Fohadi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2020
- 770
- 2,408
- Thread starter
- #41
umemaliza kila kitu mkuu.PB imejipambanua vizuri kabisa, kila mmoja ana role yake na anaimudu vizuri. Barbara ni Host mzuri kabisa, KP & Cza ni wachambuzi wanaochambua mambo kwa kina.
Sam anamudu vizuri usomaji wa magazeti kwa mtindo wa kipekee unaovutia masikio ya msikilizaji.
Bonge naye nafasi yake anaimudu vizuri jambo ambalo wanajikuta wanatengeneza timu moja hatari sana yaani akikosekana mmoja unaona kabisa kuna pengo.
Napenda sana pia segments zao zimepangiliwa vizuri sana ingawa huwa navutiwa zaidi na magazeti kutokana na namna Sam, KP na Cza wanavyoungana kuchambua mambo.
Huwa sifurahii kipindi Fredwaa akiwepo, sielewagi position yake pale CMG. Ila kwangu PB ya Clouds FM ipo juu sana na haina mpinzani kwenye shows za asubuhi kwenye redio za Tanzania.