Nguvu ya Rais Magufuli sasa inajulikana ilipo. Ni hatari kwa uchumi wetu

Hivi operesheni ya Jesh ya kuendesha biashara ya korosho iliishia wapi ๐Ÿ˜ƒ ๐Ÿ˜ƒ ๐Ÿ˜ƒ ๐Ÿ˜ƒ ๐Ÿ˜ƒ viwanda vya kijeshi vya kubangua korosho!

Inashangaza Sana Mambo yanaharibika Wazee wameufyata. Hata Taasisi ya Mwalimu Nyerere siku hizi ni inazidiwa hata na Mke wa Godbless Lema, hakika hizi Zama Ni Zama!
Huu upuuzi wanajifanya wameusahau.
 
Hata mke wa lutu aligeuka jiwe Kwa kuanza kumbuka ushenzi uliokuwa ukifanyika Gomola na Sodoma,

Ni Yule Yule mke wa lutu aliyekuwa akilalamikia biashara ya ukahaba kuchukuliwa na wanaume na wanawake wakikosa soko

Wake za lutu ni vigumu kuisha duniani kumbe??
Kwa zuri lipi lililopo leo ndugu yangu ?!.
Angalia kichowakuta wafugaji, wavuvi, wafanya biashara, utumbuzi usio wa haki wa watumishi, miaka 5 hakuna ajira nk nk . Uchumi utakuwaJe bora ?!.

Uongozi wa awamu ya nne ulikuwa na mapungufu tena makubwa tu, hasa kwenye mikataba. Lakini angalau uchumi wa watu ulikuwa stable.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, Kwanza nakupongeza Kwa kujikita kuzungumzia mapungufu mengi yaliyopo sasa na hata Mimi naungana na wewe katika hayo ingawa si yote

Binafsi siungi mkono unafki mkubwa uliokubuhu Kwa wengi wetu hapa, hasa mtu anapokumbuka ya utawala uliokuwepo kabla ya huu,

Mkuu, mtu anapojaribu kukumbuka nyuma maana yake inabidi atueleze pia yoote tuliyokuwa tukishinda hapa kuyaponda, Mkwere alidharilika Sana hapa na waliomdharilisha ni haohao ambao leo wanasema wamekumbuka Uongozi wake,

Na ndiyo maana nilihitimisha kusema, wake za lutu ni wengi na hawatakaa waishe

Je kipindi cha JK wanakumbuka pia kwamba Maskini wengi waliswekwa ndani Kwa makosa yasiyo Yao, Maskini wengi walikuwa wakinyang'anywa mashamba na viwanja na matajiri, tena usinikumbushe kabisa kuna ndugu yangu alinunua kiwanja alikuwa akikiendeleza kidogokidogo siku ya siku alikuta kiwanja kile kimepigwa fensi kwenda mahakani akafungwa yeye,

Wanakumbuka pia kwamba member wa hapa bwana BAK karibu Kila siku alikuwa analeta liwaya jinsi serikali ya kipindi hicho ilivyokuwa imeoza

Staki kukumbuka uozo wa nyuma, Tusemeni na tukaze kukemea uozo uliopo leo
 
Mi nasikitika na Korosho aisee hasara kubwa sana na sasa wapo kimya hakuna anayezungumzia.
Ngoja waje wale waliopangwa zamu ya leo waje wakanushe kila kitu ulichokisema. Lakini waswahili wana msemo wao, mficha maradhi kifo humuumbua.

Kama kwenye viwanda tumerudi nyuma, kama kwenye kilimo cha mazao hasa ya biashara hatufanyi vizuri kuanzia uzalishaji, kuchakata na hata kuuza nje, kama uvuvi umeathirika na viwanda vya uchakataji samaki vimefungwa na orodha ni ndefu ni nini sasa kinaendelea kwenye uchumi wetu!!!?

Zisipochukuliwa hatua za haraka na za makusudi kabisa kuokoa hali, basi ni suala la muda tu tutakua na crisis ya kiuchumi. Biashara za ndani nazo bado hazijarudia hali yake ya miaka mitano iliyopita. Hata miundombinu inayojengwa kama kutakua hakuna marekebisho muhimu ya sera, sheria na nia ya dhati bado mchango wake hautaonekana sana kwenye uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Busara zilikuwa ziaze ktk kufufua mazo ya biashara kwanza ili kuvutia uwekezaji ktk viwanda, Pia tuanze kufufua viwanda vyote alivyoanzisha Mwalimu. Badala yake tukaanza mkakati wa kujenga viwanda vipya bila dira ya aina yoyote! Tumeishia kuhesabu vyerehani na machine za kufyatulia matofali kama viwanda! Shame!

