Ni ahadi zipi zilitolewa na kiongozi wako ambazo hazijatekelezwa mpaka sasa?

JF Toons

Digital Art by JF
Feb 19, 2024
32
66
IMG_1609 (1).PNG

Si vyema kuweka ahadi ambazo unajua huwezi kuzitimiza au zisizotekelezeka.

Baadhi ya watu hupatwa na msongo wa mawazo na kupoteza uaminifu kwa kushindwa kutimiza ahadi.

Uwekapo ahadi hugeuka deni, na usiku wa deni haukawii kukucha.

Je, ni ahadi zipi ziliwekwa na kiongozi wako ambazo hazijatekelezwa mpaka sasa?
 
Ahadi ya Noah kwa Kila mtanzania
Ahadi ya kuuwa upinzani kabla ya 2020.
 
Ahadi ya kusambaza umeme kila kijiji jimboni ila ilishindwa kutekelezeka ikiwa mbunge wetu alipewa dhamana ya kuwa waziri wa nishati na madini kwa muda wa miaka isiyopungua 4 hii inawaumiza sana wananchi na hawamuamini tena huyu jamaa kama ni kiongozi bora
 
Hata nyie wapiga kura em tumieni akili bc, haiwezekani tokea 1995 mpaka sasa ahadi ziwe zilezile za kuboresha maisha ya watu
 
Kwa sasa watanzania tunatakiwa kupima sana kauli za wagombea wetu, tusiwape dhamana wagombea watakao onesha kutoa ahadi ambazo uhalisia wa utekelezaji wake ni mgumu sana gombea wa namna hii maranyingi wanakuja na sera kwaajili tu ya kuwateka wananchi ili wapate kura na wengi wao hutumia sana hata njia zisizo halali kama vile rushwa kwa wapiga kura. Hivyo tujiahadhari sana na wagombea wa namna hii.
 
Mwenyekiti wetu alituahidi 2023 ndiyo mwisho wake, jamaa kauchuna mpaka sasa March 2024 hakuna hata dalili za kuachia ngazi.
Watu tumepiga jalamba za kuwania uenyekiti mpaka tumechoka.
 
Back
Top Bottom