A
Anonymous
Guest
Walimu wa Shule za Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida (Singida DC) tuna malalamiko yetu kadhaa hasa yanayohusu kutolipwa malimbikizo ya fedha za kujikimu kwa muda mrefu.
Tatizo la Malipo
Wengi wetu tumefanya kazi kwa zaidi ya mwaka mmoja tangu tulipoanza kazi mwezi Januari 2025, lakini bado hatujalipwa fedha za kamili za kujikimu.
Katika kipindi hicho wengi kila mmoja tulilipwa takriban TZS 520,000 lakini Walimu wengi bado tunadai kati ya TZS milioni 1.8 mpaka milioni 3.
Inadaiwa kuwa walimu wa Shule za Msingi katika Halmashauri hiyo tayari wameshalipwa, huku sisi walimu wa Sekondari tumeachwa nyuma.
Mara kadhaa Halmashauri imekuwa ikitoa sababu kuwa mapato yake ya ndani ni madogo, hivyo kushindwa kulipa walimu wote kwa wakati wakati tunahisia kuwa huenda fedha hizo tayari zimeshatolewa na Hazina lakini halmashauri inazichepusha na kuzitumia kwa shughuli nyingine.
Kinachotokea sasa ni Walimu tunaishi katika mazingira magumu sana, tunakumbana na madeni yasiyo ya lazima ili kuweza kujikimu na familia zetu.
Watumishi wengi wanaogopa kulalamika rasmi kwa kuhofia usalama wa ajira zao, hasa kwa wale ambao bado hawajathibitishwa kazini.
Walimu tunaomba suala hilo liwekwe wazi ili kuishitua serikali kuu na kuwashinikiza viongozi wa halmashauri kulipa madeni hayo.