuwa kuna amani ipi ambayo imepotea. Je wanapigwa risasi kwa sababu ya kuharibu amani ya wanyama waliopo porini?
Vilio na machozi yametapakaa kila.mahala kwa watu kupoteza ndugu zao na jamaa zao wa karibu. Mmewaua ni kweli, Je hao yatima ni nani atakayewashika mkono, mmesababisha wajane pasipo mapenzi ya mola. Huu ni ukatili uliyopitiliza kwenye jamii zilizostaarabika.
Ukimya utakapozidi kuendelea na huku damu za watu zikimwagika ni laana kwetu wote kwa ambao wameua na sisi ambao tunaendelea kukaa kimya pasipo kujua hatima ya jambo hili.
Rai yangu kubwa kwenye jambo hili lisifichwe fichwe wajulikane waliyofanya haya mauaji ya kikatili na adhabu kali zichukuliwe dhidi yao na kama ikitokea walichofanya ni sahihi basi tujulisheni hao walioua wapewe nishani za heshima.
Mo mlimwengu
Niko juu ya mti