NHIF: Tutaanza kutambua Wanachama wetu kwa Kitambulisho cha NIDA

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umebainisha kuwa umeanza utaratibu wa utambuzi wa wanachama wake kwa alama za vidole kupitia usajili wao wa kitambulisho cha Taifa (NIDA).

Kauli hiyo imetolewa wakati wa kujibu hoja ya Mdau wa JamiiForums aliyedai baadhi ya Wafanyakazi wa NHIF waliopo Hospitalini hukataa kutoa Huduma mpaka Wazazi wabadilishe Kadi za Watoto wakidai Picha zilizopo kwenye Kadi hazifanani na Watoto kutokana na kubadilika (Watoto kukua).

NHIF imeongeza kuwa “Utaratibu wa utambuzi kwa njia ya sura umeshaanza kufanyika ambapo umuhimu wa kuwa na sura halisia ya wakati husika ya Mwanachama ni hitaji muhimu. Hivyo unahimizwa kuhuisha picha ili kuepuka usumbufu wakati wa utambuzi vituoni.”

Hoja ya Mdau: NHIF watumie mfumo wa fingerprint scanner kutambua wanufaika/ watoto badala ya kusumbua wazazi
 
Back
Top Bottom