Ni Biashara ipi iko na faida mzuri

Ni Biashara ipi iko na faida mzuri

Kama huna uzoefu na Biashara bora uchukue hizo hela weka UTT au Nunua Hisa, Kuwa makini kama utanunua Hisa unaweza poteza hela zote.

Iendelee kuzalisha wewe uendelee kutafuta zingine. Biashra ya kushauriwa siyo nzuri kuweka hela zako zote 🤔🤔🤔
 
Iyo pesa ni nzuri sana .Tuliza akili kwanza usiwekeze katika biashara moja . 2 usiwekeze katika biashara yenye mtaji mkubwa bali tafuta biashara ndogo yenye mzunguko mkubwa mfn Biashara kuuza chakula . 3. Hakikisha iyo biasha unaisimamia kwa 90%.... UTAKUJA KUNISHUKURU .
 
Huu ni kati ya ushauri nisio ukubali
Kwa hiyo kama mtu alikuwa anauza Baiskeli akaona hazilipi aendelee kuuza hizo hizo kwa kuwa amezoea?
Faida ya biashara hutegemea; Eneo, Eneo, Eneo ulipo, na vitu vingine kama ukubwa wa mtaji, Kujitangaza, ushindani uliopo na uwezo wa kuisimamia
Niliposema biashara aliyoizoea ni kwa sababu mtu anajua changamoto zake hivyo ni rahisi kuzitatua. Nashukuru umeongeze kuhusu location na mie nasema mtu anakuwa anajua wapi apate mzigo kwa bei nafuu na nikipindi gani bidhaa zinatoka sana na aina gani ya bidhaa inafaida.

Hivyo ushauri wangu hauzuii kubadili biashara bali ni kuanza biashara nyingine kwa tahadhari bila kuacha ile uliyoizoea.

Ukiwa tayari umeishaifahamu vizuri hiyo mpya ndio unaweza kufungua ya zamani
 
Nadhani kabla ya kushauri ni biashara gani ufanye na hiyo 40m kwanza ungeelezea mambo ya msingi yafuatayo;
1. Umejichanga hiyo 40m kwa mda gani?
2. Umejichanga kwa kufanya shughuli gani?
3. Umejichanga kwa mda gani
4. Katika kujichanga ulikuwa na malengo gani
5. Una umri gani na uko katika hatua gani ya kimaisha

Angalizo:
Bila kuwa na majibu sahihi ya maswali haya ushauri wowote utakaopewa na kupokea ni batili.
 
Waungwana naomba munisaidie mwenzenu nimejichanga na kupata TZS 40,000,000/ ila kwa kweli nimeshidwa kuona ni Biashara gani ya kufanya

Naomba msaada kwenye tuta wasichana wasije kuchungulia mifuko yangu
Unaonaje tukianzisha biashara ya mikopo ila kwa mtaji wa Milioni 10 tu kwanza.

Lengo ni dhamana nzuri kama viwanja tu.

Walengwa wawe ni watumishi wenye uwezo wa kurejesha hela zetu.

Mfano mkopeshe laki 5 mwisho wa Mwezi arejeshe laki 6 na nusu.

Screenshot_20251221-224347.jpg
 
Umemuita secretarybird hatabiriki kichwa chake anakijua yeye tu anaweza akaja na ushauri mzuri au akasema kitu 😁
Mi naona biashara inategemeana na mtu inaweza kukubali kwa hyu na ikakataa kwa mwingine ila mimi ningefungua ki mgahawa ka kiana. Au ampe barcelona na moroco over 2.5 alafu amuue man u apige mil 100 kuendelea 😅
kama wewe ndo umetoa huu ushauri basi secretarybird atakuja na ushauri wa ajabu zaidi. maana mimi nilitegemea wewe ndo afadhali kidogo

anyway, me naona aendelee kufanya hicho kilichompa 40m
 
Waungwana naomba munisaidie mwenzenu nimejichanga na kupata TZS 40,000,000/ ila kwa kweli nimeshidwa kuona ni Biashara gani ya kufanya

Naomba msaada kwenye tuta wasichana wasije kuchungulia mifuko yangu
uza sigara za jumla weka 30m
 
kama wewe ndo umetoa huu ushauri basi secretarybird atakuja na ushauri wa ajabu zaidi. maana mimi nilitegemea wewe ndo afadhali kidogo

anyway, me naona aendelee kufanya hicho kilichompa 40m
Mkuu ona kilichonikuta miaka ya nyuma baada ya kuwasikiliza motivation speakers.
Ona 👇

 
Piga mishe hiyo hiyo iliyokupa hizo mil 40 mkuu
 
Mkuu ona kilichonikuta miaka ya nyuma baada ya kuwasikiliza motivation speakers.
Ina 👇

Hahah ulikosea sehemu ndogo sana, ni kweli ilikuwa ni fursa ila wewe ungeenda kununua ARV uwauzie, badala yake ukaenda kuagiza mabalo ya condom dah 😂😂😂

hiki kichwa 🙌🙌🙌
 
Back
Top Bottom