KERO Mbulu DC lipeni watumishi hela za kujikimu

KERO Mbulu DC lipeni watumishi hela za kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna watumishi tumemaliza mwaka hatujalipwa fedha za kujikimu. Kuna baadhi wamekuja na hawana mda mrefu wameshalipwa kwani wanalipana kwa kujuana.

Kuna wanaotakiwa kulipwa Tsh 150,000/= na Tsh 130,000/= per day lakini wanakatwa na kulipwa Tsh 80,000/= hiyo nyingine inaenda wapi? Kama sio kuiba pesa ya wanaotakiwa kulipwa.

Badala walipe watu kiasi kinachotakiwa, wanajilimbikizia hela za watu wenye mishahara ya kawaida.

Soma Pia:
Tunaomba OWM TAMISEMI ichunguze suala hili kwa ukaribu zaidi na itoe majibu haiwezekani Halmashauri karibu zote Tanzania nzima ziwe zinalalamikiwa
 
Waambie watalipwa ukute bajeti iliwekwa kidogo au hawakuweka bajeti kabisa..lakin wasiache kufatilia japo kuna viongozi wengine janja janja ni nyingi hao ndo wakula nao sahani moja..Utumishi wa Umma ni kazi ya kujitolea sio sehemu ya kujipakulia minyama hili nalo walizingatie..Kila la heri watumishi.
 
Mimi ni muajiriwa mpya wa Halmashauri ya Mbulu Mji (TC), mpaka leo hatujapewa hela ya kujikimu. Kila tukifuatilia tunaishia kuambiwa majina yametumwa hazina. Kibaya zaidi ni kuwa kuna idara zishapewa, lakini zimepewa fedha isiyokamilifu kulingana na kiwango stahiki.

Tumewauliza walioajiriwa Mwaka jana (2025), hata wao hawakupewa fedha kamili. Sasa tunauliza je hizo hela zingine wanaenda nazo wapi na je watatupa lini?

Halmashauri ya Mbulu Mji, Mkoa manyara
Ajira za January, 2026
Sisi ni Kada ya Afya
 
Back
Top Bottom