Ni kweli Anna Makinda ni 'Mbabe'?

Ni kweli Anna Makinda ni 'Mbabe'?

:nono:mungu ongeza njaa tanzania labda wataelimika"siko la kufa zibuka usikie hizi dawa"
what next..........???
 
Hii naona ni opportunity nyingine nzuri tunapewa na Mungu ya kuwaadhibu mafisadi kutumia sanduku la kura.Huyu Mama mbona ni njia nzuri sana ya kuwaadhibu mafisadi?.Njia za Mungu hazichunguziki,hivyo tungoje.Kuna njia ionekanayo kuwa njema machoni pa binadamu lakini mwisho wake ni mauti.Viongozi wetu wa Imani mbalimbali wameomba Mungu amesikia kilio chetu,hawezi kutuacha.Hii itakuwa ni njia nzuri kufikia malengo ya mabadiliko ya kweli yanayokuja Tanzania.
 
Hivi mayai ya ndege yakiatamiwa,wale watoto wakianguliwa wanaitwaje vile?!
 
mafisadi gani hao waliosherehekea kuanguka kwa 6?
 
Siamini kuwa huyu Anna Semamba Makinda aliyechaguliwa na Wabunge wa CCM kwa kishindo baada ya kuteuliwa na CCM(CHAMA CHA MAFISADI) ameanza kuchemsha hata kabla ya Bunge kuanza rasmi.

Anne Makinda ameanza kuropoka na kuongea hovyo kana kwamba bado ni Mbunge wa kawaida. Inasikitisha sana. Kuna kauli mbili zenye utata ambazo tayari ameshazitoa katika siku hizi mbili. Hebu tizijadili:

  1. Kwamba FISADI ni yule anayeiba WAKE ZA WATU. Siamini masikio yangu kama kweli huyu mama ameongea kwa dhamiri toka moyoni au ilikuwa ni joke! Kama ni joke basi HATATUFAA kwenye nafasi hii ya Spika kwasababu huwezi kuanza kuleta utani kwenye maswala ambayo ni very sensitive kama hili la UFISADI. Hii tayari inaanza kutupa picha na uhalisia wa Spika tuliyenaye. Kama ameshaanza kupindisha maana halisi ya UFISADI ndipo tuanze kujua kuwa huyu mama kweli amewekwa na MAFISADI na tayari ameshaanza kazi ya kuwasafisha mafisadi.
  2. Kwamba katika kuzungumzia UHUSIANO wake na Spika Samwel Sitta kuwa ni kaka yake na anamheshimu na kama kuna mazuri au mabaya yaliyofanyika kwenye uongozi wa Spika Sitta na yeye anahusika. Sawa. Kauli iliyonipa utata mimi ni hiii ya kusema kuwa anamuheshimu Spika Sitta na kama Jina la Sitta lingelikuwemo kwenye orodha ya walioomba kugombea Uspika yeye angetoa jina lake!!!Uongo mkubwa. Kila mtu anajua kuwa Sita alishatangaza mapema kuwa ataendelea kuwania kiti chake cha Usipika na mdiyo maana hata mzee wa Vijisenti Chenge alianza kumrushia makombora Sitta kuwa hafai. Katika majina 13 yaliyopelekwa CC jina la Sitta lilikuwemo,Je mbona hatukumsikia Anne akijitoa kumwachia kaka yake Sitta anayemweheshimu. Na kama Chenge alitupa lawama kwa Spika Sitta kuwa aliliongoza Bunge vibaya basi nayeye Makinda ANAHUSIKA MAANA ALIKUWA NAIBU WAKE kwa hiyo na yeye angewajibika kwa kutoa jina lake lakini haikuwa hivo. Kwa hiyo huyu mama ni mwongo,mzushi na kigeugeu na hii inathibitisha tu kuwa ni kweli akatae au akubali ukweli ni kwamba yeye ametumwa na hao MAFISADI kuwa angombee hiyo nafasi ili kumtibulia na hatima yake kumnng'oa Spika Sita ili MAFISADI wapate nafasi ya kufanya mipango yao ya UFISADI na kuandaa Rais wao atakayekuja 2015.
Kwa hiyo BELIEVE ME,ANNA MAKINDA HATAKUWA SPIKA MZURI WA HILI BUNGE LA 10. YEYE ATAKUWA NI MWANAMKE WA KWANZA KUWA SPIKA NA SPIKA ALIYE MBOVU KABISA KULIKO MASIPIKA WOTE WALIOWAHI KUONGOZA BUNGE LA TANZANIA TOKEA WAKOLONI MPAKA SASA.

