Ni aibu taifa letu kuwa na Waziri wa Nishati anayesisitiza mgao wa umeme bila kutuhakikishia JNHP itaanza uzalishaji lini

Sitaki kusikiliza kwa sababu zifuatazo.
1. Ikiwa miundo mbinu ni mibovu, je kipindi cha JPm uchakavu huu ulikuwa na Utii?
(i) Yaani nguvu haikuanguka kwa kuwa JPM aliilazisha isianguke, je waya haukukatika kwa kuwa rais amesema? Je vifaa kama transfoma, capacitors n.k zi a hofu na sauti ya rais?
(ii) Je mgawo waliotangaza na baadae kuondolewa kwa kauli ya rais, na baadaye kuja na ngojera nyingine kuwa makadirio yao hayakuwa na usahihi na pia kumbe ujazo wa maji ulikuwa unaongezaka ni kukiri kuwa hawana uoni wa kisayansi au ndio miundo mbinu kuwa na utii kauli za rais?
2. Huyu alipokuwa waziri wa mazingira alikuwa negativu na JNHP Project, je awezeje kutekereza kile alicho kinyume nacho?
(i) Kitendo cha kuja na hoja ya kuwa hakuna winchiya kubeba milango ina ukakasi maana haiwezekani mkandarasi hakujua kuwa moja ya vitendea kazi ni winchi hizo na kuwa hoja hiyo imewashtukiza. Hii ni ngojera yenye mashairi yasio na mizania ya vina. Haimbiki kirahisi.
(ii) Hii habari ya kuulizwa bungeni na kudifendi hoja kwa kusema kama wana haja na uwaziri na kumuingiza rais kama kinga ni mbinu chafu ya kutojibu swali na kujaribu kumuingiza rais katika utendaji wake dhaifu na kufanya watu waamini kuwa kusuasua kwa mradi una baraka za nyumba nyeupe. Jambo ambalo linaweza kuwa si kweli.
(iii) Kukimbilia kuona bora kuingia mikataba na makampuni ili yazalishe umeme inamaanisha hakuna seriousness ya JNHP kukamilika upesi. Inaleta kijana kutoamika kabisa na uwaziri wake japo anau difendi kwa vitisho bungeni lkn yeye ndio sio smart.

Simusikilizi kwa kuwa ameingia na failed to accomplish atitude na kubeza waliomtangulia, na kusema mradi ulikuwa nyuma kuliko ripoti zilizokuwepo. Je mfano wakipewa nafasi ya kum challenge hoja zake itakuwa ni serkali ya aina gani? Sema ni wastaarabu wako kimya au wana hofu na mfumo uliomuweka madarakani.
Kama huyu bado waziri wa hii sekta tutegemee next episode ya mifuko ya hela.
Well said mkuu Omulasil
Big up kwa kusema Ukweli.
 
Januari ni clown he ain't a leader yuko hapo sababu ua legacy ya babake .

Hana chochote cha kutu proove kwamba he can stand on his own feet and he deserves it!!

He ain't visionary not smart as u think!!

Huku tunakokwenda Dr kalemani ataonekana ana uafadhali kidogo japo kuwa alikua na ushamba wa kisukuma
Ushamba ni nini
 
Sijawahi kuona kiongozi kilaza Tanzania kama huyu kijana
 
Mimi mwana if mwenzenu, nimefanya mahojiano na Waziri JM na hizi hoja, amezijibu vizuri kwenye mahojiano yangu msikilize hapa kuhusu JNHPP

Pia Waziri JM, amezungumzia issues mbalimbali za Nishati ya umeme, gesi, umeme jua, mkaa, kuni etc
P

Mkuu Pascal hapa sijaona alipojibu hoja za Bwawa kukamilika zaidi ya kuchepusha topic kwenda kwenye njia za usambazaji za dollar 800

Tusaidie hapo... na je kwenye mkataba hakukuwa na ujenzi wa distribution lines Au Tanesco hawakua na huo mpango kabla ya waziri huyu ?

Tumeona kwenye SGR Tanesco wakienda sambamba Na mkandarasi kwa kujenga mifumo ya umeme Na usafirishaji wake Vipi kwenye bwawa linalowahusu wao 100% wasahau hili ? 😰😂
 
Huyu jamaa anazidi kuonyesha jinsi anavyopwaya kwenye uongozi.

Ujenzi wa bwawa na vitengo vyake vyote, ukamilishwaji wake hatua kwa hatua, viliishaelezwa vizuri tu na mzalendo mmoja huko TBC.

Paschal naona umemtafuta/amekutafuta kwa lengo la kujisafisha.... Kimsingi hakuna alichosema cha maana zaidi ya kuuza sura.
 
Hii ni aibu kubwa sana badala ya kudili na taifa letu kuwa na uzalishaji mwingi na wa uhakika ili umeme ushuke bei na sekta binafsi iweze kukua kwa uzalishaji kuongezeka. Waziri wa nishati anawakatisha tamaa sekta binafsi na kutamka bila aibu mgao utakuwepo .

Kama njia za kusafirisha umeme zimechakaa mbona wakati huyu waziri hajateuliwa hatukusikia habari ya mgao sababu njia za kusafirisha umeme zimechakaa?

Kama njia zimechakaa kwa nini zisifanyiwe ukarabati bila kuwepo mgao unaothiri uzalishaji mali?

