Ni benki gani huwa zinasaidia wanafunzi wa Vyuo Vikuu (bachelor degree students) wanaokosa mikopo kutoka HESLB

Lexus SUV

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
4,193
5,123
Habari za leo wakuu?

As regard with the heading above, ninapenda kuulizia ni benki zipi zinaweza wasaidia wanafunzi wa vyuo vikuu, mikopo ya ada tu (tuition fees), ili kufanikisha upatikanaji wa elimu kwa mlengwa?

At any interest rate and which can be paid after completion of studies, maana kuna wanafunzi wa Vyuo Vikuu kadhaa wamekosa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo (HESLB), shida kubwa kwao wanahitaji elimu. Tatizo linalokuja wao ni kukosa tuition fees.

Naombeni ushauri wenu.

Asanteni kwa kunisikiliza na karibuni.
 
Hebu fuatiria na NSSF kuna scheme flani niliiona kuhusu mkopo wa elimu!.
 
CRDB wanatoa ila wanatoa tu kwa ambao wamepata mkopo alafu asilimia chache, hivyo wao wanaongezea asilimia zilizobaki lakini kama hujapata kabisa mkopo wao hawatoi mkopo.
 
Asanteni jamani ,nimshauri jamaa akomae kiume tu , maana ndiyo kukuwa huko , changamoto katika kutafuta elimu haziepukiki .
 
Kati ya ABC au NBC kuna bank inatoa mkopo kwa wanafunzi ila kimsingi ule mkopo ni kama anakopeshwa mdhamini wako ambaye ni lazima awe mfanya kazi wa serikali na atakatwa hiyo hela kwenye mshahara wake kama wanavyokata madeni ya kawaida.
 
Back
Top Bottom