Ni aibu taifa letu kuwa na Waziri wa Nishati anayesisitiza mgao wa umeme bila kutuhakikishia JNHP itaanza uzalishaji lini

Well said mkuu Omulasil
Big up kwa kusema Ukweli.
 
Ushamba ni nini
 
Sijawahi kuona kiongozi kilaza Tanzania kama huyu kijana
 
Mimi mwana if mwenzenu, nimefanya mahojiano na Waziri JM na hizi hoja, amezijibu vizuri kwenye mahojiano yangu msikilize hapa kuhusu JNHPP
Pia Waziri JM, amezungumzia issues mbalimbali za Nishati ya umeme, gesi, umeme jua, mkaa, kuni etc
P
Mkuu Pascal hapa sijaona alipojibu hoja za Bwawa kukamilika zaidi ya kuchepusha topic kwenda kwenye njia za usambazaji za dollar 800

Tusaidie hapo... na je kwenye mkataba hakukuwa na ujenzi wa distribution lines Au Tanesco hawakua na huo mpango kabla ya waziri huyu ?

Tumeona kwenye SGR Tanesco wakienda sambamba Na mkandarasi kwa kujenga mifumo ya umeme Na usafirishaji wake Vipi kwenye bwawa linalowahusu wao 100% wasahau hili ? 😰😂
 
Huyu jamaa anazidi kuonyesha jinsi anavyopwaya kwenye uongozi.

Ujenzi wa bwawa na vitengo vyake vyote, ukamilishwaji wake hatua kwa hatua, viliishaelezwa vizuri tu na mzalendo mmoja huko TBC.

Paschal naona umemtafuta/amekutafuta kwa lengo la kujisafisha.... Kimsingi hakuna alichosema cha maana zaidi ya kuuza sura.
 
Kwa viongozi vilaza kama hawa tusitegemee maajabu. Kufanya kitu kile kile huku ukitegemea matokeo tofauti ni insanity.
 
Mmliki wa bwawa ni Tanesco ndio mwenye wataalamu wa Nishati,kwanini tusimuulize anaweza akawa na majibu ya uhakika.

Pili yupo mkandarasi Arab Contractor ndie mjenzi mkuu wa mradi , pia kuna project consultant nao wanaweza wakatoa majibu.

Mwisho malipo ya mradi yakoje,isije ukakuta kuna ukata.Tumeaona mradi wa SGR Dar-Moro licha ya serikali kujitutumua ilishindwa kabisa kuikamilisha na kuanza kutumika miaka 5 ya Mjomba Magu na sasa zaidi ya mwaka ya SSH.

Kumekosekana tranparency kwa miradi yote miwili.Utafikiri hawakuwa na plan.
 
Mwenzako RPC wa Kagera aliomba Rais amteue kuwa IGP na wewe omba uteuliwe kuwa Waziri wa Nishati ila kwa sharti moja tuu la kuhakikisha umeme haukatiki..

Failure to do that utawajibishwa sio kwa kutenguliwa bali na Kwa kulitapeli Taifa kwamba unaweza kudhibiti kukatika kwa umeme..

Maana ujinga umewazidi Sana nyie kenge hata mkiambiwa ukweli huwa hamtaki.

Waziri amesema kuna tathmnini upya inafanywa Kati ya Tanesco,Wizara na Mkandarasi Ili wakubaliane tarehe mpya ya kukabidhiana mradi baada ya June 22 kutowezekana kutokana na sababu alizozieleza hapo awali.
 
Wewe kwa akili yako mbovu Waziri anaweza kujipigia pesa bila Serikali/Baraza la mawaziri kufahamu?

Ndio hivyo sasa mkataba wa awali haukuwa na hicho kipengele sasa unaposema haiwezekani tupe wewe mkataba wenu wa awali tujiridhishe.

Kwani Wewe unaniamini Sana Serikali ya awamu ya 5 au ndio unataka kutuaminisha kwamba ile serikali haikuwa ya wapigaji wa 10%?
 
Narudia. Kwenye swala la nishati ya taifa yeyote anaye hujumu kwa namna yoyote huyo ni adui namba moja. Kwa hili Akumbukwe Magufuli. Nitasimama na msimamo huo milele na milele.
Unamfahamu yeyote aliyekuwa anahujumu?

Mhujumu wa kwanza na Magufuli kwa kuchukua pesa za Tanesco na kuleta Mkandarasi asiye na uwezo wala mtaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…