Ni dawa gani ya kupaka(Tube)inayosaidia kuondoa chunusi au mashimo usoni ambayo hutengeneza utando mweupe.

Clark boots

JF-Expert Member
Jun 5, 2017
6,402
5,527
Habarini jamani..
Naomba kufahamishwa tube nzuri (dawa ya kupaka) usoni ambayo inaweza kuondoa chunusi au mashimo usoni ambayo yanapelekea kutengeneza utando(ugaliugali) mweupe kwa ndani.
Kama umewahi kukutanana hizi chunusi/mashimo mwenzangu ulipona kwa dawa gani..?
 
Habarini jamani..
Naomba kufahamishwa tube nzuri (dawa ya kupaka) usoni ambayo inaweza kuondoa chunusi au mashimo usoni ambayo yanapelekea kutengeneza utando(ugaliugali) mweupe kwa ndani.
Kama umewahi kukutanana hizi chunusi/mashimo mwenzangu ulipona kwa dawa gani..?



Komamanga: Maganda Ya Mkomamanga yaliyosagwa, yakichanganywa na habbat sodah ya unga, hutengeneza dawa nzuri ya asili ya kuondoa tatizo la vipele vya usoni ( chunusi )

Kuna idadi kubwa ya watu wanao kabiliwa na tatizo la vipele vya usoni
( Chunusi). Kuwa na chunusi ni jambo lenye karaha sana, kwani linakufanya upoteze mvuto wako wa asili na hivyo kukukosesha raha.
Zipo njia mbalimbali za asili zinazo weza kutumika kutibu tatizo la chunusi na vipele vya usoni.
Ifuatayo ni miongoni mwa njia bora kabisa na ya uhakika itakayo kusaidia kuondokana na tatizo la Chunusi au vipele kwenye uso.


Habbat Soda : Hii ni Habbat Sodah Ya Mbegumbegu. Habbat Sodah iliyosagwa ndio inayo hitajika katika kutengeneza dawa ya asili ya kuondoa tatizo la vipele vya usoni ama chunusi.


MAHITAJI :
i. Habbat Sawdah ya Unga iliyo sagwa.
ii. Nusu kikombe ya maganda ya komamanga yaliyo sagwa.
iii. Nusu kikombe ya siki ya tofaha(apple cider vinegar )

MATAYARISHO NA MATUMIZI

Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu)
kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple).

Paka katika sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila siku usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubarid.

NJIA HII IMETUMIWA NA WATU WENGI NA IMEWASAIDIA SANA. JARIBU NA WEWE KUTUMIA NJIA HII UONE MAFANIKIO YAKE.

Kwa habari na taarifa mbalimbali kuhusu masuala ya tiba zitokanazo na dawa za mimea na vyakula lishe
 
Back
Top Bottom