Lissu aonekana Mahakamani leo

Lissu aonekana Mahakamani leo

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,165
Reaction score
60,513
Kutoka kwenye akaunti ya X ya Hilda Newton, anaripoti kuonekana kwa Lissu mahakamani leo asubuhi bila chama au mawakili wake kupewa taarifa.

IMG_20260430_105258.jpg


UPDATES:

Brenda Rupia: Ni kweli kuwa, Mwenyekiti alifikishwa mahakamani kusomewa uamuzi mdogo kufuatia Maombi yake ya kuunganishwa kwenye kesi ya said Issa Mohamed na wenzake wawili dhidi ya Bodi ya wadhamini na Katibu Mkuu wa Chama.

Katika uamuzi wake, Mahakama kuu imekataa Maombi ya Mhe Lissu kuunganishwa kwenye kesi hiyo.
 
Hata kama anajiwakilisha bado yeye ni Mkiti wa chama lazima chama kipewe taarifa.
Kisheria siyo lazima. Hakushitakiwa kama Mwenyekiti wa CHADEMA Bali kama Tundu Lissu.

Naelewa unachomaanisha lakini na hao waliomshitaki wametumia mwanya wa kisheria kufanya walichofanya.

Labda wanamsomea mashitaka mapya yanayotokana na maelezo ya Tume ya Jaji Chande ama pia DPP ameleta "Nole Prosequi" ili afute mashitaka.
 
JE, MAMLAKA IMEPANGA KUMUACHIA LISSU KWA SIRI KUPITIA MAHAKAMA LEO?

Kuna taarifa zinaenea mtandaoni kuwa Mhe. Tundu Lissu amepelekwa mahakamani kimya kimya asubuhi hii. Kama taarifa hizi ni za kweli tutasubiri kupata ufafanuzi kutoka kwa Wakuu wa Magereza ni kwa nini wamefanya hivyo!

Lakini kwa nini Lissu apelekwe ghafla na kimya kimya mahakamani muda mfupi baada ya ntiiti ya Seneti ya Marekani kusambaa mitandaoni. Je, mamlaka imeamua kumuachia Lissu kimya kimya baada ya kumkamata kwa mbwembwe nyingi sana.

Pengine ni busasa kwa wafuasi wa CHADEMA walioko Kigamboni, Magomeni, Ubungo, Ilala, Kariakoo, Buguruni, nk wawahi haraka wafike mahakamani kwani ni haki yao kujua hatima ya kiongozi wao.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Cc: Boniface Anyisile Mwabukusi Paul Kisabo Azaveli Lwaitama John Heche

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 30 Aprili 2026; Saa 4:50 asubuhi
1777539102653.jpg
 
Back
Top Bottom