Wakti mwingine inabidi watu turudi kwenye vitabu vitakatifu kabla hatujachukua maamuzi. Kweli watu wanazungumzia GENDER ISSUES,GENDER EQUALITY,etc. Usawa na upuuzi mwingine kama huo. Lakini hebu tuwe wa kweli wa kusema;call a spade a spade and not a big spoon. Biblia inasema SIMPI RUHUSA YA MWANAMKE KUMTAWALA MWANAMME.Yes,I like this. Utasema oh,mfumo dume,oh unyanyasaji wa kijinsia etc,etc.Lakini ukweli utasimama. Mwanamke hapashwi kuongoza wanaume,NEVER! Hiyo ni Biblia,Huyo ni Mungu. Anayepingana na hilo ataona matokeo yake. CCM kimetufikisha hapo kwa kisingizio cha kijinga kabisa! Kwamba ati tangu tupate uhuru nchi yetu haijawahi kuweka mwanamke kwenye mojawapo ya mihimili 3 ya nchi! Ebo,yaani all thise years mlikuwa wapi,mmekuja kuzinduka kwenye kiti cha Usipika 2010 kuwa ndiyo awe mwanamke. Basi na Waziri Mkuu 2010 awe mwanamke na Rais wa 2015 wekeni mwanamke halafu mtaona muziki wa kinamama kuendesha nchi!! Hivi kwanini mnafikiri Mungu amekataza wanawake wasiwatawale wanaume? Kwanini wanawake hawaruhusiwi kuwa Wachungaji au Mapadre?Je, kuna mwanamke anaweza kumuweka mwanamme mimba?? Show me one. Watu wanatafsri vibaya kuhusu hii lugha ya usawa. Ni katika maeneo fulani fulani tu siyo kuwa mwanamke anaweza kufanya kila jambo. Kuna mambo wanawake hawayawezi na hawatakaa wayaweze hata siku moja!Maumbile yao proves what they are. Biblia ina sema kuwa KAENI NA WANAWAKE KWA AKILI MAANA NI VIUMBE DHAIFU.That is the Bible. Kiumbe dhaifu unakipa kuongoza mhimili wa nchi kama Bunge,what do you expect?Sitaki kuingia sana into details kuhusu hayo lakini is a big discussion forum.

Mbona JK hakuanzaia kwake kwa kujitoa kwenye kugombea Urais akawaachia mwanamke ili awe Rais wa kwanza mwanamke? Kwanini Mwanamke aanzie kwenye Bunge kama siyo ilikuwa janja ya kumwengua Sitta.
Matokeo yake hayako mbali sana mtaanza kuyaona muda si mrefu.

CCM msifikiri Watanzania tunadanganyika kwa upuuzi wenu huu mnaowafanyia. Anne Semamba Makinda tuna uhakika AMEWEKWA KWA AJILI YA MASLAHI YA MAFISADI n akuna gazeti leo limeandika kuwa MAFISADI WAMEKUNYWA POMBE KUSHANGILIA KUONG'OLEWA KWA SPIKA SITTA.

Iko siku CCM mtakuja kulipia uhuni mnatufanyia Watanzania.

Wasaalamu.

Mtake msitake, ukweli ndio huu.