Mkuu zaidi ya nusu ya viwanda alivyoacha mwalimu ni vya technology ya kizanani. Kusema vifufuliwe ni sawa na kukutana na mtu anataka kufufua Leyland Albion likabebe mizigo kwenda DRC. Kinachoweza kutumika kwenye hivyo viwanda ni majengo tu boss.
 
Tatizo la hii nchi hatuna mipango endelevu

Ccm ndio wanaongoza hi nchi tatizo ni kwamba hawana ilani ya miaka 50 au miaka 100 ilani yao ni miaka 5 au 10 hapo ndipo kwenye shida

Kwa mfano Kikwete alikuwa na Sera ya kilimo kwanza na alianza kujenga miundombinu ya hicho kilimo kwanza kama

Banki za wakulima ili wakulima wakope

Kuleta zana za kilimo kama matrekta kupitia suma jkt

Kujenga mabwawa ya umwagiliaji

Wataalamu wa utafiti ili kufufua kilimo cha mazao ya biashara kama mkonge, pamba ,kahawa ,korosho, karafuu ,alizeti na mawese

Lakini cha kushangaza alipoingia muheshimiwa Magu wala hakuyaangalia hayo mambo ya kilimo kwanza badala yake na yeye akanzisha Sera yake mpya ya viwanda

Sijui kama Magu atafanikiwa katika hili la viwanda au la

Na amini usiamini atakapo ondoka Magu akija Raisi mwingine utashangaa na yeye anaanzisha Sera mpya anaweza akarudi katika Sera ya kilimo kwanza sasa nchi haiwezi kuendelea kwa mtindi kama huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, Kwanza nakupongeza Kwa kujikita kuzungumzia mapungufu mengi yaliyopo sasa na hata Mimi naungana na wewe katika hayo ingawa si yote

Binafsi siungi mkono unafki mkubwa uliokubuhu Kwa wengi wetu hapa, hasa mtu anapokumbuka ya utawala uliokuwepo kabla ya huu,

Mkuu, mtu anapojaribu kukumbuka nyuma maana yake inabidi atueleze pia yoote tuliyokuwa tukishinda hapa kuyaponda, Mkwere alidharilika Sana hapa na waliomdharilisha ni haohao ambao leo wanasema wamekumbuka Uongozi wake,

Na ndiyo maana nilihitimisha kusema, wake za lutu ni wengi na hawatakaa waishe

Je kipindi cha JK wanakumbuka pia kwamba Maskini wengi waliswekwa ndani Kwa makosa yasiyo Yao, Maskini wengi walikuwa wakinyang'anywa mashamba na viwanja na matajiri, tena usinikumbushe kabisa kuna ndugu yangu alinunua kiwanja alikuwa akikiendeleza kidogokidogo siku ya siku alikuta kiwanja kile kimepigwa fensi kwenda mahakani akafungwa yeye,

Wanakumbuka pia kwamba member wa hapa bwana BAK karibu Kila siku alikuwa analeta liwaya jinsi serikali ya kipindi hicho ilivyokuwa imeoza

Staki kukumbuka uozo wa nyuma, Tusemeni na tukaze kukemea uozo uliopo leo
Ila hakuingilia privet sector kama wakulima wa korosho
 
Inashangaza sana kuwa haya yanatendeka ,walio takiwa kukosoa wanashambuliwa! Hivi kina Mzee Butiku na wenzake wanajisikiaje namna walivomkomlia kumkosoa JK na BWM ,Leo hali ni mbaya wamekaa kimya utawala bora uanabakwa!
Butiku ni homeboy anangoja tu nafasi ipatikane apate uteuzi uzeeni.
 
