NHC yambwaga Mbowe Mahakamani

NHC yambwaga Mbowe Mahakamani

QUOTE="Ntandaba, post: 18105532, member: 312276"]Mleta mada mbona unaharaka sana?hebu ivisha kwanza hii habari kwa maana sijaona maneno kama "kwa mujibu wa kifungu namba...,neno katiba nk[/QUOTE]

Sikiliza cue ya kibatala iyo video utapata ivo vifungu
 
Safi sanaaaaaa Mbowe alipe deni aache usanii, huu ni wakati wa kazi tu, hongera mahakama kutenda haki.
 
Uzi wote umejaa Lizaboni na mhaya mmoja nshomile rutashobolwa
 
Hii inasikitisha sana kwa siasa zetu pamoja na sura halisi ya viongozi wetu
kitaifa. Je Mbowe ni kama Trump kukwepa kodi tangu miaka ya 90?

-------------
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameangukia pua mahakamani baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kutupilia mbali maombi yake katika mgogoro wake wa umiliki wa jengo la Shirika la Nyumba (NHC).

Mbowe alifungua maombi mahakamani hapo kupitia kampuni yake ya Mbowe Hotels Ltd, akipinga uamuzi wa NHC kumuondoa katika jengo ambalo alikuwa akilitumia kama ofisi ya kampuni yake ya Magazeti ya Free Media na klabu ya Bilicanas.

Katika maombi hayo, pamoja na mambo mengine Mbowe alikuwa akidai kuwa aliondolewa katika jengo hilo jinyume cha sheria kwa kuwa hakupewa taarifa na kwamba kampuni ya udalali iliyotumiwa kumuondoa haijasajiliwa kama dalali wa mahakama.

Hata hivyo katika uamuzi wa mahakama hiyo uliotolewa leo na Jaji Sivangilwa Mwangesi, imetupilia mbali maombi hayo ya Mbowe ikisema kuwa hayana msingi

Jaji Mwangesi alikubaliana na hoja za NHC na akasema kuwa Mbowe aliondolewa katika jengo hilo kisheria.


Chanzo: Mwananchi

Hilo pingamizi halikuwa na mashiko!! Mwanasheria gani huyo kwenda kusema kwamba points za pingamizi ni kutopewa taarifa na kwamba dalali hakuwa na usajili!! Hizo tu basi!!
 
Hata hapo chamani anawapiga sana tu sema analundo la running dogs ambao kawajaza ujinga kwamba yeye ndiye anakifadhili chama.

Chacha Wangwe pamoja na kuwa na elimu ya kawaida tu aliukataa huo ujinga lakini leo hii pana wasomi pale mpaka maprofesa lakini wamegeuka Yes-men kazi kufuga ndevu tu.

They can't even question!!

Running dogs like father and mother as running dogs of lumumba
 
Kwan advocate wake hakuwa yule wa kule mijo ya katkat ya nchi sijui anaitwa nani? Si wanasema huwa hashindwi kesi advocate wao?
 
Hii ni dalili mbaya kwa Seif vs Lipumba.

Ila kwa nini wafuasi wake wasiendeshe harambe ya kuchangia deni la boss wao. Ninauhakika watakusanya pesa nyingi kuliko za tetemeko la Kgera na Mangi Mbowe hatawasahau aisee
 
Mbowe kama bado una amini haki haijatendeka,kata rufaa.
Salary Slip siku hizi unajitambua. Njia pekee iliyobaki ni kukata rufaa na wala si kupambana facebook ama JF.

Ila mkuu nimesikia wanasema mkataba haujawahi kutekelezwa hivyo mkataba ulivunjika!! Tusubiri legal reasoning ya Majaji wa Rufaa.
 
You raise a really good point.
Ila hii kesi nayo unless there is something am missing, kuna kitu kama hakiko sawa. Si ni hii mahakama ilikataa kumtambua dalali aliyetoa vitu vya mbowe nje... Which in essence means taratibu hazikufuatwa kwasababu NHC walitumia dalali ambaye hajasajiliwa/hatambuliki na mahakama.

Huyu Jaji sijui jina hata Arusha alifanya vya kwake
Video for sivangi wa mwenge, high court tanzania
[emoji666] 1:51
 
Kwa majigambo yaliyotolewa majukwaani siku chache baada ya Mbowe kutolewa vyombo vyake...
Ningeshangaa sana kama ingekuwa tofauti na hivi.
Safari bado ni ndefu.
Alienda mahakamani kufanya nini kama tayari alijua maamuzi yatakuwa haya?
 
Kuna shida gani Mbowe kulipa pango NHC, Mbowe watu wengi wametimuliwa hakuna aliyehusisha kutimuliwa kwao na maswala ya kisiasa?? Mbona kutimuliwa kwa Mbowe kumehusishwa na siasa???
Kamanda Mbowe lipa deni ili tuondoe utata wa kutimuliwa kwako toka kwenye nyumba ya NHC na maswala ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom