Ni kweli Anna Makinda ni 'Mbabe'?

Ni kweli Anna Makinda ni 'Mbabe'?

Huyu mama ameyataka matatizo mwenyewe, am sure kuna kipindi atakuwa anajilaumu kwa nini aliutaka u-speaker, any way tumwombee kwa muumba amuongezee busara na hekima.
 
Yale maswali ya Lisu yalikua mtego sana kwake ndo maana akavuta pumzi ili apate madesa ya kumsaidia. Wapiganaji wa CHADEMA wameonyesha wapo makini sana. Kama swali la mnyika hakulijibu inavyotakiwa alienda nje ya swali kwa sababu ya jazba aliyokua nayo. Zile karatasi zilikua na serial no sasa yule aliekua anagawa zile karatasi baadae anaweza kujua kua mnyika alimpigia kura nani kwa sababu aliiona serial no ya mnyika wakati anagawa zile karatasi. pia unaweza kua mchezo wameucheza kwa kugawa serial no kutokana na vyama na hapo ndo inaweza kuwarahisishia kuwagundua wana CCM ambao wamewasaliti. Yule mama amejibu bila kuangalia msingi wa swali ulikua vipi. Asidhani wananchi hatuoni hapo tume note tutaonana kwenye hukumu yao 2015
 
kwa kweli namtabilia kutoa machozi this time bungeni
 
Jordan emechemsha, hata kama chadema imefadhiliwa na huyo unayemuita jambazi, ukweli unabaki kwamba watanzania wengi walimchagua Dr Slaa, kwa hiyo ina maana wewe hutaki mabadiliko. unanikumbusha ule usemi uliosemwa na JK eti tunajenga nyumba moja tusigombee fito mbona yeye anaiba fito za wenzake, kwani CCM inatakiwa kutawala milele, basi hatuna sababu ya kuwa na opposition parties.
 
Ndg zangu, tangu mwanzo tu nimeweza kutambua kuwa wapiganaji wetu wapo makini sana. Ebu angalia tu suala la serial number kwenye karatasi za kupigia kura. Swali la Mnyika lilikuwa na mantiki kubwa sana na nadhani thithiem imefanya hivyo deliberately (kama kawaida yake) ili kupunguza 'uhuru' wa wabunge wake kumchagua mgombea kutoka chama kingine. Kwa jinsi thithiem inavyodhibiti wabunge wake, sitashangaa wabunge wake kuingiwa uoga wa kuja kujilikana hapo baadaye kama walimpigia nani.

Ninachomshukuru Mungu ni kuwa ubabaishaji wote huo sasa umepata dawa yake. Chini ya wapiganaji wa aina ya akina Tundu Lissu, Myika, Mbowe n.k. lazima utapungua sana kama siyo kuondolewa kabisa.
 
Wapiganaji wa CHADEMa nimewapenda sana Mwanzo mwisho hakuna kucheka wala kupiga makofi ya kinafiki. Endeleeni na msimamo huo huo hadi tutakapoikomboa nchi yetu kutoka kwa mafisadi. "Mwanajeshi hacheki vitani"
 
Ninachokiona ni kuzima hoja zote za akina Lissu.Napata wasiwasi kama kweli ipo hoja ambayo itapita ukizingatia idadi ya wabunge matumbo ndani ya bunge.Haki haiwezi kutendeka ndani ya bunge kwa hii bad start.Hoja hazijibiwi ikaridhisha bali kinachofanyika ni kuongea chochote waccm wapige makofi na vigelegele mambo yaendelee kawaida.Huyu bibi jamani hana uzuri hata kidogo!Ni pandikizi.Tunahitaji mjadala wa kitaifa kuhusu hili
 
Ndg zangu, tangu mwanzo tu nimeweza kutambua kuwa wapiganaji wetu wapo makini sana. Ebu angalia tu suala la serial number kwenye karatasi za kupigia kura. Swali la Mnyika lilikuwa na mantiki kubwa sana na nadhani thithiem imefanya hivyo deliberately (kama kawaida yake) ili kupunguza 'uhuru' wa wabunge wake kumchagua mgombea kutoka chama kingine. Kwa jinsi thithiem inavyodhibiti wabunge wake, sitashangaa wabunge wake kuingiwa uoga wa kuja kujilikana hapo baadaye kama walimpigia nani.

Ninachomshukuru Mungu ni kuwa ubabaishaji wote huo sasa umepata dawa yake. Chini ya wapiganaji wa aina ya akina Tundu Lissu, Myika, Mbowe n.k. lazima utapungua sana kama siyo kuondolewa kabisa.

