Ni Kweli Jumanne ni Siku ya "Nuksi"?

Ni Kweli Jumanne ni Siku ya "Nuksi"?

kwa nusu ya muda nilioutumia kwa masomo ya shule ya msingi niligundua jumanne napata viboko vingi kuliko siku nyingine ya wiki, nikawa sihudhurii shule siku hiyo kwa kipindi chote cha shule msingi na upili.

huu ni ushuhuda wa kwanza hapa
 
Asante sana, mimi haikua katka mkabala wa ushirikina na wala sijawahi kuuliza kwa mzee yyte yule
labda niweke hivi.....

Siku ya jumanne ni kama siku nyingine katika hali ya kawaida ispokuwa kwa wanaofanya mambo ya kishirikina huwa wanazitumia sana siku za jumanne na jumamosi katika kufanya mambo yao kwani kwa itikadi zao ndio siku ambazo ni nzuri katika kufanya mambo yao yafanikiwe.

Kwa mantiki hiyo ndio maana hata wazee wengi ukitaka ushauri kama kuna uwezekano wa kutokufanya mambo yako (hasa kama unaanza jambo jipya) wanakushauri usifanye katika siku hizo.

Kinachotokea sometime intaokea coincidence mtu kila habari mbaya kwake zinaangukia aidha jumanne au jumamosi ndio anaitakidi hivyo.
 
nimekutana na mama muuza supu analalamika Jumanne hakuna biashara
 
Labda niweke hivi.....

Siku ya jumanne ni kama siku nyingine katika hali ya kawaida ispokuwa kwa wanaofanya mambo ya kishirikina huwa wanazitumia sana siku za jumanne na jumamosi katika kufanya mambo yao kwani kwa itikadi zao ndio siku ambazo ni nzuri katika kufanya mambo yao yafanikiwe.

Kwa mantiki hiyo ndio maana hata wazee wengi ukitaka ushauri kama kuna uwezekano wa kutokufanya mambo yako (hasa kama unaanza jambo jipya) wanakushauri usifanye katika siku hizo.

Kinachotokea sometime intaokea coincidence mtu kila habari mbaya kwake zinaangukia aidha jumanne au jumamosi ndio anaitakidi hivyo.
Mkuu umemaliza kila kitu.......................
 
Imekuwa ikiniathiri sana siku ya Jumanne kutokana na ukweli kwamba imekuwa siku ya bahabti mbaya kwangu haswa matukio mengi makubwa kunikuta siku ya Jumanne likiwemo la hivi karibuni

Jana nimestushwa sana baada ya kijana niliyemsaidia kuandika CV aliponiambia kwamba amepata lazi lakn ameambiwa asianze leo jumaan hadi kesho kwani si siku nzuri

Nilianzisha mjada palepale na kwa kuwa niko uswahilini nilipata majibu yaliyoungwa mkono sana kwa visa mkasa

Kuna ukweli wowote?

Jumanne ndio siku ambazo huwa nikpeleka mzigo sokoni napata hasara sana,mara ya mwisho nilipata hasara kubwa kwenye biashara yangu ambayo sitokuja isahau maishani mwangu...ilikua ni jumanne ya pasaka mwaka huu.
 
cku mbaya ni jumanne na jumamosi ila jumanne zaid.dk mzizi popote ulipo tunakuomba uje huku umalize ubishi
 
YOUR LIKE YOUR CHOICE
images
tuesday_t_shirt-rdb50aec1c3ca42099eec83c7458ca6d7_804gs_324.jpg
 
Siku zote ni nzuri. cha muhimu jikabidhi kwa Mwenyezi Mungu kabla ya mapambazuko ili kuweza kuitawala siku yako, hata kama shetani na makuhani wake wamekupangia mabaya yatashindikana. Usipofanya hivyo lazima utaoparate ndani ya ratiba ya shetani kwani wewe ukiwa umelala fofofo yeye anakupangia siku yako itakavyokuwa. So, kuwa na hulka ya kuiamuru siku yako na kukabidhi mipango yako kwa Mungu kabla ya mapambazuko, usiamke tu kama chizi.
 
Back
Top Bottom