Zoezi la kuhakikisha MAFISADI wanaendelea kupeta lilianzia kwenye kura za maoni CCM. Pesa nyingi sana iliandaliwa kuhakikisha kwamba idadi kubwa ya wabunge ambao (ndani ya CCM) walikuwa mwiba kwa mafisadi waliondolewa. Ushahidi wa jinsi kura zilivyoibwa upo, na ulipelekwa NEC ya CCM, kama Makamba alivyoagiza, lakini hakuna kilichofanyika. Kauli ambayo haikutarajiwa - kutoka kwa mtu ambaye ninamheshimu sana - Mzee wetu, Alhaji Mwinyi, kwamba "tusiwachagulie wananchi viongozi, walioshinda ndio hao hao wapite" ilinisikitisha sana. Wananchi HAWAKUWACHAGUA viongozi, bali walichaguliwa kwa NIABA YAO. Hujuma zilifanywa na viongozi wa CCM katika ngazi za Wilaya. Hili liliandaliwa rasmi ili kuhakikisha kwamba Wabunge "mavuvuzela" (ambao hawatakuwa na ubavu wa kuipinga CCM, kutokana na kuwa na upeo mdogo na elimu duni... wapo wengi wa Darasa la Saba, lakini wameapa kwamba wao ni wa Sekondari!) ndio wanaoingia Bungeni ili kuondoa upinzani ndani ya bunge, hoja zitakazopelekwa pale ziwe za kuunga mkono, si kuupiga ufisadi!

Kwa upande wa Spika, Sitta, ambaye amedhihirika kuwa shujaa dhidi ya ufisadi, aliondolewa mapema ili asirejee bungeni kuendeleza kile alichokifanya. Sitta alionekana dhahiri kuwa mwiba kwa CCM kwa kuwa alitetea hoja dhidi ya ufisadi, kama vile kashfa za Richmond, EPA, Buzwagi, Meremeta, n.k., nyingi ambazo zililetwa bungeni na kambi ya upinzani.

Kambi ya upinzani isitarajie kupata mtu wa kuisaidia bungeni, kwani Makinda si mpiganaji dhidi ya ufisadi. Amewekwa pale kutetea ufisadi, na atafanya kazi yake ipasavyo. Tayari ameanza.

Jenerali Ulimwengu aliandika "Ukichagua hovyo, ukatendewa hovyo, usiseme hovyo!"

Walioichagua CCM waendelee kulia kimya kimya. Msilalamike. Mlipokuwa mnaishabikia HAMKUYAJUA HAYA?

2010 TUTAFANYA KWELI ZAIDI! MMETUIBIA, HATULETI RABSHA kwa kuwa tunapenda amani!

-> Mwana wa Haki
 
huyu ma ma ni debe tupu!!
kwanza hana staha, pili ikumbukwe kwamba anaishi bila haya!!
akili yake ina 20% ya utulivu na 80% ya upayukaji, kuliko kufikiri
bado tutaendelea kusikia mengi mobovu, machafu, na yasiyofaa
kabisa kutua masikioni mwa mtu mwenye akili timamu
 
Kwa upande wa kidini mwanamke yeyote anaekimbilia kuwa na mamlaka juu ya wanaume huyo anajulikana kama Yezebel. Yezebel ni mwanamke aliyejiweka juu ya watumishi wa Mungu kwa kumpiku mmewe Ahabu aliyekuwa mfalme wakati huo. Huyu spika tuliye naye sasa hana tofauti na Yezebel na kibaya zaidi kawekwa pale na kundi lililojiapisha kudhulumu haki ya wanyonge (mafisadi) na tayari kashaanza kuwazuga wananchi kuhusu maana ya fisadi tofauti na jinsi walivyowapa jina hilo wezi wa hazina ya taifa. Kuhusu usawa wa kijinsia, haiingii akilini kunyanyasa kijinsia kwa maana ya kutibu unyanyasaji kijinsia. Sita hakuondolewa katika nafasi yake kwa kushindwa kuimudu bali ameondolewa pale kwa sababu moja tu kwamba yeye ni mwanamume. Huu ni unyanyasaji wa kijinsia wa kiwango cha juu kabisa. Kama sivyo basi kauli za makamba kuhusu kuondolewa kwa Sitta zifutwe. makamba amekuwa akitumiwa na mafisadi ya ccm bila yeye kujitambua na amekuwa akitoa kauli zenye utata zinazozihirisha kuwa elimu yake ni ndogo na hivyo ni vigumu kwake kupambanua kip ni kipi. Sasa hivi nimepoteza imani na bunge kwa asilimia 85 unless otherwise!
 
