Ni Kipanya tena, kwa wenye akili pekee

Ni Kipanya tena, kwa wenye akili pekee

Hongera sana mkuu kwa kuwa na hiyo satifiketi ya mochware
Hii katuni inahitaji kuwa na PhD ya roketi sayansi ili uweze kuilewa, mimi nina satifiketi ya mortuary, ngoja nisubiri mjadala labda nitaelewa
 
Nabahatisha tu, kuna watu wachache ndani ya ccm wamejitoa muhanga kuhakikisha jamaa haongezewi miaka mingine ya kuongoza hiyo 5 inamtosha
 
Hii kila mtu anaweza kuipa tafsiri yake sio kila kitu ni siasa. Naona hakuna anayeongelea hiyo Dice imeangukia 5. yaani aliyebashiri 5 ndio kashinda.

Yaani kichwa hapa ni yule ataweza kuongelea vyote Nyoka mkubwa na Mdogo number 5 nyekundu na Number 5 kwenye Dice.

Mimi tafsiri ninayo
 
Mkuu inawezekana kuwepo na wana ccm hao ndani ya chama pamoja na kutangaziwa kuwa bwana mkubwa ndiyo malaika?
Nabahatisha tu, kuna watu wachache ndani ya ccm wamejitoa muhanga kuhakikisha jamaa haongezewi miaka mingine hiyo 5 inamtosha
 
Hilo ni game la nyoka, ukicheza kete zako vizuri, unaenda kwenye chumba chenye ngazi unapanda, ukicheza kete zako vibaya unaangukia kwenye chumba chenye joka unaliwa unarudishwa kuanza tena moja. Na ndio system inavyofanya kazi wakati wa sasa. Wengi wamecheza kete zao vizuri wamepanda, wengine wamecheza kete zao vibaya wameliwa na nyoka wamerudi kuanza tena upya.
 
kwa mtazamo wangu, nikionacho kipanya safari hii kaamua kupuliza, maana huwa anang'ata na kupuliza
namba 1 hadi 5 ni mihula ya uongozi wa nchi hii tangu rais wa kwanza hadi wa sasa, sasa nyoka mdogo ndio wale mafisadi ambao walizoea kujichotea na kula tu, tena ni wakijani kabisa,
sasa awamu hiyo ya tano wamekutana na ndugu yao wenyewe familia moja, baba mmoja mama mmoja, ila ndio hivyo anawamaliza hao mafisadi(anawameza),
 
Huu mchezo tuliuchezaga mashuleni. Unaitwa 'snakes and Ladders'(nyoka na ngazi). Unarusha kete, namba inayotoka kwenye kete, ndio unavosogeza kwenye mabox hayo yaliyoandikwa moja mpaka tano na kuendelea. Hapo ukiangukia kwenye ngazi, unapanda na kwenda juu zaidi. Ukiangukia kwenye kichwa cha nyoka unashuka chini, nyoka kakukumeza.(kwenye picha ya Masoud kapata tano, kwaio akisogeza mara tano anaangukia kwenye nyoka, na hapo atarudi chini) Mshindi ni ataeweza kucheza na kufika box la 100 kwanza. Tafsiri kisasa hilo.
 
Shukrani kwa kutuongezea madini

Pamoja sana mkuu

Muhula wa mwaka wa Sita baada ya miaka mitano kuisha joka lililotesa watu miaka mitano linajaribu kubahatisha kukamata muhula mwingine kwa mbinu zilezile maana kwa Sasa halibebeki ngazi za kupandia zimeharibika linatumia kamali kuona uwezekano
Joka limeficha meno limevaa vazi safi la kondoo linamezea huruma za wanyonge.Wanyonge wakihadaika kutolifurusha ndani ya nyumba watanyongelewa mbaya msimu wa mvua ukifika.
 
Bado yule msanii matata na mzoefu wa katuni leo hii ametujia na katuni tatanishi na safari hii ili uweze kuisoma inabidi akili yako iwe inachaji.

Kwetu siye kina asante Kayumba hatuja funua kitu.View attachment 1214895

Hapa ukiangalia Nyoka anaemezwa ni wa Kijani.
Mwanzo kabisa kuna ngazi ambayo nyoka huyu wa kijani aliipanda na akaa juu kwa miaka Minne.

