Ni kwanini ni vigumu kumngoja BWANA?

Ni kwanini ni vigumu kumngoja BWANA?

Mimi sio mtumishi na sitakuja kuwa. Am a business man. Ila najua kinachosumbua watu wengi ni kushindwa kutafsiri kile kitabu walicholetewa na wazungu, wakabiwa wakikifuata wataenda mbinguni😂 Bila kujua ile blue print ya kufanikiwa kwenye kila jambo ulitakalo chini ya jua, shida hawana uwezo wa kutafsiri kilicho andikwa. Sasa wanatafsiriwa na watu wanaotaka kuwaburuza
Uko sahihi watu wengi hawawezi kutafsiri na kuelewa mantiki ya neno la kwenye biblia wao huishia kusoma kilichoandikwa na kuishia hapo bila kujua inahitajika kuchimba neno lile na kulielewa katika muktadha wa kiroho zaidi na si kimwili
 
Uko sahihi watu wengi hawawezi kutafsiri na kuelewa mantiki ya neno la kwenye biblia wao huishia kusoma kilichoandikwa na kuishia hapo bila kujua inahitajika kuchimba neno lile na kulielewa katika muktadha wa kiroho zaidi na si kimwili
🤝
 
  • Wanataka majibu ya haraka.
    Binadamu kwa asili hupenda kuona matokeo ya haraka. Kusubiri huwa kugumu, hasa wakati wa matatizo ya kifedha, magonjwa, changamoto za kifamilia au mahusiano. Mara nyingi watu huona ni afadhali kuchukua hatua mara moja kuliko kusubiri.
  • Hofu ya kupoteza fursa.
    Watu huogopa kwamba wasipochukua hatua sasa watapoteza kazi, biashara, ndoa au nafasi nyingine muhimu. Hofu hii huwafanya wategemee muda wao wenyewe badala ya muda wa Mungu.
  • Ni vigumu kumwamini Mungu bila kuona matokeo mara moja.
    Kumngoja Mungu kunahitaji imani. Kwa kuwa mipango ya Mungu haionekani mara moja, watu huanza kujiuliza:
    • Je, Mungu ananisikia?
    • Je, hali yangu itabadilika kweli?
    • Je, nasubiri bure?
  • Shinikizo la dunia ya leo.
    Dunia ya sasa inathamini mambo ya haraka:
    • Mawasiliano ya papo kwa papo.
    • Huduma za haraka.
    • Mafanikio ya haraka.
    • Kutimiza mahitaji mara moja.
    • Mtazamo huu huwafanya watu waone uvumilivu wa kiroho kuwa jambo lisilo na maana.
  • Maumivu ya kukatishwa tamaa zamani.
    Wengine wameomba kwa muda mrefu bila kuona majibu waliyotarajia. Kukatishwa tamaa mara kwa mara kunaweza kuwafanya waache kumngoja Mungu na kuamua kufanya mambo kwa njia zao wenyewe.
  • Tamaa ya kutaka kudhibiti kila kitu.
    Kumngoja Mungu kunahitaji kujisalimisha kwa mapenzi yake. Watu wengi hupenda kuwa na udhibiti wa maisha yao, hivyo huona ni rahisi kufanya maamuzi yao wenyewe kuliko kusubiri mwongozo wa Mungu.
  • Kutokuelewa maana halisi ya kumngoja Mungu.
    Kumngoja Mungu hakumaanishi kukaa bila kufanya chochote. Badala yake, kunamaanisha kuendelea kuomba, kufanya yaliyo sahihi, kutenda kwa hekima, na kubaki waaminifu huku ukimwamini Mungu kuhusu matokeo. Watu wengine hudhani kusubiri ni uvivu, hivyo hukata tamaa.
 
Unaweza kusubiri miaka 40 in really?

Mda mwingne nahish kama kila kitu ni planned toka kuumbwa.
Mkuu kila kitu kiko planned, yes! lakini chaguzi zetu zinamatokeo pia, ukichagua njia ya mkato leo unakuwa unajichelewesha mwenyewe au unaharibu ramani, ile miaka 40 ya Waisraeli jangwani haikuwa plan ya Mungu, safari ilikuwa ya siku 11 tu, lakini kiburi na malalamiko yao ndio vilitengeneza hiyo miaka 40.
 
