Ni ipi hasa sababu ya Freeman Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa kipindi kirefu hivi?

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Jan 9, 2022
449
1,009
Je, CHADEMA watu wenye hakuna uwezo wa kuwa wenyeviti? Mbona kina Mtei na Bob Makani walimuamini inamaana baada ya yeye hakuna mwingine mwenye uwezo?

Ni kipi kinafanyika kwenye chama chetu CHADEMA kinachoonesha uwepo wa Demokrasia? Ni miaka zaidi ya 20 mwenyekiti yule yule.

Binafsi kama mwanachama huwa najiuza hili swali nikiuliza najibiwa akiondoka chama kinakufa, je kweli?

Je, hakuna namna ikawekwa misingi Imara kama ilivyo kwa Republican na Democratic US?

Au kuna elements za dictatorship kama

Kuamini hakuna mtu mwenye uwezo zaidi yako

Tamaa ya kuendelea kuwepo madarakani?

Kuna muda naona kama anafanya vitu ambavyo vinaipa faida sana CCM kuliko CDM naona akipumzika akawa Mlezi wa chama kinaweza songa mbele zaidi .
 
Sababu ni moja tu, Muda haujasema na pengine mbingu bado iko upande wa Mh.Mwenyekiti kuendelea kuhudumu katika nafasi yake kama ambavyo CCM inavyoutumia Utamaduni wao kwa Rais kuhudumu mihula miwili.

Kupanga ni kuchagua na hivi ndivyo ilivyo kwa Nchi nyingi za Kijamaa ikiwemo na sisi.
 
Kiukweli hili halileti picha nzuri kwa chama kinachojipambanua kwa demokrasia.

Kama chama tu anakaa madarakani miaka 20, nchi itakuwaje?
Hili linawapa sababu CCM ya kuwadhihaki kwa wananchi na ni ukweli ambao haupingiki.

Mbowe ni moja ya wanasiasa mahiri na historia itamkumbuka kwa hilo, lakini mtumbuizaji bora ni yule anayejua muda wa kuondoka jukwaani.
 
Hawa ndio huwa wanabadili katiba
 
Je CHADEMA watu wenye hakuna uwezo wa kuwa wenyeviti ? Mbona kina Mtei na Bob Makani walimuamini inamaana baada ya yeye hakuna mwingine mwenye uwezo ?

Ni kipi kinafanyika kwenye chama chetu CHADEMA kinachoonesha uwepo wa Demokrasia ? Ni miaka zaidi ya 20 mwenyekiti yule yule .

Binafsi kama mwanachama huwa najiuza hili swali nikiuliza najibiwa akiondoka chama kinakufa ,je kweli ?

Je hakuna namna ikawekwa misingi Imara kama ilivyo kwa Republican na Democratic US ?

Au kuna elements za dictatorship kama

Kuamini hakuna mtu mwenye uwezo zaidi yako

Tamaa ya kuendelea kuwepo madarakani ?

Kuna muda naona kama anafanya vitu ambavyo vinaipa faida sana CCM kuliko CDM naona akipumzika akawa Mlezi wa chama kinaweza songa mbele zaidi .
Chadema ni chama cha familia, ni family business. Ndio maana siwaelewagi
 
Kiukweli hili halileti picha nzuri kwa chama kinachojipambanua kwa demokrasia.

Kama chama tu anakaa madarakani miaka 20, nchi itakuwaje?
Hili linawapa sababu CCM ya kuwadhihaki kwa wananchi na ni ukweli ambao haupingiki.

Mbowe ni moja ya wanasiasa mahiri na historia itamkumbuka kwa hilo, lakini mtumbuizaji bora ni yule anayejua muda wa kuondoka jukwaani.
Wewe kakate vitunguu huko, unamuwaza mbowe wakati hapo kwa huyo geto la mumeo wa tamisemi mko gizani saa hizi umeme hamna na kesho hamna uhakika wa kunywa chai
 
Back
Top Bottom