Ni kweli Anna Makinda ni 'Mbabe'?

Ni kweli Anna Makinda ni 'Mbabe'?

Nimepima kauli za Spika mpya Mheshimiwa Anne Makinda na kugundua silaha anayoitegemea kuzima mijadala bungeni ni kifungu cha 90 (13) ambacho kinasema kauli ya spika ni ya mwisho anapoamua kufunga mijadala bungeni...................Kifungu hicho hicho ndicho kilitumiwa na Spika mstaafu Samweli Sitta kuzuia mjadala wenye masilahi makubwa kitaifa wa Richmond........................

Swali la Tundu Lissu lilipaswa lijibiwe kabla ya kura ya kumthibitisha PM lakini Spika akaamua kulihairisha hadi baada ya uchaguzi na akalijibu visivyo huku akilikumbusha Bunge mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 90(13)............huo siyo uongozi wa pamoja ambao Spika aliuahidi hata kidogo.........Ni ubabe tu........

La msingi swali la Lissu lilihusu kanuni za uendeshaji wa Bunge kulingana na kifungu cha 53 (a)-(c) ambavyo kwa pamoja vimebainisha ya kuwa mijadala inayoanzishwa na serikali lazima itoe nafasi kwa kiongozi wa upinzani kutoa kauli yake...........

Hili halikufuatwa kwenye uteuzi wa kura ya kulithibitisha jina la PM......na Mheshimiwa Tundu Lissu aliomba ufafanuzi ambao Mheshimiwa Spika alighaili kuutoa bali aliahidi kuutoa baada ya kura kupigwa na matokeo kusomwa na PM kupewa muda wa kushukuru ndipo Spika alirudia kuishughulikia hoja ya Mheshimiwa Tundu Lissu......................

Tatizo hapa ni kuwa Spika hakutoa umuhimu kwa hoja ya Mhe. Lissu kujibiwa kabla ya kura tajwa.........kwani kama utaratibu ungebainika umekosewa yaamanisha ya kuwa zoezi zima la kura lingerudiwa ukiachilia mbali majibu ya Spika aliyoyatoa baadaye kukosa mashiko katika kubeza hoja tajwa...........haya ni matumizi mabaya ya wakati...


Spika alijitetea ya kuwa serikali haipo kwa kuwa baraza la mawaziri halijaundwa.......What a nonsense......lakini hoja ya uteuzi wa PM ilitoka serikalini sasa ilikuwaje aikubali kuipokea na kuifanyia kazi kama Raisi na Mwanasheria Mkuu bado siyo serikali?........................tukumbuke ya kuwa hata baada ya bunge kuvunjwa serikali hiyo hiyo ilituambia bado yenyewe ipo kazini sasa sijui ni lini Mheshimiwa Spika aliivunja hiyo serikali...............

Ukiachia mbali hilo, Mheshimiwa Spika alitafuta kuegemea kwenye kanuni nyingine ambayo inagongana na kanuni ya 53(c)....kiutaratibu huwezi ukaikuza kanuni moja kwa kuziathiri haki ambazo tayari zimekwisha kutolewa na kanuni nyingine isipokuwa kama kuna kanuni inayoelekeza hivyo.........yaani haki zilizotolewa na kanuni moja huwezi ukazififilisha kwa kutumia kanuni nyingine...........................pengine kwa Mheshimiwa Spika kwa vile ni mbumbumbu wa sheria ndiyo maana ameshindwa kuona ukweli huu..................na ndiyo maana maombi ya Mheshimiwa Anne Kilango Malecela ya kuua mjadala wa kulithibitisha jina la PM aliupa uzito kinyume na sheria za kuliongoza bunge hilo.......hususani ukizingatia ya kuwa ni maombi ya mbunge wa CCM dhidi ya haki za Kiongozi wa upinzani kutoa maoni yao......CCM hawana sababu ya kuwapunguzia wapinzani hakl zao za kimsingi za kutoa maoni ambazo wamepewa na kanuni......


