Mwanamke kumtongoza mwanaume siyo jambo la kawaida kabisa kwenye jamii yetu ya Tanzania ndiyo maana inapotokea inabidi kutafuta ushauri. Kuna dada amekuwa akinipigia simu za kunitaka niwe naye kimapenzi toka januari mwaka huu lakini nimeshindwa kukutana naye kutokana na mimi kubanwa na shughuli nyingi. Huyu ni mwanafunzi wangu kwenye chuo kimoja nilichokuwa nikifundisha mwaka jana kwa sasa ameshamaliza na anafanya kazi. Binafsi siikumbuki sura yake lakini jina nalikumbuka, mwanzoni alianza kwa kuniomba nimtafutie kazi kwa madai kuwa haridhiki na mshahara anaopata kwenye kazi yake ya sasa.Nilimuahidi kumpa taarifa za uwepo wa kazi ili afanye aplication endapo ningepata taarifa hizo.Hilo likampa fursa ya kunipigia simu mara kwa mara kuulizia kama kuna updates za kazi. Baadaye uvumilivu ulimshinda na akaamua kuweka nia yake bayana kwamba ananipenda na anataka niwe kifuani kwake hata siku hiyo kama ningeamua kumfuata, binafsi nilistaajabu sana na kumshauri atulie nikipata muda ntamtafuta tufahamiane zaidi jambo ambalo halijatokea mpaka sasa. Sasa leo kaniomba nimtumie nauli aje kwangu kwan ana likizo kazini kwake, hilo pia limenitatiza kwani simfahamu undani wake hivyo nimemjibu kama kweli ana nia ya kuja kwangu ajigharamie kwani mipango yangu ya pesa iko tight sana kwa sasa. Ushauri wenu, je, kama akija nimpokee na nianzishe naye mahusiano kwani sina demu? AU nimpotezee kwani anaweza kuwa malaya?