Kutokana na yaliotokea na ambayo yanaendelea kutokea nnaiomba serikali kwa kuangalia sheria zinavyoelekeza kuhusu uwepo wa vyama ambavyo vinawagawa watanzania, vinachochea uvunjifu wa amani, udini na ukabila kuwa ni vyama visivyohitajika tanzania
kwa hio nnaomba kama mwananchi mwenye mapenzi ya nchi yengu chama hiki kifutiwe usajili na viongozi wake wakumbane na mkono wa sheria
OOOOOOOOH GUYS,, :hungry: THIS MAN WHO POSTED THE TOPICS ANAFIKIRI WE LIKE SUCH CCM WE TIRED FOR EXPLOITATION WE NEED RIGHT TOWARDS OUR OWN LIFE....SASA YEYE HAS LIFE GIVEN BY CCM THATS WHY ANATAKA CDM IFUTWE MY FRIEND UR STILL ASLEEP WHILE US WE WAKED UP WE DONT WANT TO BE RULED OUT LIKE CUF. MTAISHIA KUSHIND KIUJANJA UJANJA KILA SIKU. WANASEMA MAENDELEA HAYAJI KWA BAHATI MBAYA LAZIMA WATU WAJITOE MUHANGA...NDIO CHADEMA YENYEWE... POLE SANA FOR FEW SUPPORT. TEHE TEHE TEHE.
Umesahau wana watu zaidi ya mil 2.2(jumlisha uchakachuaji??)?? Hahaha unataka nchi ifumuke nini?? Maana sasa ndio tutajua kuhesabu wafuasi kwa kutumia kidole tuu.. Kila nyumba itaulizwa jumlisha kituo cha oysterbay(ambacho Slaa alipata kura 58 na JK 54)... Watu walijua pale ndo wasaliti kumbe weee nchi nzima hahawawataki CCM... Mkwere kapata pwani tuu na Unguja kwishnei.....
Ulitaka msimamo wa aina gani?? kama Ivory coast au?? Mi hata sikuelewi maana hujui tume ilifanya nini siku ile?? CHADEMA walipewa mill 66 kila mwezi kuanzia 2005/10 lakini wamepanda wafuasi kutoka 6% to 26%.. Hao CUF unaosema walikuwa wakipata mill 99 lakini uliza walitoka wapi kwenda wapi kama sio 11% to 8% ooh shame on Lipumba bora arudi Stanford atufundishe uchumi tuu siasa kipaji sio bahati!!!
Wao(CUF) walikubali mshindi huku wakidai tume sio huru...nafuu CHADEMA wanajua wanachokifanya .. wametoka bungeni na hisia za katiba mpya na tume huru zikaingia... Lakini CUF wamedandia mada kama wanaharakati uchwara waliojaa tanzania....
CUF ina wabunge 2 na wengine zanzibar... Lakini CHADEMA ina wabunge 23 huku kwetu Tanganyika.. Labda kakigute Zanzibar na CUF kifutwe huku Tanganyika..
Nawasilisha
Baba wa Taifa alipofariki Chadema ilikuwa haipo ? Nyerere alimwita Seif Sharif Hamad Butiama wakafanya private masungumso ,hakuna kiongozi yeyote yule aliewahi kufanya masungumso ya siri na Mwalimu au yupo ? Sema basi kama ni Slaa ,Slaa amevamia mambo ya watu lakini nakuhakikishieni kabisa hawezi hawezi hawezi kufanya kazi ya siasa ,ataulisha watu kwa maelufu ,na nyie angalieni kauli zake hata macho yake yanaashiria ubabe.Na ndio huyo kishawasukuma watu bila ya mpango !Bila shaka umechanganyikiwa. Nyerere alitabiri kuwa CHADEMA ni chama mbadala
Baada ya kupoteza dira na mkondo wa siasa za kidemokrasia, na dhamira halisi ya kuwepo upinzani, chadema kimepoteza uhalali wake wa kisiasa hivyo hakuna sababu kuwapo katika daftari la msajlli wa vyama vya siasa Tanzania, hivyo kifutwe!
