Ni ipi logic ya kupewa hela au zawadi yoyote siku ya kuzaliwa kwako?

Yani nimezaliwa tarehe kama ya leo unanipa zawadi au hela kwamantiki gani? kwamba unanipa zawadi kwa kuzaliwa? unanipa hela sababu nimezaliwa leo?

Sijaelewa naomba kueleweshwa
Ni kama graduation tu.... Kwani wanakuvisha taji na kukupa maua kwakuwa umemaliza kazi ya kukariri?
 
Yani nimezaliwa tarehe kama ya leo unanipa zawadi au hela kwamantiki gani? kwamba unanipa zawadi kwa kuzaliwa? unanipa hela sababu nimezaliwa leo?

Sijaelewa naomba kueleweshwa
Hizi ni mila na desturi za wazungu. Waafrika hususani watanzania, hatujawahi kuwa na siku kama hizi. Siku hizi kuna ulimbukeni wa aina fulani na ukienda sehemu za uswazi unaweza kutapika kwa kichefuchefu. Mashanginfi ya huko siku hizi huyaambii kitu kwenye sherehe za birthday, au wenyewe wakiita besidei. Wanwake wa huko wako radhi kubana fedha za matumizi au kutembea na wanaume nje ya ndoa ili mradi tu wapate fedha za kununua keki ya kupiga picha kuweka kwenye mitandao. Wki moja kabla utakuta wanaanza ku post ''besidei roading'' (birth day loading), yaani kichefuchefu tupu.
 
Unapongezwa kwa kuuona mwaka mpya. So pongezi inaendana na zawadi au la.
Ni kama tunavyopumzika Nyerere day... Wengine hufanya dua, wengine huenda kumtembelea mjane, wengine wanapiga ulabu, wengine wanangonoka... ili mradi tu kila mtu ana namna yake ya kuweka kumbukizi.... Haimaanishi kwamba tunafanya hivyo kwakuwa Nyerere alidedi na maua yake....

Cha msingi kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe
 
Ile fathers day ndio mtu anampost mshua na maneno kibao. Vipi siku zingine hastahili haya maneno mazuri na zawadi??? Kwanini iwe mbaka hizo siku tajwa tu ndio haya mambo yawe kwa wingi?? Au ndio technolojia labdaa....
 
Graduu zikiwa nyingi sana maisha yako yote sidhani kama hata 5 au 6 zinafika kwa sisi watanganyika. Birthday ni nyingii alooo....anyways sio kitu mbaya lakini kufanyaaa......ila binafsi naona kama ni utumwa flani hivi wa kisasa
 
Ni kama graduation tu.... Kwani wanakuvisha taji na kukupa maua kwakuwa umemaliza kazi ya kukariri?
heri hio umesoma unahitimu kusoma sasa kuzaliwa? tena mtu anafanya na party sjawah kuelewa hili
 
Yaani nimezaliwa tarehe kama ya leo unanipa zawadi au hela kwamantiki gani? Kwamba unanipa zawadi kwa kuzaliwa? Unanipa hela sababu nimezaliwa leo?

Sijaelewa naomba kueleweshwa
Tumeiga kutoka kwa wazungu, ni kama tulivuoacha kunya pombe za Umkhomboti na sasa watu wanapiga Haineken.
 
Hizi ni mila na desturi za wazungu. Waafrika hususani watanzania, hatujawahi kuwa na siku kama hizi. Siku hizi kuna ulimbukeni wa aina fulani na ukienda sehemu za uswazi unaweza kutapika kwa kichefuchefu. Mashanginfi ya huko siku hizi huyaambii kitu kwenye sherehe za birthday, au wenyewe wakiita besidei. Wanwake wa huko wako radhi kubana fedha za matumizi au kutembea na wanaume nje ya ndoa ili mradi tu wapate fedha za kununua keki ya kupiga picha kuweka kwenye mitandao. Wki moja kabla utakuta wanaanza ku post ''besidei roading'' (birth day loading), yaani kichefuchefu tupu.
sijawah kuelewa zawadi za nn siku yangu ya kuzaliwa, upande wangu hua nina swala maalum ya kumshukuru Mungu kunipa uhai kuongeza siku za kuishi, nawaombea wazaz wangu kwa kunilea had hapa nilipofika na najiombea mwenyewe nizipi kumiminiwa riziki huyo mpenz ni akiniwish her ya siku ya kuzaliwa babe inatosha kabisa
 
Ile fathers day ndio mtu anampost mshua na maneno kibao. Vipi siku zingine hastahili haya maneno mazuri na zawadi??? Kwanini iwe mbaka hizo siku tajwa tu ndio haya mambo yawe kwa wingi?? Au ndio technolojia labdaa....
siku ya baba na siku ya mama hiz ndio siku zakutoa zawad kama mtu unaamua siku ya kuzaliwa sidhan
 
siku ya baba na siku ya mama hiz ndio siku zakutoa zawad kama mtu unaamua siku ya kuzaliwa sidhan
Lakini hata hii pia kwanini uwape zawadi mbaka hii siku ambayo ndio kila mtu utaona anampenda mzazi wake. Usipopost ww unaonekana kama huna upendo na wazazi. Upendo uwepo siku zote tu. Wazazi tena ndio bila wao sisi tusingekuepo......utandawazi pia unachagiza sana haya mambo....huko nyuma hizi 'special days' nina uhakika hakuna aliekua na mpango nazo sana
 
Unapewa zawadi kwa kuwa Muda wa kufa unakaribia. Kadiri Muda unavyoenda ndivyo na mauti yanakusogelea.
 
Ni kukutakia heri tu ndugu,hiyo huambatana na maneno mazuri ya kukutia moyo na kouona mchango wako kwa watu wako.kuna mtu ulimgusa jwa namna moja au nyingine au hata ni kipenz chako anamua kukupa zawadi.ni hongera pia kwa kujitunza maana maisha na afya vinaanza na wewe kwanza
 
Back
Top Bottom