Mwishowe Spika alipoona hoja zake binafsi za utetezi hazina mashiko akakimbilia kuficha makosa yake kwenye kifungu cha 90(13) kuwa kwa vile alikwisha kufunga mjadala tajwa basi uamuzi wake ni wa mwisho........................

Hilo lilikuwa ni kosa..............udikteta kamwe hautafanikisha malengo ya Spika mpya kuleta maelewano bungeni....................But what do we expect from a political party that came to power through a backdoor? We should expect more of the same...................dhuluma on top of dhuluma to continue besieging this otherwise great nation.......
 
Huko mbele ya safari hali ya huyo bibi itakuwa mbaya zaidi endapo asipopunguza ubabe.
Ningekuwa ni mshauri wa Ana Makinda ningemshauri asiwe anazungumza kiingereza kwani mh!
 
The so called speaker hafai , nyota njema hounekana asubuhi
 
Huko mbele ya safari hali ya huyo bibi itakuwa mbaya zaidi endapo asipopunguza ubabe.
Ningekuwa ni mshauri wa Ana Makinda ningemshauri asiwe anazungumza kiingereza kwani mh!

Ninakubaliana na maoni haya............
 
Yale maswali ya Lisu yalikua mtego sana kwake ndo maana akavuta pumzi ili apate madesa ya kumsaidia. Wapiganaji wa CHADEMA wameonyesha wapo makini sana. Kama swali la mnyika hakulijibu inavyotakiwa alienda nje ya swali kwa sababu ya jazba aliyokua nayo. Zile karatasi zilikua na serial no sasa yule aliekua anagawa zile karatasi baadae anaweza kujua kua mnyika alimpigia kura nani kwa sababu aliiona serial no ya mnyika wakati anagawa zile karatasi. pia unaweza kua mchezo wameucheza kwa kugawa serial no kutokana na vyama na hapo ndo inaweza kuwarahisishia kuwagundua wana CCM ambao wamewasaliti. Yule mama amejibu bila kuangalia msingi wa swali ulikua vipi. Asidhani wananchi hatuoni hapo tume note tutaonana kwenye hukumu yao 2015

Nakubali mkuu nafikiri tatizo ni pale mpiganaji aliposema "karatasi zimetwanywa zikiwa na unique serial Number" na mama akafikiri number imestand badala ya jina la mteuliwa.

Huyu ndio speaker wetu
 
Lakini kila kitu kina mwisho Anna ana mwisho pia. She is unsuitable for that high and sensitive post siyo kwa wabunge tu bali kwa taifa zima.
 
Pia kama wanajua serikali haipo hicho kifungu wamekiweka cha nini na hali wakijua waziri mkuu anachaguliwa kabla ya serikali kuundwa, na lini serikali ilivunjwa wakati wale waliokuwepo tunawasikia bado ni mawaziri .

Za mwizi ni 40 zikifika hakuna discussion na anaye kamatwa na ngozi ndiye mwizi

mzee gomezi
 
Jambo jema ni kwamba sura halisi ya Anna Makinda itajitokeza muda si mrefu. jinsi alivyohangaika kutafuta msaada baada ya hoja ya Tundu Lissu, inaonesha kwamba kazi anayo. hii itampunguzia confidence, maana huwezi siku zote ukategemea tu kujificha katika rungu la spika. hii itampeleka katika udikteta uliokithiri, ambayo itawapa nafasi CHADEMA, baada ya kuwasilisha hoja nzito na kupingwa kwa udikteta ama wa wingi wa wabunge wa ccm, au rungu la spika, kupeleka hoja kwa wananchi. na hii itaturejesha katika ule mzunguko wa Mwembeyanga, ambapo ililazimu JK atume mawaziri wake nchi nzima. alternative ni kwa wabunge wa ccm kuungana na wa upinzani katika hoja mbalimbali za msingi, ili kuepuka kuonekana wapo kinyume na maslahi ya taifa, kama walivyokuja na hoja ya wabunge wanaopambana na ufisadi. it will be very interesting to watch!
 
