Lidafo
JF-Expert Member
- Sep 26, 2019
- 551
- 747
Wasalamu ndugu wana JF wote.
Historia ni somo muhimu na lenye tija sana kwa kuzingatia ukweli kwamba historia inatunza kumbukumbu muhimu kwa taifa, Kuanzia ngazi ya shule za msingi mpaka vyuo vikuu somo hili limekuwa linawajengea wanafunzi , walimu na wanahistoria kwa ujumla uwezo wa kutoa hoja na kuzitetea na historia inatumiwa na wanahistoria kama dira katika kuishauri jamii na serikali juu ya mambo ya mbeleni kwa kuzingatia athari na tabia za mambo ya nyuma.
Historia ni pana sana kuanzia historia ya dunia ambapo hapa sio wana historia tu bali hata wanasayansi wanaingia, Historia za mabara, Nchi mpaka vijiji juu ya maendeleo ya Kiuchumi, Mabadiliko ya tabia ya nchi, Maswala ya kisiasa kama ukoloni na harakati za uhuru, Historia za watu mashuhuri n.k
Sasa turudi upande wa pili, Mambo yote haya yanayohusu historia pamoja na tija zake bado kunabakia swali moja la msingi ambalo ni ..NI KWA KIASI GANI TUNAWEZA KUPIMA UKWELI WA HISTORIA TUNAYOFUNDISHWA?
Mfano katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika wapo watu wengi wanadai kuwa historia imepindishwa kidogo na inampendelea zaidi mwalimu Nyerere na kuwaacha baadhi ya watu ambao ndio walikuwa chachu ya uhuru wenyewe hasa kwa Tanganyika, Hili linatoa shaka juu ya ukweli wa historia zinazotolewa.
Mifano ni Mingi ambayo historia Imekuwa na utata katika kuelezea uhalisia wa jambo lililopita kwa uchache ni taje baadhi ya mambo kama Utata juu ya Maiti ya Farao wa Kipindi cha Musa, Ukweli kuhusu mapinduzi ya Zanzibar, Historia ya Mwenge wa uhuru n.k
Sasa kama mwanahistoria au mtu unayependa kujifunza mambo ya mada mtambukaa unafikiri ni kwa jinsi gani Tunaweza kupima ukweli wa historia?