Hapa kuna kitu kinaitwa ''psychology''. Huyu ameingia kwa msaada wa kamati kuu ambayo tunajua wazi inamilikiwa na kundi gani. Kuna pressure kutoka katika jamii inayoletwa na hasira za kumuondoa mzee Sitta. Kwahiyo mheshimiwa Mama ana kazi za njia panda. Mosi, kuwaridhisha mafisadi kuwa hoja za kuwaumbua zinaishia mikononi mwa mama, lakini pia anataka authibitishie umma kuwa yeye ni makini kuliko mtangulizi wake. Hili linampa taabu sana, hasira na jazba ni dalili za mkandamizo[pressure] unaotokana na mambo hayo mawili.
Hatari ya jambo hili ni kuwa ipo siku atasahau sheria akijua jazba zitamsaidia na hapo ndipo mama ataumbuka. Ninawahakikishia kuwa kutokana na pressure inayomkabili si zaidi ya vikao viiwili vijavyo mtaona ukweli huu. Na kwabati mbaya sana timu iliyopo mjengoni intisha ya wapiganaji ni makini na inatisha.
It is a matter of time, mtaona atakavyoumbuka.
 
Time will tell waungwana time will tell atakuja omba jiuzuru uko mbele ya safari cz this time is NO MERCY TIME nilikuwa namtegemea mh Sitta aendelee na wadhifa wake huo wa uspika cz kwa maoni yangu ndie ambae angeliweza hili bunge la sasa
 
DESPERATE, CONFUSED, SHORT TEMPERED, UNPRESENTABLE, RUDE.! Tutammiss baba 6 jamani. He waz charming, calm, understanding. Utani wake uliwafurahisha wabunge. Jamani hamjambo? Na wake zenu? Najua wengine wake zenu wako hapa.... Cool. LAKINI SIO HUYU HEADMISTRES ndugu zangu, Mbona shule tutaiona chungu!
 
Wakina mama wanaweza wajitokeze wagombee washindane na wanaume si kusubiri kupewa nafasi za upendeleo..
kusubiri nafasi za upendeleo kwa kigezo cha gender ni ishara tosha kuwa hawawezi. Kuwaondoa wanaume kwenye mchakato kabla ya kupigiwa
kura na kuwaacha wanawake pekee ni ishara tosha kuwa wanawake hawawezi ila wanapachikwa kwa masilahi binafisi
ya wachache.
Waliopewa nafasi za upendeleo huishia kuwatumikia mabwana zao waliowapa hizo nafasi badala ya kulitumikia taifa.
 
panic ni hulka yake, you can not teach an old dog new tricks!
 
Ana kazi moja tu ya kutuonyesha kwamba bunge linaendeshwa kwa kanuni. Akiendekeza jazba basi wapinzani wasimcheleweshe. Wapekue mahala kujua kanuni zinasemaje kuhusu spika anayeingiza masuala yake binafsi bungeni kama jazba wakati hakuna aliye juu ya kanuni hata kama jazba hizo zina washabiki wake hata humu JF.
Kazi aliyopewa na sisiem ni moja tu, kuhakikisha kuwa anausambaratisha upinzani bungeni. Na ole wenu wapinzani mkijitia kujua, mtajikuta kila bunge mnatolewa nje, ili "sheria na kanuni zenu" mkanukuu nje ya mjengo!!!kazi ipo mwaka huu. Lets wait n see
 
Mwanzo wake unaonyesha upungufu wa ukomavu wa mtu mzima, labda waliompendekeza walifanya hivyo ili watumie hiyo silika yake ya jazba, ukosefu wa staha, kutokubali sababu na kudandia hoja.
Ana kitu kimoja tu anakitegemea, kishindo chorus ya thithiem. Aloweke miguu majini ili asilale kuhusiana na kanuni za Bunge.
 
Mheshimiwa Anna Makinda au hafahamu sheria au anatumia vibaya kiti cha Uspika. Kusema kwamba Tanzania Bara hakuna serikari ni uongo kwani katiba iko wazi, mawaziri wanaendelea na kazi zao mpaka mawaziri wapya watakapo apishwa, na ni wao watakao kabidhi kwa hao wapya! Hata walioanguka kama Mh. Masha na Mh. Mama Mwangunga bado wanapeta kwenye maofisi yao. Kuhusu CHADEMA kutotambua ushindi wa Mh Kikwete, lazima tukumbuke kwamba kuna uraisi kama taasisi, na Kikwete kama mtu. Naamini kwamba taasisi ya uraisi haina utata kwa mtu yeyote. Mheshimiwa Makinda ukumbushwe kwamba mihimili ya nchi ni mitatu, yaani, the Executive, the Legislature na Judiciary. Hii mihimili inatakiwa isiwe tegemezi; the executive inatekeleza kwa kufuata sheria, legislature inatunga sheria, judiciary inatoa tafsiri za sheria kuona kwamba haki inatendeka. Tukumbuke kwamba CUF hawakuzitambua shindi za viongozi wawili waliopita mpaka majuzi tu, lakini waliendelea kuingia bungeni na kushiriki kikamilifu, na aidha kutumia mahakama palipobidi.
 
madaktari (Gynaceologists/Obstreticians) nisaidieni jambo hili, je menopause haiwezi kuwa reversed? Yaani menopaused women kupata hedhi? Kama inawezekana, namtabiria huyu mama kuna siku atachafua kiti cha spika!!!
 
Back
Top Bottom