Inawezekana kuna kitu unakijua au upo kwenye process za kujua. “Ongeza kuutafuta ufalme wa Mungu” soon utafunguka na kuongezewa kila kitu
Hiyo Mathayo ni ngumu Mkuu. Mbona hata Biblia yenyewe inasema kwenye Mithali mkono mlegevu huleta umaskini?

Wakati mwingine tunasingizia tu mchakato wa Mungu kuficha ukweli kwamba mifumo ya kiuchumi ya nchi au uzembe wetu ndio unatufanya tusubiri sana, sio ufalme wa Mungu.
 
Hiyo Mathayo ni ngumu Mkuu. Mbona hata Biblia yenyewe inasema kwenye Mithali mkono mlegevu huleta umaskini?

Wakati mwingine tunasingizia tu mchakato wa Mungu kuficha ukweli kwamba mifumo ya kiuchumi ya nchi au uzembe wetu ndio unatufanya tusubiri sana, sio ufalme wa Mungu.
😂😂😂 bado hujasoma na kuelewa mkuu. Mkuu kwani inadhani kuna mwanaume mlegevu? Hafanyi kazi? Hatafuti maisha? Hapana mkuu, wanaume wote tunatafuta, ila tunapungukiwa ndani yetu.

“Wabie wautafute kwanza ufalme wa Mungu na hayo yote mtazidishiwa”
 
"""Bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya;,,,, watapanda juu kwa mbawa kama tai;,,, watapipiga mbio wala hawatachoka;,,,, watakwenda kwa miguu,,, wala hawatazimia"""
Zaburi 40:31......

"""Umngoje BWANA uwe HODARI,,,, Upige moyo konde,,,,,, naam umngoje BWANA.....
Zaburi 27:14......

Kwanini leo ni vigumu, kumngoja BWANA???

Cc: Samson Ernest, Baba mtakatifu91, Dogoli kinyamkela, Matunzo 02, Mopak, Seran
Bwana Gani tenah 🤣🤣 unae mzungumiza ww mkuu ambae unamngoja
 
Enzi hizo ukitaka kusafiri ilikuwa ni lazima utembee kwa miguu au utumie mnyama, ukitaka habari utaipata kwa njia ya barua , maisha yenyewe yalikuwa yanawalazimisha kuwa na patience, tofauti na sasa hivi ambapo kila kitu unakipata ndani ya muda mfupi sana.

Kumbuka Ibrahimu alisubiri mtoto miaka 25, na Musa alisubiri miaka 40 jangwani, shida ni kwamba historia inasomeka kwa dakika 5 kwenye Biblia, lakini kiuhalisia hao watu walisota sana kuliko sisi.
Ila ni kweli, hata ukitafuta kitu for a long time ukikipata lazima ukiheshimu....
 
Kumgonja Bwana ni changamoto hata akija leo waliomugoja ni wachache sabab huwezi kumgoja mtu ambaye humkumbuki wala kumfikilia mtu akipata nafasi kidog anaigia kwenye mitandao ya jamii kwa hali hiyo unadhan mtu atamgojaje bwana?
Mpango wa shetani ni kuhakikisha tunakuwa na mambo mengi... ili tusiwe na mda na MUNGU yani mtu kusikia hadi ibadani baada ya hapo mpaka next week¡
 
😂😂😂 bado hujasoma na kuelewa mkuu. Mkuu kwani inadhani kuna mwanaume mlegevu? Hafanyi kazi? Hatafuti maisha? Hapana mkuu, wanaume wote tunatafuta, ila tunapungukiwa ndani yetu.

“Wabie wautafute kwanza ufalme wa Mungu na hayo yote mtazidishiwa”
Huo mstari wa mithali ni ushahidi tosha kuwa wapo wanaume wavivu pia, siyo wote wanapambana, hili wala halihitaji mjadala Mkuu.

Hiyo ahadi ya kuzidishiwa inafanya kazi pale tu ambapo tayari kuna kitu kinafanyika mtaani. Mungu hazidishi uvivu , huwa anazidisha juhudi zako, akili yako, na nidhamu yako ya kazi. Ufalme wa Mungu unakupa ile hekima, nidhamu na kibali cha kukusaidia kuendesha biashara yako au kazi yako ili isife.

Inatakiwa watu walitambue sana hili.
 
Back
Top Bottom