Radio One na Kipindi chenu cha Mazungumzo ya Familia huyu Mgeni wenu Maajabu 18 atawashushieni Thamani

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,646
109,034
Zifuatazo ni Kauli zake za Kipuuzi ambazo hazivumiliki tena na zinakera amezisema Leo Jumapili tarehe 7 May, 2023 katika Kipindi cha Mazungumzo ya Familia cha Radio One.....

1. Mwanaume yoyote anayecheza VICOBA au yuko katika Vikundi vya Mikipo vya Mtaani ni Dhaifu na Hajitambui

2. Mwanaume yoyote wa Kiislamu anayeishi na Mke Mmoja ana matatizo ya Urijali ila Mtume ametuambia Mwanaume wa Kweli wa Kiislamu lazima awe na Wanawake kuanzia Wawili

3. Mwanaume yoyote aliyeoa / anayeishi na Mwanamke akiona Siku zote hagombezwi au hasemwi na Mkewe huyo siyo Mwanaume na hafai. Kugombezwa au Kugombana kila Siku na Mkeo au Mpenzi ni Jambo jema na Afya katika Mahusiano yenu

Radio One kupitia Boss Wenu na Mtani wangu wa Kihaya Deogratius Rweyiyunga ( Boss Rweyu ) nimeshawahi kuandika Uzi hapa hapa JamiiForums nikiwatahadharisha kuhusu huyu Mgeni wenu Maajabu 18 kuwa anaharibu ila cha Kushangaza bado mnamkaribisha tu hapo.

Mambo yake yanayonikwaza kila Akialikwa nanyi hapo Radio One katika Kipindi chenu cha Mazungumzo ya Familia ni kama yafuatayo......

1. Mdini sana na sijui ni kwanini huwa anapenda Kuzungumza Mambo ya Dini yake Redioni akijua kuwa hiyo Redio ( Radio One ) haisikilizwi na Waislamu Wenzake.

2. Ana maneno ya Kejeli kwa Wakristo na pia ana Chuki zisizojificha kwa Sisi Wakristo na ukiwa makini Kumsikiliza utaligundua hilo.

3. Apunguze Ushamba na Sifa za Kijinga kwani kila mara anapenda kutuonyesha kuwa hana Tatizo na Mkewe ( Ndoa ) yake huku akijisifia kuwa akiona Mkewe Kakasirika basi haraka anamrushia Pesa au anamnunulia Gari.

4. Aache Kujipendekeza Kunakoboa kwa Mtangazaji wa Kike Farhia Middley kwa Kukubaliana nae kwa kila akisemacho ( Farhia ) hata kama ni Pumba ( cha Kipuuzi ) huku akimkandamiza Mtangazaji wa Kiume Haji Kibwana.

5. Akialikwa hapo Studioni Kwenu Radio One awe Mgeni na kamwe asitake nae Kujionyesha ni sehemu ya Watangazaji na Wafanyakazi wa IPP Media ( Radio One ) ikiwemo.

6. Aache kujifanya ni Mtabiri na Kuwatabiria Watu kwa Majina yao. Kwa mfano kuna Msikilizaji alituma Meseji iliyosomwa na Mtangazaji Farhia Middley akiuliza je, James na Joyce Kinyota wanaweza Kudumu cha Kushangaza huyu Mgeni wenu wa hovyo hovyo Maajabu 18 kabla ya hata Kusubri Meseji imalizwe Kusomwa Yeye upesi sana akadakia na kujibu / kusema kuwa Watu wenye Majina ya James na Joyce hawaendani Kimahusiano na Kimaisha pia.

7. Aache Dharau, Kujisikia na Kuropoka Siri za Ndani za Wateja wake ( Anaowatibia na Mauchawi na Dawa zake za Uwongo na Kweli ) akiamini kuwa labda akizisema Hewani basi atapendwa na Kuaminika.

Wageni pekee wa Kuwaalika na Wanaojitambua katika hicho Kipindi chenu cha Mazungumzo ya Familia ya kila Jumapili ( ambacho GENTAMYCINE ni Balozi wenu Tukuka wa Kujiteua Mwenyewe Kilazima ) ni Yule Dada Muandishi wa Vitabu aitwae Anaclea na Yule Mwanasaikolojia Dk. Xavery kwani hawa hata Ukiwasikiliza tu utajua Akili Kubwa inaongea ila huyo Mswahili wenu sijui Maajabu 18 na Dawa yake ya Kiuganga anayeipigia Promo mara kwa mara.

Mwisho mwambieni huyo / huyu Mgeni wenu Maajabu 18 kuwa ule Wosia wake aliotuambia Wanaume kuwa endapo Wake zetu au Wapenzi wetu Wakitukosea tu tusiwapige bali tuwasamehe na tuwasindikize na Zawadi au Pesa Shilingi Elfu Hamsini ( Tsh 50,000/= ) Mimi GENTAMYCINE ( Rais wa Wanaume wasiopenda Upuuzi JamiiForums na Mtaani ) nimeukataa na mtindo Wetu utakuwa ni ule ule Wake zetu au Wapenzi wetu Wakizingua / Wakitukosea kitakachofuata Kwao ni Kipigo tu cha Kishalubela ( cha Kikatili ) ili Wanyooke na Washike Adabu zao.

Yaani kabisa eti GENTAMYCINE nimkute Demu wangu au Mke wangu Anabanduliwa Mubashara Ghetoni Kwangu au Guest House au Lodge na Mjuba Mkomavu nimsamehe kisha Mimi niliyekosewa nimnunulie Zawadi au nimpe Pesa. Wewe Jamaa ni Bwege hadi natamani ningekuja hapo Studio Radio One ili Nikuwambe / Nikuzabe Vibao ili Akili zako zikurudie.

Umenikera kweli kweli.
 
Kaharibu sana hicho kipindi, bora umegundua na unatusaidia kupaza sauti atolewe kwenye hicho kipindi pendwa ambacho hata LOTH HEMA huwa nakifuatilia kipindi hicho kila jumapili na marudio yake usiku
 
Back
Top Bottom