Kumradhi mapema kaka. But this is id!otic. Re-read your post again. Who are you now, a prophet?

Hivi kwenye uzi wake huu ni wapi katabiri chochote..........alichofanya ni kutoa maangalizo ya kimsingi kabisa.........
 
Kwa upande wa kidini mwanamke yeyote anaekimbilia kuwa na mamlaka juu ya wanaume huyo anajulikana kama Yezebel. Yezebel ni mwanamke aliyejiweka juu ya watumishi wa Mungu kwa kumpiku mmewe Ahabu aliyekuwa mfalme wakati huo. Huyu spika tuliye naye sasa hana tofauti na Yezebel na kibaya zaidi kawekwa pale na kundi lililojiapisha kudhulumu haki ya wanyonge (mafisadi) na tayari kashaanza kuwazuga wananchi kuhusu maana ya fisadi tofauti na jinsi walivyowapa jina hilo wezi wa hazina ya taifa. Kuhusu usawa wa kijinsia, haiingii akilini kunyanyasa kijinsia kwa maana ya kutibu unyanyasaji kijinsia. Sita hakuondolewa katika nafasi yake kwa kushindwa kuimudu bali ameondolewa pale kwa sababu moja tu kwamba yeye ni mwanamume. Huu ni unyanyasaji wa kijinsia wa kiwango cha juu kabisa. Kama sivyo basi kauli za makamba kuhusu kuondolewa kwa Sitta zifutwe. makamba amekuwa akitumiwa na mafisadi ya ccm bila yeye kujitambua na amekuwa akitoa kauli zenye utata zinazozihirisha kuwa elimu yake ni ndogo na hivyo ni vigumu kwake kupambanua kip ni kipi. Sasa hivi nimepoteza imani na bunge kwa asilimia 85 unless otherwise!
Makamba anatambua waziwazi kuwa anatumiwa na mafisadi. And he likes it just fine that way.
 
Kwa hiyo BELIEVE ME,ANNA MAKINDA HATAKUWA SPIKA MZURI WA HILI BUNGE LA 10. YEYE ATAKUWA NI MWANAMKE WA KWANZA KUWA SPIKA NA SPIKA ALIYE MBOVU KABISA KULIKO MASIPIKA WOTE WALIOWAHI KUONGOZA BUNGE LA TANZANIA TOKEA WAKOLONI MPAKA SASA.

AU ni yaha maoni yanayokusukuma kumwaga haya:-

Kumradhi mapema kaka. But this is id!otic. Re-read your post again. Who are you now, a prophet?
 
Bila shaka mama Makinda ataweza.Ataweza kwa kiwango gani, ndo swali. Lazima atakuwa na majibu ya maswali yote; iwe kwa mkato au kwa kirefu, nk,lazima ataweza. Ataweza kwa mtazamo wa nani pia itategemea nani anafanya tathmini. Mwaka huu-2015, ipo kazi
 
any way , tusimpuuze huyu mdau nae inawezekana ana aikli

ndugu zangu, najua sote tumeumizwa sana na padri Slaa kutokuwa raisi, juhudi za maaskofu na wana mtandao wengine wa kanisa waliojivika kofia za wanaharakati wa demokrasia hazikusaisia, ifike wakati tuache jazba tuwe wazalendokwani kura zimeamua

hiviiiiiii kwani Biblia ina ruhusu kuiba wake za watu? au tulipo fungua tu ukurasa ulio funguka uliandika kwamba mwanamke hafai kuwa kiongozi,, na tumsaidie mwenzetu juuu ya kazi za spika kama yeye ni mtawala au kiongozi wa bunge, na kama ni kiongozi basi quotation zaka za Biblia hapa hza apply kwani anaekemewa na Mungu ni mwanamke anae watawala wanaume

aaaaaa bana tunatia aibu,,, hivi nani asie jua kuwa kampeni za chadema zilifadhiliwa na Alex Massawe, lile jambazi la Moshi, nani asiye jua fedha za kuendeshea Chadema zinatoka kwa ufulisi na uhujumu uchumi uliofanywa na viongozi waandamizi wake wa akina mzee MTEI,, ANY WAY TUANGALIE TULIKO JIKWAAAIYA SIO TULIPOANGUKIA

TUACHENI UTABIRI WA KINA SHEIKH YAHYA

TUMUACHENI TUMUONE

Jordan! Nonesense.
 
