hashim mwamba
JF-Expert Member
- Sep 2, 2016
- 1,018
- 1,105
Wanatafakari bdae wataleta mrejesho
Leo mawakili nguli kuliko wote tanzania wameangukia pua... hakika lazima judge alipokea simu kutoka ikuluPro-Chadema JF utasikia wanasema Mahakama aitendi haki baada ya kesi ya Mbowe kutupiliwa mbali.
Hamna namna Mbowe alipe deni.
Dawa ya deni ni kulipa mkuu sio hasira.....lazima tutambue ruzuku ndio itatumika kulipa deni ujenzi wa makao makuu kwisha tena.Ulivyo na akili ndogo hukawii kudai hadi mama yako mbowe alimrithi ndio mkapatikana nyie na wadogo zako!
Hahahahaha aiseee kwa hiyo kuna simu ilitoka ikulu? aisee makamanda mnajua kunikosha.Kwa majigambo yaliyotolewa majukwaani siku chache baada ya Mbowe kutolewa vyombo vyake...
Ningeshangaa sana kama ingekuwa tofauti na hivi.
Safari bado ni ndefu.
Makamanda wana andaa tamko lazima waseme wamefatilia mawasiliano ya judge na wamegundua alipigiwa simu kutoka ikulu TEH TEHMahakama imetenda haki kwa sisi wananchi dhidi ya wezi wa mali za umma.Hakika tumefurahia sasa shirika letu NHC litapumua baada ya kunyonywa na wadhalimu.
Huyo hakimu alijuaje kama mkataba haukutekelezwa (maana hajasikiliza hoja za upande wowote juu ya hilo)MAHAKAMA YAITUPILIA MBALI KESI YA MBOWE HOTELS DHIDI YA SHIRIKA NA NYUMBA LA TAIFA (NHC)
![]()
Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi imefuta kesi iliyofunguliwa na Mbowe Hotels Ltd. dhidi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuwa Shirika hilo liliitoa kampuni hiyo katika jengo lake jijini Dar es salaam kwa kufuata taratibu zote na kuzishikilia mali zake kihalali.
Uamuzi huo umetolewa asubuhi hii na Jaji Sivangilwa Mwangesi, ambaye amesema madai ya Mbowe kwamba aliingia mkataba na NHC hayana mashiko na kwamba mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.
Mawakili wa Mbowe Hotels Mhe. John Mallya na Mhe. Peter Kibatala (pichani ) wakiongea na waandishi wa habari mara tu baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu kutoka, wakidai kwamba hawakuridhika na uamuzi wa kufutiliwa mbali kwa kesi ya mteja wao.
Ha ha ha, sijamaanisha hivyo kamanda.unafikiri kila uzi lazima watu wachangie?
Kuna mambo mengine ni kujishushia heshima tu wala aina maana...kweli kabisa kamanda
Wanajifanya wema mbele za watu kumbe majizi yaliyokubuhu!Wajifunze kulipa kodi, mwanasiasa mzima huwezi kutumia vitu vya umma bure. Shame on you.
Yeah right. Kesi nyingi sana wapinzani wanashinda mahakamani. Tundu Lissu ameshaigaragaza serikali mara ngapi? Ikitokea wakashindwa hata kama siyo masuala ya kisiasa basi maneno kibao na kujiapiza kusiko na misingi. Tukumbuke tu kuwa nobody is above the law; na hata ukijifanya leo kuwa uko above the law kesho na kesho kutwa the law will find you. ...Boss alisha-shabikia jamaa kutolewa pale xo haishangazi kwa maamuzi yaliyofikiwa leo.
Mbegu inayopandwa sasa ikikomaa, tuwe tayari kwa mavuno.