Ni jambo zuri Serikali inavyohimiza tupande miti ila napendekeza ingehimiza tupande miti ya matunda kama machenza mpaka katika barabara zetu

FrankLutazamba

JF-Expert Member
Aug 9, 2018
443
500
Serikali yetu pendwa inaendelea kuotesha maelfu ya mbegu za miti kwa ajili ya kupandwa, pendekezo langu wangekuwa wanapanda miti ya matunda inayodumu na kuchanua kama mipera, machenza, michungwa na kadhalika hata katikati ya majiji katika barabara badala ya miti isiyo zalisha matunda. Ila katika mahali pa kupumzikia ndio ipandwe miti ya kivuli.
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,117
2,000
Ila kuna baadhi ya miti ya matunda kama uliyoitaja wewe, huhitaji matunzo na ufuatiliaji wa karibu muda wote, ndiyo iweze kutoa matokeo chanya.

Sasa ikipandwa kwenye maeneo ya umma kuna shida kidogo katika kuitunza na kuifuatilia, labda miembe, yenyewe hainaga 'kinyaa', popote inakubali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,117
2,000
Mm nataka kupanda miti home. Ushauri wa miti gani mizuri kuweka nyumbani.
Miti ya matunda: michungwa, milimao, mipera na mipapai.

Hiyo utakuwa na uwezo wa kuitunza kwa karibu.

Kwa mfano, michungwa na milimao inahitaji umwagiliaji usiokoma ndiyo ikutolee matunda matamu muda wote, hainaga msimu wa kuzaa, ilimradi ipate maji tu.

Pia michungwa na milimao inatengeneza vivuli vya kutosha kupumzikia.

Ningeshauri mwembe, lakini mti huu unahitaji nafasi kubwa kama ilivyo kwa mkungu.

Sasa kwa viwanja vyetu vya mjini, miti hii ni mizuri lakini ni kitendawili kutokana na eneo.

Kama una kiwanja kikubwa chenye ukubwa wa medium ama low basi waweza panda mwembe ajili ya kivuli na matunda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

christeve88

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
1,168
2,000
Serikali yetu pendwa inaendelea kuotesha maelfu ya mbegu za miti kwa ajili ya kupandwa, pendekezo langu wangekuwa wanapanda miti ya matunda inayodumu na kuchanua kama mipera, machenza, michungwa na kadhalika hata katikati ya majiji katika barabara badala ya miti isiyo zalisha matunda. Ila katika mahali pa kupumzikia ndio ipandwe miti ya kivuli.
Kabisa tena jiji kama la Dodoma ningependekeza ipandwe mizabibu kandokando mwa barabara na katikati mwa mtengano wa barabara.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom