Ni Jambo gani unaloweza kusema Rais Samia hajatekeleza?

Mama tunashukuru kwa kujenga shule nyingi nchini na pia hakuna walimu ni jambo zuri sana usiwalete tu hao waalimu waache waendelee kusota mtaani KWANI watoto watajifundisha wenyewe mpaka waelewe tuu
 
Ndugu zangu Watanzania,

Embu niambieni ndugu zangu Watanzania kuwa ni jambo gani ambalo unaweza kusema kuwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama wa shoka ,jasiri muongoza njia, shujaa wa Afrika na nuru ya wanyonge mh Mama Samia Suluhu Hasssan hajafanya kwa Taifa letu? Kipi ambacho hajagusa? Nini ambacho hajafanya na ambacho kimekuwa kero kwa watanzania? Wapi ambako hajapeleka pesa kwa ajili ya maendeleo? Mkoa upi ambao haujafikiwa na miradi ya Rais Samia?

Niambieni watanzania wenzangu ni jambo gani ambalo watanzania tulihitaji na tulikuwa na kiu nalo na ambalo halijaguswa na Rais wetu? Kundi lipi ambalo halijatendewa haki na Rais wetu? Secta ipi iliyoachwa nyuma? Wapi ambako hakujapelekwa pesa za maendeleo na Rais huyu mcha Mungu ,mchapa kazi, mnyenyekevu, mwenye upendo wa dhati na Taifa letu,mzalendo wa kweli ,akili kubwa na mwenye maono ya mbali?

Nani mwenye afya ya macho na asiye kipofu wa macho na akili hajaona kazi kubwa alizofanya Rais samia kwa Taifa letu? Nani hajaona juhudi za Rais samia? Tunataka Rais Samia afanye nini na kipi ili mioyo yetu iridhike? Changamoto huwa hazikosekani ,lakini je hatuoni juhudi za mama yetu katika kutatua changamoto? Hatuoni mipango mikakati hatua kwa hatua katika kumaliza kero mbalimbali? Hatuoni utayari wake katika kuleta suluhisho la kudumu kwa changamoto mbalimbali? Afanye nini zaidi ya haya afanyayo?

Embu tumuungeni mkono Rais wetu,Tumpe faraja na kumtia moyo, tuendelee kumuombea ili Mungu amlinde,kumpigania na kumtetea dhidi baya lolote, lisiwepo jambo lolote baya litakaloinuka mbele yake.kila mtu kwa imani yake Aendelea kumuombea afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Jinga namba moja la taifa. Umeme mgawo wala haliwezi sema,kila siku kusifia. Shetani kufa wewe, Mungu chukua hili lishetani hasara haraka
 
Mama tunashukuru kwa kujenga shule nyingi nchini na pia hakuna walimu ni jambo zuri sana usiwalete tu hao waalimu waache waendelee kusota mtaani KWANI watoto watajifundisha wenyewe mpaka waelewe tuu
Serikali ya Rais samia imetoa ajira nyingi sana za ualimu na itaendelea kufanya hivyo kwa kadri uchumi wetu utakavyo ruhusu.
 
Back
Top Bottom