Kama uliangalia bunge ijumaa, utakumbuka makinda alionesha waziwazi upendeleo kwa ccm katika kila jambo lililokua likiwekwa mbele. Majibu yake yalikua ya kujibishana, ya kuonesha ubabe, kulazmisha ukubwa (mfano kuna pahala alimwambia Mgombea uspika wa CHADEMA alipokua anajilinda kwa kanuni X asijibu swali Y, alisema kwa kukaripia..."kanuni nazijua mimi, wewe jibu swali), na hata alisubutu kutoa majibu kwa 'tone' za ukali (mithili ya mama kwa mwanae) pasi na sababu. Kama vile anataka kufikisha meseji kwamba YEYE ni tofauti na U-SITA..... Wadau, impression yenu ni ipi... ukizingatia ilisemwa 'first impression, last impression! Mi namwona akijiuzulu baada ya miezi kadhaa....akishurutishwa na emotions zaidi ya hoja!
 
Mimi pia niliiona hiyo hali, nahisi kama anaendesha bunge ki'mama na mwana', as if amewakamia kambi ya upinzani. Napata hofu na kauli aliyokuwa ameitanguliza mwanzo kuwa ataendesha kimtindo wa 'no research no right to speak', vitu vinaweza kupaishwa kwa misingi ya kuwa havijafanyiwa research! Anyways, safari ni ndefu bado lets wait for a proper session ndio tutaweza ku-judge uendeshaji wake, tusije tukaanza kulaumu mapema.
 
No, asiendeshe bunge kama darasa la vidudu, hawa ni watu wazima wametumwa na wapiga kura wao na wananchi kwa ujumla kuwakilisha maoni ya wananchi, tunajua iko wazi anatetea maslahi ya mafisadi ambao wameanza kuwania urais 2015 kiaina.
Nina hakika nitafika pahala bunge litalipuka na litamshinda aendeshe bunge kidemokrasia.:nono:
 
tatizo amekamia kuwanyamazisha wabunge pinzani, unaweza ukaona waziwazi hizi siku mbili tatu za bunge, halafu kingine anataka kuendesha bunge kama anaendesha familia yake, mama anagombeza watoto..
 
No, asiendeshe bunge kama darasa la vidudu, hawa ni watu wazima wametumwa na wapiga kura wao na wananchi kwa ujumla kuwakilisha maoni ya wananchi, tunajua iko wazi anatetea maslahi ya mafisadi ambao wameanza kuwania urais 2015 kiaina.
Nina hakika nitafika pahala bunge litalipuka na litamshinda aendeshe bunge kidemokrasia.:nono:
Ukiwa na wabunge wanao behave kama watoto wa chekechea unatakiwa uwa handle vipi? She was right and firm - Tukubali kukosolewa kila taaluma ina sheria na misingi yake, Spika ndani ya Bunge ni Mmoja tu!:A S angry:
 
Ukiwa na wabunge wanao behave kama watoto wa chekechea unatakiwa uwa handle vipi? She was right and firm - Tukubali kukosolewa kila taaluma ina sheria na misingi yake, Spika ndani ya Bunge ni Mmoja tu!:A S angry:

Siku zote Wabunge wa CCM ni zaidi ya Chekechea. Subu!!
 
