Ni kitu gani wanaume hufuata kwa wanawake?

Ni kitu gani wanaume hufuata kwa wanawake?

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,988
Wanaume huwafuata Wanawake kwa mambo mawili, ambayo ni MAPENZI na SEX. Lakini inapofika hatua ya Kuoa, Wanaume hawaoi kwa sababu ya SEX au MAPENZI, wanaoa kwa sababu ya kutafuta AMANI NA UTULIVU WA NAFSI (STABILITY).

Mwanaume anaweza kukupenda na asikuoe. Mwanaume anaweza kuwa anafanya mapenzi na wewe tena mkadumu kwa muda mrefu lakini asikuoe. Lakini akampata mtu mwingine akamuoa hata kama mahusiano yake na mtu huyo yalikuwa ya miezi miwili.

Wanaume wengi hutizama mbali zaidi pale wanapotaka KUOA. Huwa hawafikirii habari za suti kali za harusi na sherehe ya gharama, vitu ambavyo hufikiriwa zaidi na wanawake kila wanapoiwaza ndoa.

Wanaume huwaza, iwapo mwanamke huyu anaweza kuijenga familia bora, anaweza kuwahudumia watoto? Hatanipa stress huko mbeleni, hatanisumbua katika masuala ya tendo la ndoa?

Wanaume wanaotaka kuoa huwa hawapendi wanawake wanaowapa mawazo, ndio maana wengine hukaa muda mrefu kwenye mahusiano lakini unajifikiria bila sababu ya msingi anakuja kuoa mtu amekaa nae kwa miezi miwili.

Ni ile utafutaji wa AMANI YA NAFSI.

Sex is a pleasure, love is an affection, RESPECT is Stability.

1625563558018.png

​
 
Nilijua umeuliza swali unataka ujibiwe... kutokana na kichwa cha uzi.

Hata hivyo jibu nililoliandaa kichwani kabla ya kufungua uzi ni

Wanaume wanafata manyonyo kwa wanawake.

MK hata shoga anao.
 
We Noelia sex bila chura ni sawa na kubeba wallet bila pesa
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hapo kwenye amani na utulivu wa nafsi mkuu kuna watu wameoa jehanam ndogo kila siku tunashinda nao bar wanakunywa wanaogopa kurudi nyumbani kwao mapema wakiwa na akili timamu maana nyumba kama afganistan au izrael na palestina
 
Ndio maana hata bibilia ilisema enyi wanaume mkae na wake zenu kwa akili maana inawajua jinsi mlivyokuwa vichaaa
Sio kwamba iliona kuna kauzezeta ndani yenu? Huwezi kutumia akili kwa kitu kijinga obviously mtu yeyote akikwambia kufanikisha jambo fulani tumia akili means kakuona mjinga usietumia akili
 
Sio kwamba iliona kuna kauzezeta ndani yenu? Huwezi kutumia akili kwa kitu kijinga obviously mtu yeyote akikwambia kufanikisha jambo fulani tumia akili means kakuona mjinga usietumia akili
Hapana bhana nyinyi vichwa vibovu
 
Hapana bhana nyinyi vichwa vibovu
Ukiona mtu anahangaika kuonyesha udhaifu wa mwenzie baso ujue yeye ndie mwenye udhaifu husika, mbovu Ni wewe na unaofanana nao
 
Ukiona mtu anahangaika kuonyesha udhaifu wa mwenzie baso ujue yeye ndie mwenye udhaifu husika, mbovu Ni wewe na unaofanana nao
Ni nyinyi wanawake vichwa vinaenda mbio kuliko gari ya mbeya Sauli
 
Wanaume wapo matabaka Mengi.

1.Serious Men hawa wanataka future nawewe wanaangalia mambo ya msingi wewe unaweza kumfaa kama mke. Sasa huangalia lifestyle lako unahandlelije. Halafu pia unavyowachukulia watu wakuzungukao. Na ulivyo kwa watu hivyo vitu ndio anavutiwa.

Tabia yako inangaliwa pia kwasababu ukiwa na madharau ,matusi,nakejeli kwa watu je kwake nafamilia yake. Unafiki hapendi watu wanafiki ,upendokana unao kwa wazungukao na pia kujali kama unacare wakuzungukao. Mwanamke real na sio pretenders haya ndio mwanaume huangalia kwa mwanamke.

Bila kusahau appearance sio uzuri unavyopangilia nguo zako unavyotembea kujichukua na pia kujipenda. Unavyoongea nawatu huwavutia wanaume serious maana humfanya avutiwe.

Mwisho uzuri mtu serious hupenda mwanamke wa kati mzuri wa wastani. Uvaaji wa wastani not too much. Admires/Waliotamani
Hawa wanaangalia mvuto wako jinsi ulivyovaa na jinsi ulivyovutia kwa mapamboo sio asilia mtu wa muda hawezi kukuangalia kama hujapaka make up nakuvaa vizuri sana hajali hata kama unajiaibisha kusudio lake nikujiridhisha yeye.

Anangalia umboo lako pia je unatako? Vivutio vyote anaangalia. Hawa ukiumwa anakimbia,ukipata shida yeyote umekwisha anakimbia.
Kutafuta ambaye yupo perfect.

Mume za watu. Hawa huwa wanaangalia je wewe utaweza mamboo? Anakufaaa je huyu yupo kwenye vile nataka ni vyombo vyangu anapiga mchezo kwisha.hadi atake tena. Ndio unamwona.

Mamas boys na marioos. Hawa wanaangalia hela zako tu naunavyowatunza ila hakuna kingine. Kwao ilimradi uwape watakacho nakupiga tungi, starehe kwa sana na story ambazo haziishi,kwenda shopping,malls kupiga picha,nawaterfalls kuogelea basi. Kuangalia mpira na kwenda high classes places na simu za gharama.

Basiiii.
 
Wanaume wanaotaka kuoa huwa hawapendi wanawake wanaowapa mawazo, ndio maana wengine hukaa muda mrefu kwenye mahusiano lakini unajifikiria bila sababu ya msingi anakuja kuoa mtu amekaa nae kwa miezi miwili.
 
Back
Top Bottom