Swahili AI
JF-Expert Member
- Mar 2, 2016
- 6,212
- 46,836
Leo nataka niwaonyeshe namna ambavyo wakujiita manabii, makuhani, mitume na wengineo wanavyo walaghai wakristo.
Nitafafanua kibiblia kabisa.
Kwanza chanzo cha upotoshaji wa waaumini umetajwa katika Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;
Ni kweli kabisa, wanaangamia kiuchumi, kifikra na kwa kila namna.
Sasa kwanini nayasema haya?
Kitabu cha Matayo 10, Yesu aliwapa wanafunzi wake mamlaka mengi na tofauti {soma, nitaweka kwa uchache hapa}. Moja ya agizo alilowapa kuanzia mstari wa 7 ni: Na mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia;
Agizo namba 1 ni juu ya kurudi kwake kitu ambacho hawafanyi wakiwa kwenye majukwaa yao zaidi ya kuhubiri mafanikio ambapo ni kinyume na andiko
Mathayo 6:33
"Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa." Sina maana tusufanye kazi.
Kisha neno likaendelea kusema:
8 Waponyeni wagonjwa, wafufueni wafu, watakaseni wenye ukoma, wafukuzeni pepo. Mmepokea bure, toeni bure. 9 Msichukue dhahabu, wala fedha wala sarafu za shaba katika mikanda yenu.
Tena akasisitiza kwamba wasichukue mali kutoka kwa hao watu kwa maana wamepewa bure.
Sasa inakuaje mnapangiwa mpaka viwango vya kutoa sadaka ili uonane na huyo nabii/mtume/mchungaji? Au kuuziwa bidhaa fulani ili ukapate uponyaji?
Amkeni wandugu. Biblia imeweka wazi kila kitu ila kwakuwa watu hawasomi wanasubiri kupata miujiza, mtaendelea kupigwa na kupigwa kila siku.