Jimmy De Lite
JF-Expert Member
- Jun 10, 2019
- 635
- 2,341
Kila mtu Anaweza kuchora kitu chochote na kuwauliza watu alimaanisha nini,so huwa me sipotezi muda na katuni.
umekariri ee?hii katuni ukiangalia kwa maoni yangu naweza kusema hivi
Nyoka huyo mkubwa ni jpm na huyo mdogo ni makonda😎😎😎.
Naijua hii katuni inavyosema, lakini sijui inamsema nani.
Bwana yule kaingia MZIGONI kwa KUPANDISHWA, kapiga mzigo mwaka wa kwanza, kapiga wa pili na watatu. Tunavyoongea, anapiga wa nne. Kwa mujibu wa sheria za kazi, kila baada ya miaka mitano, MWAJIRIWA wa ajira hii hulazimika kufanyiwa upya USAILI ambapo mchujo hufanywa ndani ya AGENCY iliyokudhamini kwa ajira hiyo ambayo kwa hapa ni JOKA KIJANI na ukifanikiwa kuvuka mchujo bado kuna upinzani mwingine wa AGENCY NYINGINE ambayo nayo ina candidate wake inataka aajiriwe yeye.
Kwa kutambua UPINZANI utakaokuwepo kutoka ndani ya AGENCY YAKE (Joka Kijani) na AGENCY PINZANI (Joka Kijivu) Bwana yule kaamua kuweka mazingira sawa kabla ya USAILI. Ndani ya mwaka wa nne kaamua kubutua kombolela kwa ....aaah, nimechoka bwana.
Ngoja nikaombe kazi ya kuchimba mitaro Naniliu Mashariki, nasikia kuna bilioni kadhaa zimetengwa huko ndani ya huu mwaka wa 4 zikomeshe tatizo la maji.
Shikamoo Masoud Kipanya, utatupasua vichwa...hebu toa majibu ya mtihani.
Hata wao wanajiuliza....Hilo joka ni lipi na limetokea wapi ndani ya chama?
Siasa siipendi ila ngoja nijaribu. Mwaka wa kwanza ile ngazi ni upinzani uligalagazwa kwenye uchaguzi chama cha kijani kikashinda. Kwenye mwaka watatu na wanne kuna kibox kina matundu kumi na moja hapo kamanisha Tundu lissu alipigwa Risasi zaidi ya kumi ili kupunguza upinzani kwa kwenye mwaka watatu wa utawala wa chama cha kijani, lakini ghafla bila kutengemea kwenye mwaka wa nne wa utawala wa chama cha kijani ngazi ya upinzani inaonekana kunyanyuka tena means Tundu lissu amepona anataka kuludi kumzuia nyoka wakijani asiingie kwenye utawala wa mwaka wa sita ndo maana Unamuona nyoka wakijivu anataka kumvuta nyoka wa kijani ambaye anataka kuingia mwaka wa sita.
Hii katuni inahitaji kuwa na PhD ya roketi sayansi ili uweze kuilewa, mimi nina satifiketi ya mortuary, ngoja nisubiri mjadala labda nitaelewa