Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 674
Mafundi warejea kushughulikia umeme Z`bar
2008-06-02 09:32:07
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema wataalam wa umeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wamerejea tena Zanzibar kuanza kazi ya matengenezo ya njia ya umeme iliyoharibika katika eneo la Fumba wilaya ya Magharibi Unguja.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Bw. Mausosur Yusuf Himid alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kufuatia kukosekana kwa umeme visiwani hapa kwa wiki mbili.
Alisema matengenezo hayo yanashirikisha jopo la mafundi kutoka Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) na wataalam wengine kutoka nje.
``Kazi ya matengenezo inaendelea huku tukiendelea kusubiri wataalam walioshughulikia mradi huu na wakati wo wote watawasili toka Norway na Ufaransa,`` alisema.
Alisema hadi sasa serikali imefanikiwa kudhibiti tatizo la uhaba wa maji baada ya kuweka majenereta katika vyanzo vya maji, lakini serikali imeagiza jenereta nne kutoka Tanzania Bara ili maeneo yaliyosalia yawe yanapata huduma hiyo.
Awali wataalam kutoka TANESCO waliondoka Zanzibar baada ya kushauriwa na SMZ wasifanye matengenezo hadi watalaam kutoka nje watakapowasili.
Wakati huo huo, Rais Aman Abeid Karume anaondoka kwenda Italia kuhudhuria mkutaano wa wakuu wa nchi unaohusiana na Usalama wa Chakula Duniani na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi na matumizi ya nishati inayotokana na kilimo.
Taarifa ya serikali imesema kuwa Rais Karume anamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano huo unaotarajiwa kuanza Juni 3 hadi Juni 5.
Rais Karume ameandamana na mkewe, Mama Shadya, Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Muungano, Stephen Wassira na Waziri wa Kilimo na Mifugo Zanzibar, Burhan Saadat Haji.
Taarifa ilisema kwamba mkutano huo una lengo la kutafuta hatua za pamoja katika kushughulikia upungufu wa chakula duniani uliosababisha mfumuko wa bei na kuathiri nchi mbalimbali duniani, hususan Afrika.
Wakati huo huo, Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, anaondoka kesho kuelekea Afrika Kusini kwa ziara ya wiki moja.
Taarifa ya serikali imesema kwamba akiwa nchini humo Waziri Kiongozi atakutana na viongozi mbalimbali wa serikali nchini humo.
SOURCE: Nipashe