Ni Kipanya tena, kwa wenye akili pekee

Ni Kipanya tena, kwa wenye akili pekee

Hilo ni game la nyoka, ukicheza kete zako vizuri, unaenda kwenye chumba chenye ngazi unapanda, ukicheza kete zako vibaya unaangukia kwenye chumba chenye joka unaliwa unarudishwa kuanza tena moja. Na ndio system inavyofanya kazi wakati wa sasa. Wengi wamecheza kete zao vizuri wamepanda, wengine wamecheza kete zao vibaya wameliwa na nyoka wamerudi kuanza tena upya.
Umenena vyema ukiujua mchezo Unaitwa snake and ladder ni rahisi kutafsiri
 
Unamvunjia heshima sasa
Siyo kumvunjia heshima mkuu,

Maisha yalivyokaba hivi halafu kipanya na yeye tena hataki kutulegezea hata kidogo sasa tufanyeje...

Mimi huwa nazipenda sana katuni zake, lakini kuna zingine huwa analeta utafikiri anatupa adhabu mkuu.
 
Nimekupata mkuu pamoja sana
Siyo kumvunjia heshima mkuu,

Maisha yalivyokaba hivi halafu kipanya na yeye tena hataki kutulegezea hata kidogo sasa tufanyeje...

Mimi huwa nazipenda sana katuni zake, lakini kuna zingine huwa analeta utafikiri anatupa adhabu mkuu.
 
Joka kubwa limekatapika kanyoka kadogo, kanyoka kadogo kanaisoma namba
 
Hizo namba nyekundu ni awamu za serikali, ya kwanza hadi ya tano.

Lakini huyo joka la kijani ni ccm limenasa katika utawala.

Hilo joka la hudhurungi ni cdm linataka kumuondoa kwa kummeza ccm mwishoni mwa awamu yake, lakini halimfikii.

Limebakia tu kuachama kwa tamaa ya shibe ya kulimeza joka la kijani bila mafanikio.

Lakini joka la kijani liccm limeng'ang'ania kama ruba, limekazia kinyama, halitoki.
 
Hii katuni inahitaji kuwa na PhD ya roketi sayansi ili uweze kuilewa, mimi nina satifiketi ya mortuary, ngoja nisubiri mjadala labda nitaelewa
Ukiingalia kwa jicho la kisiasa na kinachotarajia kujiri mbele yetu, ni simple kutafakari.

Hayo majoka ni rangi za vyama hasimu hapa nchini. Mengineyo ungaunga utapata jibu.
 
kwa uelewa wangu mdogo (yawezekana nisiwe sahihi)

Hizo namba zina maanisha ni AWAMU za utawala wa hii nchi yetu

Awamu ya 1,2,3,4

Hapo kwenye awamu ya 4 kuna ngazi akimaanisha Watanzania walipaswa kupanda ngazi baada ya awamu ya 4 kuisha ili waondoke kwenye barabara ambayo nyoka yupo mbele.

Ila bahati mbaya ngazi tukaiacha na kuendelea na awamu ya 5 ambayo kwa sasa tunaiona kama CHUNGU

ILA tusichofahmu namba 6 pale ndio penye utamu zaidi maana ndio penye mdomo wenyewe

Huyo nyoka wa kijani ni utawala wa CCM uliopo madarakani unatusubiri kwa hamu tusogeee ili ututie Jino

so kwa utabiri wa kipanya nikwamba awamu ya 6 itakua shubiri zaidi ya hii ya sasa

Na hamna namna ni lazima tuinywe dawa maana ngazi tuliiacha tangu awamu ya 4.


Kuna hicho kikete cheupe chenye vidoti doti

Maana yake hii ni siasa,nilichokisema hapo juu mimi kinaweza kuwa kweli au si kweli naweza patia au kosea kwasababu hatujui kete itadondokea wapi.

Kuna huyo nyoka mwingine nyuma ya huyo wa kijani

Huo ni utawala mwingine ambao wananchi wanaupigia kelele wanatamani waupate

Lakini wasichojua ni wanatamani Joka kubwa kuliko joka la sasa.

#controla
 
Najiuliza ile alama ya 'kamari' inaashiria nini?
 
maana ukiangalia hizo namba zinasimamia muda wake wa uongozi aliokaa madarakani na hizo ngazi mbili ya kwanza n aloshukia na kuanza uongozi na ngazi ya pili ipo kwenye mwaka wake wa 4 ambao ndo atapandia kuachia uongozi japo yeye anataka kulazimisha afikishe mpaka mwaka wa 5 ila jpm kangaka anataka kummeza kwasababu anajifanya kama hajaona ngazi ilipowekwa hvo anataka kupitiliza[emoji41][emoji41][emoji41].
Heshima yako
 
Kidogo tunaendana kimawazo ila mimi nimeelewa uongozi ni miaka mitano tu...huyo nyoka mdogo ni wananchi wakali/wanaharakati na wenye msimamo kuhusu kikomo hicho...joka mkubwa alivyoona kikwazo ni icho ameona bora abahatishe kama kamari kummeza hicho kikwazo (joka mdogo/wanaharakati) ili kusiwepo wakishatoka itakuwa rahisi kuendelea
Muhula wa mwaka wa Sita baada ya miaka mitano kuisha joka lililotesa watu miaka mitano linajaribu kubahatisha kukamata muhula mwingine kwa mbinu zilezile maana kwa Sasa halibebeki ngazi za kupandia zimeharibika linatumia kamali kuona uwezekano
 
Muhula wa mwaka wa Sita baada ya miaka mitano kuisha joka lililotesa watu miaka mitano linajaribu kubahatisha kukamata muhula mwingine kwa mbinu zilezile maana kwa Sasa halibebeki ngazi za kupandia zimeharibika linatumia kamali kuona uwezekano
Kwamba jamaa anatamni muhula wa sita anatumia kinyoka kinchotoka mdomoni mwake yaani watu wanampigia debe aongeze muhula lakini hawana uhakika ni kama kucheza kamari hivi kuwa watafanikiwa au watafail.

Jamaa nimekusoma vema.
 
Back
Top Bottom