Kalamu1,

Mwimbaji wa mapambio ya Viwanda Charles Mwijage si tayari alishushwa njiani katika ile safari yenu ambayo Dereva wetu alituambiwa tuwe watulivu maana yeye ndio anayejua anapotupeleka.
Duh! Nimecheka sana....anajua anakotupeleka, halafu tunakubari kupelekwa tusikokujua. Hatari sana
 
Nakumbuka zile mbwembwe nyingi za kufungua viwanda karibu kila wiki kwa wakati fulani mwanzoni mwa awamu yake. Viwanda vingi alivyovifungua, vyote vilikuwa ni juhudi za Rais Kikwete.

Siku hizi hata kusikia tu lile neno la viwanda ni nadra kabisa, na baadhi yetu hatujui kama wizara hiyo bado ipo au ilifutwa, maanake hata waziri mwenyewe hajulikani kama yupo au hayupo.

Zao la pamba, wakati wa Kikwete, lilikuwa limewekewa nguvu sana kiasi kwamba maeneo yote panapolimwa zao hilo palianza kuonekana kuwa shughuli ya kulifufua zao inafanyika. Simiyu ilianza kuonekana kama mkoa maalum wa kulima zao hili.

Juhudi za kulifufua zao hilo, ulikuwa ni mkakati wa kufufua viwanda vya nguo, ili pamba tunayozalisha isindikwe hapa hapa kwetu, na kulisha viwanda hivyo. Hali hii ilitia matumaini makubwa.

Sasa sikumbuki ni lini nimesikia habari zinazohusiana na mikakati hiyo, badala yake, inaelekea hata hiyo pamba kidogo itakayoendelea kuzalishwa, tegemeo letu ni kuwauzia wenye viwanda nchi jirani yetu hasa pale Kaskazini.

Hili litakuwa ni jambo la kusikitisha sana, kwa sababu tunapoteza fursa za waTanzania katika mnyororo mzima wa zao hili muhimu.

Na kwa uhakika, wenzetu hawa wamepania hasa na mikakati yao ya kushika soko zima la ukanda huu katika swala la nguo. Wamefufua viwanda vyao, na hata zao la pamba wakaamua kulima lile la aina mpya, lisiloshambuliwa na wadudu (genetically modified), bila shaka lengo lao likiwa kujitosheleza zaidi kwenye viwanda vyao.

Hata mitumba wameamua kuipiga marufuku, ingawa ndio waliotulazimisha tusalimu amri tulipotishiwa AGOA. Ni wajanja sana hawa watu!

Hili ni eneo moja tu la viwanda, ambalo limemshinda wazi wazi Rais Magufuli kulitilia mkazo unaostahili. Miaka mitano yake yote, mbali ya kuimba kwa nguvu sana hapo mwanzo kuhusu umhimu wa viwanda, mwisho wake, kama ni alama, anastahili F kubwa kabisa.

Rais Magufuli hatatuvusha kabisaa, katika maswala ya viwanda. Labda tutegemee hayo mengine, kama ya Miundombinu, sio viwanda.

Najua kuna maeneo mengine mengi yaliyomshinda, lakini hili la viwanda lipo dhahiri.

Hahahaha, yaani chuki imekujaa, kiasi hata ulichotaka kukieleza kimepotea. Pole sana, unajitesa bure kwa kuutamani uongo unaouamini utokee
 
Ngoma ya kitoto haikeshi mkuu. Mwijage sijui yuko wapi maana yeye angalau alikuwa ana guts za kutamka maana ya neno viwanda bila kupepesa macho

Mwijage mwenyewe Mambo yslimshinda...! Kuna siku Mhe. Heche alimbana Mwijage Bungeni kuwa AMESHINDWA KUJENGA VIWANDA na Heche akamwambia Mwijage kuwa ANATEMBEA AMEWEKA MIKONO MFUKONI ATI AKIKUTANA na Waheshimiwa Wabunge alikuwa akiwauliza," Je, unataka kiwanda jimboni kwako kana kwamba anagawa toka Mifukoni mwake..," Kazi kwelikweli!
 
Hahahaha, yaani chuki imekujaa, kiasi hata ulichotaka kukieleza kimepotea. Pole sana, unajitesa bure kwa kuutamani uongo unaouamini utokee
Huu ndio ushamba wa watu kama wewe.

Hapo chuki ipo wapi. Umeelewa nilichoandika mimi, mbona hukukijibu kwa hoja unazoona wewe ni sahihi.

Ulivyojitokeza hapa, hata Rais Magufuli mwenyewe akiona utetezi wako huu atakushangaa sana.
 
Back
Top Bottom