Ukiwa na wabunge wanao behave kama watoto wa chekechea unatakiwa uwa handle vipi? She was right and firm - Tukubali kukosolewa kila taaluma ina sheria na misingi yake, Spika ndani ya Bunge ni Mmoja tu!:A S angry:


Pole sana kwa hoja yako pofu.Ulisikiliza au kuangalia lakini maswali yenyewe na majibu yake? au unakurupuka tu. Naamini hukuangalia au kama uliangalia hukuweza kuona.Hoja ya kwanza ilikuwa ya Mnyika, alihoji juu ya dhana ya usiri katika kumpitisha Waziri Mkuu (kama ilivyo kwenye kanuni za Bunge za 2007) akaomba muongozo kwa mujibu wa kanuni ya 64 juu ya wabunge kupewa karatasi zenye namba ambazo kwazo, aliyegawa anaweza kuwa na mkakati wa kujua namba fulani kapewa fulani na hibvyo kura yake fulani ni ya ndio au hapana. Mama yetu hakuelewa swali kama kawaida yake akakurupuka kujibu mambo ya jina la Waziri Mkuu mara mtambo uliprint haraka mara kuna wawakilishi wa vyama wameenda kuhakikisha upigaji kura nk. Jibu kamili kuhusu namba hizo zinavyoweza kutunza dhana ya usiri imekosa hata sasa muongozo wa Spika.

2. Tundu Lissu akaibua hoja ya kwamba kanuni zinataka hoja ya Serikali ijadiliwe kwanza na kambi ya upinzani kabla ya mjadala. Kwanza mama akaona swali lilikuwa gumu akaahirisha kulijibu (na baada ya vikao vizito ikiwemo cha Sitta na AG mama akasaidiwa baadhi ya majibu ambayo hata hivyo naye akayachakachua). Jibu lake likawa kwamba kanuni aliyoisoma Lissu (naye akairudia kwa kupotosha tafsiri) inasema iwapo kuna hoja ya Serikali lakini akafasiri kuwa kwa sasa "hakuna Serikali" Huu ndio muongozo wa Spika kuwa Bungeni hakuna Serikali wakati yupo Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyewasilisha hoja husika ya Serikali. Kimsingi mama ametoa muongo wa ajabu zaidi wa Spika katika karne hii katika hili na akatupa hoja hiyo pia kwa kueleza kuwa kuna kanuni suala likishaamuliwa na spika halipaswi kurejeshwa tena kwenye mjadala.Katika hili moja ni kweli kwamba Lissu kwa kanuni ile labda hakuijua, hakupaswa kuuliza (alichelewa), lakini mama naye akavunja kanuni kwa kutolea mwongozo (kwa kuchakachua) suala ambalo alishalitolea uamuzi.

Tatu ni pale Lohay Akonay aliyekuwa akiwania nafasi ya unaibu spika alipoulizwa swali na Stella Manyanya kuwa anaombaje nafasi hiyo wakati chama chake hakimtambui Rais, msimamo wake kuhusu hilo ni upi. Lissu akasimama na kuomba mwongozo katika katika ya 64 inayosema

64
.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katiba
yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika
Bunge, Mbunge:-
(a) (b) hatazungumzia jambo ambalo haliko kwenye
mjadala
;

Na akisherehesha Lissu alisema suala la matokeo ya Urais na uchaguzi si sehemu ya mjadala pale Bungeni. Mjadala wa Bunge ni uchaguzi wa Naibu Spika ambao sifa zake zimeainishwa kwenye katiba ya nchi na hakuna mahali sifa hizo zinapohusishwa na masuala ya uchaguzi wa Rais.

Lo mama bila kuizingatia hoja akaripuka na kumdakia Lissu kuwa hata yeye kavunja utaratibu kwa kuingilia uhuru wa mwenzake (nadhani alimaanisha muuliza swali) lakini hapa sikuuelewa mwongo huu wa Spika ulimaanisha nini kisha akaendelea tena kwa jazba kumtaka Akonay ajibu swali husika. Da, acheni nipumzike jama, miaka mitano hii ni ze comedy.



