Ni kweli kwamba nisipoenda kuyasafisha makaburi ya wazazi na mababu nitapata laana au mikosi kwenye kazi zangu?

Wachaga wana majibu.kuna shoga yangu ni mkristo mzuri tu ila anasema kila mwaka lazima aende kwao kuchinja mbuzi.asipofanya hivyo mambo hayaendi.kazi haziendi, mikosi kibao.

Hata mwezi 12 alienda wakachinja mbuzi wakafanya mila na kuweka damu pale. Mbuzi wakamla wana ukoo.

Je kama mtu anachinja mbuzi si nakusafisha lazima?
 
Tatizo sio unajisikiaje. Je kuna laana yoyote utapata?
Wakenya wametupita katika kujibu hoja. Huwezi kumkuta Mkenya anajibu hoja bila kujua kiini cha swali na viambata vyake. Sisi wabongo tunajibujibu tu
 
Habari za muda huu!
Kufuatia uzi wa tycoon wa fasihi ndugu ROBERT HERIEL alioeleza sababu za watu wengine kuishi umri mrefu na wengine umri mfupi, kuna nukta alieleza kwamba tunapaswa kuwaheshimu wazazi hata kama mameshakufa! Na akaeleza kwamba tutawaheshimu kwa kutembelea makazi yao( makaburini) na kusafisha kila mara.

Nimeona nichukue nukta hiyo na kuuanzishia uzi ili sote tujadili kwa upana zaidi ili kama ni kweli kuna umuhimu huo, wote tuujue.

Je, ni kweli kwamba tusipoenda kuyasafisha makaburi ya wazazi na mababu tutapata laana au mikosi kwenye kazi zetu ?!

Karibuni
Sio kusafisha tu, hata kuyajengea vizuri ili yasifutike, sio kaburi linaachwa utafikiri alizikwa mbwa , kumbe ni binadamu tena mwenye ndugu wa damu waliohai, tena watoto wake wa kuzaa
 
hii mada inawahusu wanaozika tu ?
sisi tunaochoma kwenye hii mada tunawekwa kundi gani?
 
Hakuna kitu kama hicho! Ni namna ya Wazee wetu kutia mkazo ili kutunza makaburi,kuyasafisha ni jambo la muhimu kwa ajili ya vizazi vinavyokuja.
 
Mtu atakayesema kusafisha makaburi kunasaidia katika kufanikiwa maishani,
Basi inapaswa aukane ukristo wake au uislamu wake.

Kwa mujibu wa mafundisho yao, Mungu pekee ndiye msaada katika maisha.

Sasa akisema kusafisha makaburi kunasaidia maishani, tayari huyo mtu atakuwa amekubali "Mizimu" inasaidia katika maisha kama vile tu Mungu afanyavyo.

Mimi binafsi siamini katika yote hayo!
Ndicho wakoloni wa kizungu na kiarabu walichofanikiwa, tuchukie kila kilichokuwa chetu na kukubali kila kilichokuwa chao, daa, wametuweza kweli hawa mbwa
 
Mtu atakayesema kusafisha makaburi kunasaidia katika kufanikiwa maishani,
Basi inapaswa aukane ukristo wake au uislamu wake.

Kwa mujibu wa mafundisho yao, Mungu pekee ndiye msaada katika maisha.

Sasa akisema kusafisha makaburi kunasaidia maishani, tayari huyo mtu atakuwa amekubali "Mizimu" inasaidia katika maisha kama vile tu Mungu afanyavyo.

Mimi binafsi siamini katika yote hayo!
Hizi dini za kuletewa zisitufanye tukasahau asili yetu.
 
Sio mpaka upate kitu ndio na wewe uyasafishe makaburi yao.

Si ajabu wazaz wako hawajaonja mafanikio yako japo wameplay part kubwa mpaka wewe kufika hapo ikiwemo kukuzaa wewe.

Kusafisha kaburi haichukui siku nzima ama miaka au miezi kama uliyokaa tumboni mwake, ni dakika chache tu. Kwahiyo we fanya kwa upendo tu kama kuna malipo basi nature itakulipa.

Nawasilisha.
 
Kuishi muda mrefu au mfupi hakuna uhusiano wowote na imani za kusafisha makaburi,Bali ni swala LA Nature wengine wataishi miaka mingi na wengine michache.
 
Na mm niliyesawazisha makaburi yote mawili ya wazazi wangu afu nikalima mazao juu yake mnaniweka kundi gan ????? Maqna huwa na limapo mahindi na mihogo 🤕😷
 
Back
Top Bottom