Kwanini hatusikii huyu waziri akisisitiza JNHP kukamilika june 2022 kwa manufaa ya umma?
Kwa viongozi vilaza kama hawa tusitegemee maajabu. Kufanya kitu kile kile huku ukitegemea matokeo tofauti ni insanity.
 
Mmliki wa bwawa ni Tanesco ndio mwenye wataalamu wa Nishati,kwanini tusimuulize anaweza akawa na majibu ya uhakika.

Pili yupo mkandarasi Arab Contractor ndie mjenzi mkuu wa mradi , pia kuna project consultant nao wanaweza wakatoa majibu.

Mwisho malipo ya mradi yakoje,isije ukakuta kuna ukata.Tumeaona mradi wa SGR Dar-Moro licha ya serikali kujitutumua ilishindwa kabisa kuikamilisha na kuanza kutumika miaka 5 ya Mjomba Magu na sasa zaidi ya mwaka ya SSH.

Kumekosekana tranparency kwa miradi yote miwili.Utafikiri hawakuwa na plan.
 
Hii ni aibu kubwa sana badala ya kudili na taifa letu kuwa na uzalishaji mwingi na wa uhakika ili umeme ushuke bei na sekta binafsi iweze kukua kwa uzalishaji kuongezeka. Waziri wa nishati anawakatisha tamaa sekta binafsi na kutamka bila aibu mgao utakuwepo .

Kama njia za kusafirisha umeme zimechakaa mbona wakati huyu waziri hajateuliwa hatukusikia habari ya mgao sababu njia za kusafirisha umeme zimechakaa?

Kama njia zimechakaa kwa nini zisifanyiwe ukarabati bila kuwepo mgao unaothiri uzalishaji mali?

Kwanini hatusikii huyu waziri akisisitiza JNHP kukamilika june 2022 kwa manufaa ya umma?
Mwenzako RPC wa Kagera aliomba Rais amteue kuwa IGP na wewe omba uteuliwe kuwa Waziri wa Nishati ila kwa sharti moja tuu la kuhakikisha umeme haukatiki..

Failure to do that utawajibishwa sio kwa kutenguliwa bali na Kwa kulitapeli Taifa kwamba unaweza kudhibiti kukatika kwa umeme..

Maana ujinga umewazidi Sana nyie kenge hata mkiambiwa ukweli huwa hamtaki.

Waziri amesema kuna tathmnini upya inafanywa Kati ya Tanesco,Wizara na Mkandarasi Ili wakubaliane tarehe mpya ya kukabidhiana mradi baada ya June 22 kutowezekana kutokana na sababu alizozieleza hapo awali.
 
@PascalMayalla!

Ujuwe wewe humu unaheshimika sana kama senior member

Lakini usije ukawa unatetea vitu ambavyo jamii kwa upana wake inaona haviko sawa.
Hiyo clip anachoongea Makamba ni upuuzi mtupu.

Ngoja niulize.....

Anapoongea kwa kusema eti wao wameona mbele zaidi kwa kusaini mkataba mpya wa ujenzi wa njia za usambazaji umeme (Distributions)kutoka bwawani kuingia kwenye gridi ya Taifa.

:Badala ya kukalia tu kwenye ujenzi wa bwawa lenyewe"
Anamaanisha nini?

Anataka kutuaminisha watanzania kwamba

Serikali ya awamu ya Tano ilisaini mkataba wa ujenzi wa Bwawa bila kuwa na mpango wa connection ya usambazaji (distribution)?

Hilo lisingewezekana,maana hata Masanja Kadogosa wa SGR kila siku anapoelezea maendeleo ya mradi wake.

Pia huongelea ujenzi wa vituo vya kupokelea umeme kutoka Bwawa la Nyerere.

Labda Makamba anachofanya hapo ni yaleyale ya kusaini mikataba mipya ili kuweka 10% yake?

Kama tunavyomuona akifanya tangu ameshika wizara hii.

Mbona kwenye hiyo clip haongelei rasmi ni nini kinaendelea na kimefikia wapi kwa sasa?

Huyu ni waziri mpigaji hata Body language yake inaonyesha jinsi anavyotafuta cha kuongea ili kisitibue mpango wake.

mayalla unaheshimika ila angalia usitetee wataokuja kuchafuka na hivyo mkachafuka woote pamoja.

Ahsante.
Wewe kwa akili yako mbovu Waziri anaweza kujipigia pesa bila Serikali/Baraza la mawaziri kufahamu?

Ndio hivyo sasa mkataba wa awali haukuwa na hicho kipengele sasa unaposema haiwezekani tupe wewe mkataba wenu wa awali tujiridhishe.

Kwani Wewe unaniamini Sana Serikali ya awamu ya 5 au ndio unataka kutuaminisha kwamba ile serikali haikuwa ya wapigaji wa 10%?
 
Narudia. Kwenye swala la nishati ya taifa yeyote anaye hujumu kwa namna yoyote huyo ni adui namba moja. Kwa hili Akumbukwe Magufuli. Nitasimama na msimamo huo milele na milele.
Unamfahamu yeyote aliyekuwa anahujumu?

Mhujumu wa kwanza na Magufuli kwa kuchukua pesa za Tanesco na kuleta Mkandarasi asiye na uwezo wala mtaji.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom