Nguvu ya mwenye pesa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nguvu ya mwenye pesa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Cynic, Apr 12, 2009.

 1. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Kuna haja gani ya kuingia gharama/cost kama hizi?
   
 2. G

  Giroy Member

  #2
  Apr 12, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya mambo kweli yanaonyesha nguvu ya pesa,mkuu wa nchi .waziri na mkuu wa mkoa hapo lazima mkuu wa wilaya na mbunge walikuwepo jumlisha ulinzi.siyo matumizi mazuri ya fedha za serikali.wakati awamu ya tatu mheshimiwa moja alikuwa arusha kufungua gift shop ya mfanyabiasha moja.unajua iliktwaje!walifunga barabara kama harusi za uswahilini ikawa gumzo mjini.Huu ni mmomonyoko wa maadili.labda pia kuna mgongano wa masilahi.ENZI ZA MWALIMU HAKUNA AMBAYE ANGETHUBUTU KUFANYA MAMBO KAMA HAYA YANAYOFANYIKA LEO.
   
 3. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Huyu ni mjasiriamali kamili ambaye anafanya matangazo ya hotel yake kupitia Mkulu. Si unajua mkulu anapokwenda kufungua mahala habari zake uwa zinatangazwa na vyombo vingi?? vile vile hapa ndio naye anajitambuliusha biashara kwa wakulu wengine waliokuwepo na JK.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi haya mambo ya rais kufungua hoteli za watu binafsi yameanzia wapi?
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Apr 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jasusi,
  Mkapa alifungua shamba la nani sijui kule Iringa tena kama sikosei alikuwa kiongozi mbona haikuwa deal..
  Viongozi ktk nchi za Kibapari wanafanya sana haya maadam mwaliko unatimiza masharti, marais wanakwenda maharusini na sii deal iwe kufungua Hotel..... sioni big deal hapa!
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,564
  Likes Received: 18,299
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu, hili ni jambo jema, Rais kufungua kitegauchumi kikubwa hivi pwani ya Bagamoyo ni jambo la kheri.

  Tufike mahali tujisikie proud wazawa sasa nao wanamiliki hoteli ya kiwango hicho. Ni hoteli chache sana pwani ya Bagamoyo zinamilikiwa na Wabongo.

  Labda kama angefungua moja ya Sheraton, Holiday Inn, Marriott Marquez or Inter Continental labda watu wasingeshaa, wangeona its ok rais kufungua, lakini ikiwa ni hoteli ya Mbongo, ni maneno!.

  JK amefanya jambo zuri katika promotion ya uwekezaji wa ndani, na sasa mahotelini humo, tukale wenyewe na kulala wenyewe, sio kungoja wazungu tuu.

  Pamoja na umasikini wa Watanzania, wengi wa wapiga kilaji wazuri, ni sisi wenyewe. Mtu anakunywa 20,000-50,000 kwa siku akiwa na marafiki na kimwana, ila kuitoa family yake kwenda kushinda beach, or eating out ni issue!.
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  juzi nimepita kwenye hiyo hoteli na kusema ukweli ni mbaya ajabu na yale mapaa yake ya blue ndio ovyo kabisaaaa

  Eneo la kiromo ni zuri sana la ile hoteli kuwa njiani ni safi sana lakini jamani that thing is tacky to the maximum na sidhani kama ilikuwa ni Good idea kumassociate mheshimiwa na kufungua something that tacky


  ile hoteli ni mbaya kuanzia design mpaka finished product...ni ni testament tosha kuwa pesa si kila kitu...nadhani hata vyumba vyake mmeviona kwenye TV na magazeti.


  Lakini tusisahau kuwa rais huyu huyu keshafungua appartment block lililokaa kama yale ma council tower blocks pale Edmonton,North London, na keshafungua hoteli kadhaa ambazo ni tacky to the max kama Kiromo view

  Having said that, si vibaya rais kufungua hoteli au biashara iliyojengwa na mzalendo...lakini kusema kuwa huyo mwenye Kiromo view ana pesa itakuwa ni overstatement kwani hoteli yenyewe inaonyesha wazi kuwa hakuna kitu pale
  sasa baada
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Kwa maoni yangu, hili ni jambo jema, Rais kufungua kitegauchumi kikubwa hivi pwani ya Bagamoyo ni jambo la kheri.

  Tufike mahali tujisikie proud wazawa sasa nao wanamiliki hoteli ya kiwango hicho. Ni hoteli chache sana pwani ya Bagamoyo zinamilikiwa na Wabongo.

