Psalm 103
JF-Expert Member
- Jul 5, 2026
- 1,657
- 2,704
- Thread starter
- #161
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi mzuri.....Ni kweli kumngoja Bwana imekuwa changamoto kwa wengi wetu, kama walivyotangulia kusema baadhi ya wajumbe, nami niongeze kidogo;
Wengi hatuna msingi wa neno la Mungu, tunataka Mungu afanye tunavyotaka kisha tuendelee na mambo yetu yanayomchukiza Mungu.
Vingine tunavitaka kwa tamaa zetu, Mungu akiangalia nia ya vile tunavitaka hivyo vitu anakaa kimya.
Na wale ambao tupo vizuri na Mungu, dunia inatuvuta kwa mengi mazuri, tunaona kama tunachelewa, na hatuishi katika viwango vinavyotakiwa.
Lakini ukiwa na subira/uvumilivu lazima uvune matunda mema, Mungu hutuandaa hatua kwa hatua kupokea yale tunayataka.
Ndio maana mtu anayemwamini Mungu akipata mafanikio, anaweza kudumu nayo muda mrefu kama ataendelea kuwa na uhusiano naye mzuri.
Muhimu ni kuamini Mungu wetu anatupa yale tunayoyahitaji kwake sawasawa na mapenzi yake na kwa wakati wake.
Mungu akubariki sana