 
Hata kama kweli wabunge wana behave kama chekechea si busara kuwananga ki umama na mwana. Alichotakiwa na anachotakiwa kufanya ni kuwachukua kama watoto kisha yeye ajibu kwa kufuata sheria na taratibu na hata kuonesha heshima. Hekima ya mtu ni pamoja na kupuuza mawazo ya kitoto na kuyapa majibu kiungwana. Hata nchi za wenzetu ambazo wamepoteza amani na wanabutuana kila siku ni kwa sababu majibu ya kitoto yalitolewa kwa wanao behave kama watoto lakini ni watu wazima tena wenye ridhaa ya wananchi. Kwa kweli mimi nadhani busara inahitajika sana katika kutoa majibu bungeni kwa wabunge wote bila kujali huyu ni wa chama changu, ni mpya bungeni au ni wa chama cha upinzani. Toa fursa sawa. Cheki Spika wa 2005-2010 alitoa fursa sawa na hata pale ambapo ililazimu wanachama wa chama chake kuaibishwa. Kama mtu amefisadi weka peupe wote wajadili bila kujali chama. Kama mtu amefanya jambo lisilostahili kwa jamii, bunge lijadili bila vitisho. Je kwa mwendo huu, huyu aliyepo ataweza kuvumilia wa chama chake kubananishwa kama zama za Kabla yake. NAMPENDA S. SITA!
 
Jambo jema ni kwamba sura halisi ya Anna Makinda itajitokeza muda si mrefu. jinsi alivyohangaika kutafuta msaada baada ya hoja ya Tundu Lissu, inaonesha kwamba kazi anayo. hii itampunguzia confidence, maana huwezi siku zote ukategemea tu kujificha katika rungu la spika. hii itampeleka katika udikteta uliokithiri, ambayo itawapa nafasi CHADEMA, baada ya kuwasilisha hoja nzito na kupingwa kwa udikteta ama wa wingi wa wabunge wa ccm, au rungu la spika, kupeleka hoja kwa wananchi. na hii itaturejesha katika ule mzunguko wa Mwembeyanga, ambapo ililazimu JK atume mawaziri wake nchi nzima. alternative ni kwa wabunge wa ccm kuungana na wa upinzani katika hoja mbalimbali za msingi, ili kuepuka kuonekana wapo kinyume na maslahi ya taifa, kama walivyokuja na hoja ya wabunge wanaopambana na ufisadi. it will be very interesting to watch!

Point taken............
 
Ukiwa na wabunge wanao behave kama watoto wa chekechea unatakiwa uwa handle vipi? She was right and firm - Tukubali kukosolewa kila taaluma ina sheria na misingi yake, Spika ndani ya Bunge ni Mmoja tu!:A S angry:

Nadhani...haya ni mawazo mgando yaliyotiwa chachu.. si ya uzuri, bali chachu ya uharibifumbumbumbu wa kutotambua kinacho-exist kinamaana gani.... Ni ushabiki upofu, unaoendekeza kukubali mambo yalivo badala ya kuipa fikra nafasi ya kujaribu! Uoga wa kuthubutu kuruhusu fikra na maisha nje ya kibox, na si kwamba umeridhika kukaa humo.... Ukidhani ukitoka hutapata na ukitaka kurudi utakuta mlango umefungwa..... huwezi hata kuyaelewa haya!!!
 
Thankx God Its Friday! Wana JF nimekua nikifuatilia siku ya jana pale bungeni dodoma wakati muheshimiwa Raisi wa jamuhuri ya muungano wa TZ akiwa anasubiriwa kutoa hotuba yake Ndeeeeefu mpaka nilifikia wakati sikua namuelewa tena! Lakini hoja ninayoileta hapa kuhusu Spika wa Bunge ndugu Anna Makinda wakati anamkaribisha Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete aliweka neno moja na lenye msisitizo mkubwa tu kua tunamkaribisha muheshimiwa Raisi aliyeshinda kwa KISHINDO KIKUBWA!! eti alikua anamaana gani kutoa msisitizo kama ule kweli Anna Makinda ni spika mwenye maslahi ya Bunge na wananchi au ni kwa manufaa ya watu wachache walimuweka pale?? Naweka hii hoja mbele yenu the GREATY THINKERS!!
 
Back
Top Bottom