  Labda kama angefungua moja ya Sheraton, Holiday Inn, Marriott Marquez or Inter Continental labda watu wasingeshaa, wangeona its ok rais kufungua, lakini ikiwa ni hoteli ya Mbongo, ni maneno!.

  JK amefanya jambo zuri katika promotion ya uwekezaji wa ndani, na sasa mahotelini humo, tukale wenyewe na kulala wenyewe, sio kungoja wazungu tuu.

  Pamoja na umasikini wa Watanzania, wengi wa wapiga kilaji wazuri, ni sisi wenyewe. Mtu anakunywa 20,000-50,000 kwa siku akiwa na marafiki na kimwana, ila kuitoa family yake kwenda kushinda beach, or eating out ni issue!.:"

  ***************************

  PASCO: Umeenda nje ya hoja. Mwanzilishi wa thread hakusema ni vibaya kwa JK kufungua hotel au kitega uchumi chochote, bali alikuwa analalmikia ile "cost" kwa umma katika ufunguzi huo. Settting ya tukio ilikuwa very elaborate.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,564
  Likes Received: 18,299
  Trophy Points: 280
  Asante nimeelewa, sorry.
   
 10. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,400
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Mkandara,
  Pamoja na yote tuwe na standards, tuone ile thamani ya RAIS au WAZIRI, kwa mfano Rais afungue investment ya USA Dollars 50million na zaidi; Mawaziri let say 10 million hadi 49million na zingine wapewe wabunge na wakuu wa mkoa.

  Ile hotel nimeiona, sijui niweke standard gani.
  Naamini kuwa ndiyo maana hata wageni wengi wakija hapa kwetu kufanya hata biashara ndog ndogo hutaka wamwone Waziri au Rais; we are too simple, we do not have that value!
   
 11. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Sawa. Ila wasaidizi wake wamsaidie asitumike na wajanja kutangaza biashara zao kwa gharama za awalipa kodi.
   
 12. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri ni big deal kiongozi yeyote (Mkapa au nani) anapotumika na wajanja kujitangaza au kutangaza biashara zao kwa gharama za awalipa kodi.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Apr 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Cynic,
  Ndio Ubepari huo mkuu wangu kwani kodi atakayo lipa huyo mwenye biashara na wafanyakazi wake si ndiyo unazungumzia kuwa kodi ya walipa kodi au yeye hayumo ktk hesabu hiyo..
   
 14. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Rais anatokea bagamoyo.. its his former constituency and tribal home.. hichi kihoteli kama kitatoa angalau ajira fulani to 15-30 people, basi angalau its something.. Kufungua sio tatizo..
   
 15. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Jasusi,

  Ujamaa aliokuachia Nyerere naona unakutafuna kwi kwi kwi!!!

  Kuna ubaya gani rais kufungua hoteli za watu binafsi? Biashara yoyote halali au mradi wowote halali ni kwa faida ya nchi nzima. Kuna Watanzania watapata ajira hapo, kuna kodi italipwa na faida zingine nyingi tu.

  Tusiwe anti biashara sana, kuna wafanyabiashara wengi ambao wana contribute sana kwenye maendeleo ya nchi yetu. Kuna wengi ambao hawafanyi chochote zaidi ya kutuibia. Pia kuna sisi ambao sio wafanyabiashara lakini tunaongoza kuifilisi nchi kwa utendaji mbovu na kuficha vijisenti nje.

  Mkapa kafungua biashara nyingi tu za watu binafsi. Hivyo hivyo Mwinyi na hata Nyerere na yeye ingawaje wakati huo hizo biashara zilikuwa chache sana.

  Hakuna tofauti kabisa kati biashara halali ya mtu binafsi na biashara inayoendeshwa na serikali. Malengo ya biashara zote ni yale yale ya wealth creation.

  Binafsi ningependa tupate Watanzania wengi kama Mengi kwa faida ya sisi wote.
   
 16. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ninavyojua ni kuwa mwenye hotel ndo anagharamia gharama za ikulu, nakumbuka kanisa likihaha wakati fulani ku-meet gharama za ziara ya rais kuhudhuria one of its jubilee anivessary
   
 17. T

  Tujisenti JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2009
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Labda ana shares humo kwenye hoteli sio vibaya kuipigia debe
   
 18. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni rais au ni Kikwete? na gharama za mlipa kodi zingetumika tu hata angekwenda kumsalimia mama pale bagamoyo, nadhani hiyo ndiyo gharama ya kuwa na viongozi lazima wananchi wawalipie.
   
Loading...