Wana JF.Hili swala la kumwabudu marehemu au kumwombea wakati yeye kashakufa na hana ufahamu wowote kweli ni jambo jema? Maiti haijui wala haisikii nijuavyo mimi sijui wenzangu mnajuaje? Maiti haina thamani yoyote hata fungu la mchicha la mia mbili inaizidi thamani nijuavyo mimi.Naombeni na nyie mawazo yenu kuhusu hili watu wa jf.
kuabudu sio haki. ni maamuzi binafsi, ndio maana unaweza kutoabudu chochote au yeyote.
pia kuombea na kuabudu ni mambo mawili tofauti.
kwa mtazamo wangu haina maana sana kwa kua maiti ni sehemu ya tuchokipata kutokea kwene dunia hii na kuzika ni part ya kukirudisha so kuombea maiti...ni kupoteza mda......kitokacho kwa Mungu ndio kinarudi kuhukumiwa na hukumu inatokana na namna mtu alivotumia mda wake duniani kufanya mema au mabaya...cdhani kama maombi yanaweza kubadilisha chochote
Pumzi ya mungu + udongo = MTU. Na MTU toa pumzi inabaki UDONGO.
Sasa unapoabudu udongo maanake akili yako sio timamu. Abudu aliefinyanga huo udongo na kupulizia pumzi yake akatokea adam
Mawazo bhana! Kweli unaamini MUNGU wetu mtukufu atuumbe atupe thamani ya juu and then aje atutese duh!
Nadhani uanhitaji kuelewa kuwa kuabudu na kuombea ni tofauti kabisaa.
Soma Mhubiri 9:5 inasema Mtu akifa hajui neno lolote.Pia Mungu anasema usiabudu kitu chochote isipokuwa Mungu wa Mbinguni peke yake. Kwa hiyo ibada za wafu ni ibada za mizimu na Mungu amezikataza.
Kama mngalijua,imani ni kitu kigumu sana!
hata kama ni imani je ni sahihi kumwabudu marehemu au kumwombea maana marehemu hajui na hajijui kabisaa.
Wana JF.Hili swala la kumwabudu marehemu au kumwombea wakati yeye kashakufa na hana ufahamu wowote kweli ni jambo jema? Maiti haijui wala haisikii nijuavyo mimi sijui wenzangu mnajuaje? Maiti haina thamani yoyote hata fungu la mchicha la mia mbili inaizidi thamani nijuavyo mimi.Naombeni na nyie mawazo yenu kuhusu hili watu wa jf.
hivi wanaosherekea pasaka huwa wanakosea?
Sasa swali lako unataka lijibiwe kwa misingi ipi?maana chukulia mfano hapa afrika tunaupinga ushoga ila wazungu kwao ni jambo la kawaida,kwahiyo na swali lako sijajua tulijibu kwa misingi ipi.
We umejuaje kuwa marehemu hajijui?
Hapa unataka tuu kuleta mgongano wa imani wewe, off pointhivi wanaosherekea pasaka huwa wanakosea?
Hapa unataka tuu kuleta mgongano wa imani wewe, off point
Soma Mhubiri 9:5 inasema Mtu akifa hajui neno lolote.Pia Mungu anasema usiabudu kitu chochote isipokuwa Mungu wa Mbinguni peke yake. Kwa hiyo ibada za wafu ni ibada za mizimu na Mungu amezikataza.
marehemu anaweza kuombewa akarudi duniani , je kuna uwezekano wa kumuombea kwenda mbinguni.