:nono::nono::nono::nono: hapo mkuu unaleta siasa za kwenye vijiwe vya kahawa sasa...
 
jordan are sure kwmba Dr Slaa alitumwa na kanisa au wewe unataka kudhoofisha nguvu ya harakati za kuikomboa nchi yetu? Kweli wewe ni raia wa hii nchi? ukiendelea na mtazamo wako kama huu kwa kifizikia tuna sema rate ya kuchakaa fikra zako itakuwa ina tripple after every 1 year ambapo utakuwa una umuhimu tena kwa jamii.
 
Kumradhi mapema kaka. But this is id!otic. Re-read your post again. Who are you now, a prophet?

Hizi ni dalili tu za awali. Huyu mama kawekwa kuwakingia kifua mafisadi si kuongoza bunge. Tutashuhudia ngumi maana atajidai kuleta usanii kwenye jumba la sanaa na 'wanaume' hawatakubali.
 
Kwa upande wa kidini mwanamke yeyote anaekimbilia kuwa na mamlaka juu ya wanaume huyo anajulikana kama Yezebel. Yezebel ni mwanamke aliyejiweka juu ya watumishi wa Mungu kwa kumpiku mmewe Ahabu aliyekuwa mfalme wakati huo. Huyu spika tuliye naye sasa hana tofauti na Yezebel na kibaya zaidi kawekwa pale na kundi lililojiapisha kudhulumu haki ya wanyonge (mafisadi) na tayari kashaanza kuwazuga wananchi kuhusu maana ya fisadi tofauti na jinsi walivyowapa jina hilo wezi wa hazina ya taifa. Kuhusu usawa wa kijinsia, haiingii akilini kunyanyasa kijinsia kwa maana ya kutibu unyanyasaji kijinsia. Sita hakuondolewa katika nafasi yake kwa kushindwa kuimudu bali ameondolewa pale kwa sababu moja tu kwamba yeye ni mwanamume. Huu ni unyanyasaji wa kijinsia wa kiwango cha juu kabisa. Kama sivyo basi kauli za makamba kuhusu kuondolewa kwa Sitta zifutwe. makamba amekuwa akitumiwa na mafisadi ya ccm bila yeye kujitambua na amekuwa akitoa kauli zenye utata zinazozihirisha kuwa elimu yake ni ndogo na hivyo ni vigumu kwake kupambanua kip ni kipi. Sasa hivi nimepoteza imani na bunge kwa asilimia 85 unless otherwise!

Mbona unamtetea kwa kisingizio cha ujinga (ignorance)? Hivi huoni kwamba, pamoja na uropokaji wake, Makamba anao ufahamu kamili ila, kama wengi ndani ya CCM, ameamua kuweka hadhi na heshima yake matopeni almuradi anawafurahisha wanaomdondoshea makombo? Hiyo ndiyo tragedy kubwa iliyoletwa na chama hicho nchini; watu wazima na fahamu zao kuwa ni mienendo dhalili!
 
Nauliza vile viti pale mjengoni ni moveable maana naona dalili ya kurushiana viti, viatu nk. Unategemea nini pale akitokea Mnyika kuhoji utendaji wa serikali, na pale Tindu akiwasilisha hoja binafsi kuwa tume ya uchaguzi inalinda ccm, na Mustapha akihitaji ufafanuzi washeria juu ya ulipaji kodi unaofanywa na wachimbaji wa madini halafu ukasikia jibu mheshimiwa kaa chini huna data???????? nini kitatokea makinda akitoa majibu ya ubababe kama hayo, nionavyo utasikia fuuuuuuuuuuuuu puuuuuuuuuuu kiti kimetua juu ya kichwa cha mtu. lakini mm simo humo:yield:
 
Back
Top Bottom