Ni Biashara ipi iko na faida mzuri

Ni Biashara ipi iko na faida mzuri

Fanya kitu ulichokizoea chenye kukupa faida achana na mawazo ya biashara gani nzuri yenye faida kubwa. Utakuja kulia Bure, mara nyingi lakini sio asilimia zote faida ni uzoefu wa biashara ndio maana katika kila biashara kuna wanaopiga pesa na Kuna wanaopoteza mtaji.
 
Umemuita secretarybird hatabiriki kichwa chake anakijua yeye tu anaweza akaja na ushauri mzuri au akasema kitu 😁
Mi naona biashara inategemeana na mtu inaweza kukubali kwa hyu na ikakataa kwa mwingine ila mimi ningefungua ki mgahawa ka kiana. Au ampe barcelona na moroco over 2.5 alafu amuue man u apige mil 100 kuendelea 😅
 
Kwenye hii Dunia kila kitu kina faida na changamoto zake.

Hakuna kitu chochote kilicho na uzuri tu au faida tu, pasipo hasara.

Ukijiandaa kwa uzuri na faida tu, ni kujidanganya.
 
Fanya kitu ulichokizoea chenye kukupa faida achana na mawazo ya biashara gani nzuri yenye faida kubwa. Utakuja kulia Bure, mara nyingi lakini sio asilimia zote faida ni uzoefu wa biashara ndio maana katika kila biashara kuna wanaopiga pesa na Kuna wanaopoteza mtaji.
Huu ni kati ya ushauri nisio ukubali
Kwa hiyo kama mtu alikuwa anauza Baiskeli akaona hazilipi aendelee kuuza hizo hizo kwa kuwa amezoea?
Faida ya biashara hutegemea; Eneo, Eneo, Eneo ulipo, na vitu vingine kama ukubwa wa mtaji, Kujitangaza, ushindani uliopo na uwezo wa kuisimamia
 
Umemuita secretarybird hatabiriki kichwa chake anakijua yeye tu anaweza akaja na ushauri mzuri au akasema kitu 😁
Mi naona biashara inategemeana na mtu inaweza kukubali kwa hyu na ikakataa kwa mwingine ila mimi ningefungua ki mgahawa ka kiana. Au ampe barcelona na moroco over 2.5 alafu amuue man u apige mil 100 kuendelea 😅
Huu ushauri wa mgahawa sawa ila huu wa pili ndugu muomba ushauri anapoishi kuna magorofa marefu sana Kwahiyo haumfai 😅😅😅
 
Waungwana naomba munisaidie mwenzenu nimejichanga na kupata TZS 40,000,000/ ila kwa kweli nimeshidwa kuona ni Biashara gani ya kufanya

Naomba msaada kwenye tuta wasichana wasije kuchungulia mifuko yangu
40m ni mtaji mzuri hapo anzisha min hardware hapa utakua unauza

• Rangi
•vifaa vya bomba
•vifaa vya umeme
• tools na accessories za ujenzi

Kama uko dsm frame yako isiwe mbali sana na k.koo, hii itakusaidia kuchukua mzgo faster kwa vile vitu ambavyo mteja anahitaj na dukani havipo
Note: usiingize hiyo 40m kwenye biashara anza na 25m then 15m ibaki ikisubiria deals za hapa na pale coz kwenye biashara mara nyingi inatokea mteja anataka mzigo ambao huna na anakuamini kwavile tayar una frame
 
Umemuita secretarybird hatabiriki kichwa chake anakijua yeye tu anaweza akaja na ushauri mzuri au akasema kitu 😁
Mi naona biashara inategemeana na mtu inaweza kukubali kwa hyu na ikakataa kwa mwingine ila mimi ningefungua ki mgahawa ka kiana. Au ampe barcelona na moroco over 2.5 alafu amuue man u apige mil 100 kuendelea 😅
Wakuu, someni hiki kilichonikuta hapa chini 👇 miaka ya nyuma baada ya kuomba ushauri kwa motivational speaker 🔊.

Cc Legend joba.
Mbaga Jr
Vincenzo Jr.
 
Kama huna akili ya biashara tafuta njia nyengine ya kuwekeza ndugu.

Unaweza kuwa na million Mia 2 na kuanzisha biashara miaka mitano baadae huna hata jero.

Wakati huo huo kuna mwamba kaazia na laki tu miaka mitatu ana miliki mali ya bilioni. Biashara zina Siri kubwa sana
 
Waungwana naomba munisaidie mwenzenu nimejichanga na kupata TZS 40,000,000/ ila kwa kweli nimeshidwa kuona ni Biashara gani ya kufanya

Naomba msaada kwenye tuta wasichana wasije kuchungulia mifuko yangu
Tulia kwanza na usiwe mwepesi kushawishiwa na biashara zenye faida nono bila kuambiwa changamoto zake
 
Waungwana naomba munisaidie mwenzenu nimejichanga na kupata TZS 40,000,000/ ila kwa kweli nimeshidwa kuona ni Biashara gani ya kufanya

Naomba msaada kwenye tuta wasichana wasije kuchungulia mifuko yangu
Kama huna uzoefu na biashara, basi ni bora hiyo hela ukaenda kuiweka benki kwenye fixed account mpaka pale utakapokuwa na wazo la uhakika. Au kama unaweza kuwekeza kwenye real estate kwa kujenga nyumba ya viwango vizuri, halafu upangishe.

Ukiruhusu mawenge yakupitie, baada ya muda utajikuta huna kitu. Biashara inahitaji umakini wa hali ya juu! Ulinzi makini wa mtaji! Usimamizi makini wa muda wote, kupambana wakati wote dhidi ya washindani wako, ukatili wakati fulani na umafia ndani yake! nk. Ukileta ubosi kwenye biashara, utashindwa asubuhi tu na mapema.
 
Back
Top Bottom