Nasema hivyo kwa sababu chadema baada ya kukubali mtego wa CCM wa kupenyeza mamluki ndani ya chama chao wakiwamo magwiji wa usalama wa taifa wastaafu (Mabere N. Marando), pamoja na magwiji wa siasa za kipropaganda kutoka CCM (John M. Shibuda), hakina tena ile rangi yake ya siasa za upinzani.
Akina Marando wanafanya kazi yao ndani ya chadema, ya kushawishi vurugu makusudi ili kuharibu muelekeo wa chadema ulionza nao, naye ameshafanikiwa hilo, kama alivyofanya na kufanikiwa akiwa ndani ya NCCR-Mageuzi, yeye na Agustino Mrema.
Maoni yangu, chadema kifutiliwe mbali, tayari kimeshajionyesha au kimeshafanywa kijionyeshe kuwa hakitaki siasa za ushindani bali vurugu na kuleta machafuko nchini.
Mbali na kugeuzwa huko kwa hila za makusudi, chadema kimegeuka na siyo chama cha matumaini kwa wantanzania kama kinavyojidai, au kinavyodanganya wananchi, kwani ndani ya dhamira za baadhi ya viongozi wao ni kukifanya chama kuwa mtaji wa kukuza vitega uchumi vyao na kujipatia fedha tu.
Chama kinachojiita, au kinacholazimisha kuwa ni chama rasmi cha upinzani bungeni hali ya kuwa hakiwakilishi jiografia ya upinzani wa Tanzania, hakiwezi kuwa na uhalali wa kusimama na kujiita chama cha kitaifa, hivyo kifutwe!
Wakati bunge la Tanzania lina vyama vingi na wabunge wa vyama kutoka maeneo tofauti, chadema kama chama rasmi cha upinzani bungeni kinawakilisha majimbo kinayoyaongoza tu, katika serikali yao kivuli, wakati wananchi wa maeneo mengine ambao wamechaguwa upinzani pia hawana uwakilishi wowote ndani ya serikali kivuli ya chadema.
Kwa maana hiyo basi chadema wamepoteza uhalali wa kuwa chama cha kitaifa, hivyo Kifutwe!
Ikiwa Chadema imeshindwa na ustaarabu bora Msajili akifute Chama hiki,chama ambacho kinashindwa kujidhibiti na kuwezaa kufuata mkondo wa kisiasa,kwa nini hawaiangalii CUF wapi imetoka na wapi ipo ,hii leo !!
Mimi nawashauri Chadema wasitishe kuingia kwenye Bunge mara moja,nawahakikishia serikali itabadili muelekeo ,ni lazima itabadili muelekeo na vile vile lile lengo la kutomtambua Kikwete kama Raisi halali au alieshinda kihalali, hapo hapana ubishi ni lazima CCM na serikali yake ikae sawa na ni njia moja ya kidemokrasia kabisa.
Lakini kuwarubuni wananchi wakati mnaingia bungeni na kula na kusaza ,hili halikubaliki kabisa kisha kutaka kuwaburuza wananchi kwenda kuchezea maji ya washawasha ,nyie wabunge mnakuwa tandize na majokofu ya jumba la bunge,huo utakuwa utapeli kushinda wa mafisadi,amueni moja tuwafahamu.
Mimi ni mwanachama wa CCM toka mwaka 1987, ni kiongozi ndani ya CCM katika ngazi ya Wilaya lakini kwa mara ya kwanza hapa JF nimechukizwa na hii Post haiwatendei haki CHADEMA, so far sijaona kosa walilofanya mpaka wafungiwe na ndo maana hawajapelekwa mahakamani na wakapatikana na hatia hizo, unajua kwa haya malalamiko yetu inaonyesha hatutaki changamoto za kweli na hatupendi vyama vya upinzani viwe strong. Nadhani sisi CCM tuwe wa kweli wananchi wamechoka na ubabaishaji wetu chini ya huyu kiongozi wetu wa kitaifa tunatakiwa tujipange vinginevyo watatushinda kwa hoja mbele ya wananchi.
Natofautiana sana nawewe kwa hii thread