DOKEZO Tabia ya NHIF Tabora kuchelewesha kadi za Bima za Uanachama inatuumiza wengi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa Mkoa wa Tabora, Wilaya ya Kaliua, kero yetu huku ni kuhusu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuchelewa kutoa kadi za Uanachama baada ya kutuma maombi.

Inauma na inakera kwani huchukua mpaka miezi 6 unapoomba uanachama ndiyo unapewa kadi huku makato yakiwa yanaendelea hasa kwa sisi Watumishi wa Serikali.

Hii imesababisha kupata changamoto na usumbufu wa kimatibabu na husababisha kukosa huduma ya matibabu pindi unapougua.


Pia soma:

1. Nimelipia Bima ya Afya NHIF Mwanza, nazungushwa kupata kadi. Kibali cha matibabu pia hawanipi

2. NHIF: Mfumo wa uwasilishaji wa kadi kwa watumishi kupitia halmashauri ni changamoto (JIBU)
 
Wasumbufu sana,wanapiga tu story hapo gorofani,kina Mzirai hawajali wateja
 
Kwanini wasiwe wanatoa namba harafu kadi ndo inafuata kama wanavyofanya NIDA?
Mteja awe anatumiwa namba yake (Codes) ambayo anaweza kwenda nayo hospital Kwa ajili ya kupatiwa matibabu kadi ifuate baadae.
 
Back
Top Bottom