Katika mwaka wa nne kuna ngazi nyingine ambayo nyoka huyu wa kijani anaweza kuipanda na kua Juu zaidi. Lakini katika huu mwaka wa nne kuna Joka jingine linaamua kummeza kabisa Nyoka wa kijani kabla hajaipanda Ngazi katika mwaka wa nne ili nyoka huyu wa kijani asiwepo kabisa.

Hii tafsiri yake ni kua chama cha mapinduzi (Nyoka wa kijani) ndicho kilishinda uchaguzi miaka minne iliyopita, lakini baada ya miaka Minne chama kinataka kupanda juu ili kudhibiti hali ndani ya chama lakini kuna Joka halipendi hali hiyo ya chama kua juu na kutokana na nguvu lilopewa Joka hilo linaimeza Nyoka ya kijani kabla ya kuendelea mbele Mwaka wa tano na Sita na inayofuata.

Hapa CCM haipo tena linalobaki ni Joka ambalo wao wenyewe ndo walilisaidia kupanda ngazi pamoja kabla halijajionyesha. Na Chama kwa kulijua hilo wanataka kudhibiti hali hii katika mwaka wa nne lakini Joka nalo linajua Chama kinataka kulidhibiti na hivyo linaamua kukimeza Chama ili liendelee na Safari yake ya Awamu zijazo likiwa litawala la Chama.
 
Ana maanisha kuwa hadi tuna rais hadi wa awamu ya 5 lakini inaelekea rais wa awamu ya sita atamezwa na nyoka
🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄
 
Bado yule msanii matata na mzoefu wa katuni leo hii ametujia na katuni tatanishi na safari hii ili uweze kuisoma inabidi akili yako iwe inachaji.

Kwetu siye kina asante Kayumba hatuja funua kitu.View attachment 1214895
Ngazi inaashiria miaka ya uongoza kwamba baada ya kuingia madarakani watu tulitegemea mabadiliko makubwa.lakini kadili muda unavyokwenda matumaini yanapotea juu yake.

Ngazi katika namba 4 inaashiria kuna ngazi ambayo inapswa itumike kama mwanga ili kuondoa mkwamo wa maendeleo yaliyopo sasa .na kwa maana hiyoo anachomaanisha hapa ni kutumia ngzi namba 4 ambaye ni BKM ili kupata unafu.
 
Bado yule msanii matata na mzoefu wa katuni leo hii ametujia na katuni tatanishi na safari hii ili uweze kuisoma inabidi akili yako iwe inachaji.

Kwetu siye kina asante Kayumba hatuja funua kitu.View attachment 1214895
ka akili zangu naweza kusema kwamba kuna mtu ambaye huwa anacheza hilo game manapolis sijui ndo linavoitwa sasa kuna mahala wametgesha kitu fulani kitu ambacho itu ni egesho tuu na nyuma take kuna kitu kikubwa ambacho kina kula hiko kidogo amabacho mtu huyo anakua anakipata baada ya kushinda ,,mfano katika hali ya kawaida ya maisha unawza kuwa labda unafanya biashara hii ndo bahati nasibu yako..sasa kua mahali au kitu amabacho kipo kimewekwa lets say labada na mwenye kibanda au fremu ya unayofanyia bishara anakuambia hii ni ya ulinzi kumbe ni siyo ni njia mpya tuu ya kutaka kupata kile unachokipata ka bahati kila siku...kwa mawazo yangu
 
kwa mtazamo wangu, nikionacho kipanya safari hii kaamua kupuliza, maana huwa anang'ata na kupuliza
namba 1 hadi 5 ni mihula ya uongozi wa nchi hii tangu rais wa kwanza hadi wa sasa, sasa nyoka mdogo ndio wale mafisadi ambao walizoea kujichotea na kula tu, tena ni wakijani kabisa,
sasa awamu hiyo ya tano wamekutana na ndugu yao wenyewe familia moja, baba mmoja mama mmoja, ila ndio hivyo anawamaliza hao mafisadi(anawameza),
HUJAGUSIA NGAZI HATA KIDOGO
 
Kama chuma ulete tu siyo?

Nakataaa kabisa....ingekuwa ni katuni ya kusifu mamlaka asingeweka "code" ngumu kwa kuwa hakuna MWANACCM anayeweza kuumiza kichwa kiasi hiko.
 
Back
Top Bottom