Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,930
Sikutegemea huyu mama kusema maneno haya kwa wakati huu, hasa akiwa amechaguliwa kama speaker wa bunge. Hili linanipa shaka katika ufanisi wake wa kazi, kwani ameanza vibaya kwa kutumia siasa za maji taka.
Wote tunajua kuwa suala la kuongelea kuhusu 'wizi wa mke wa mtu' ni nini na linamlenga nani. Hizi ni siasa za maki taka. Ni maji taka hayohayo ambayo yalitumiwa na viongozi wa ccm dhidi ya Dr. Slaa wakati wa kampeni za uchaguzi. Kwa hili tunaweza kusema kweli kama atafanya kazi yake vizuri? La hasha! Leo hii hakuna haja ya kutafuta maana ya neno 'fisadi'. Kila mtu anajua hata mtoto wa darasa la 3 anajua.
Kwa kutamka hivyo hadharani, ameuhakikishia umma wa Kitanzania kuwa amewekwa pale kuetetea hoja za mafisadi, hakuna mjadala zaidi. Kama yeye alikuwa halijui hilo, basi imeliwa kwake! Sikuwa na imani na utendaji wa ccm tangu mwanzo, lakini hii imeniongezea kutokuwa na imani na Anna Makinda kama Speaker anayefaa.