Hujui namna gn niliumia! Hujui namna gn kutokuwepo kwake kulinipoteza ktk dira sahihi ya maisha!
Kwa kifupi niliteseka, nilimature b4 my age!
Na hv hajishughulishi ku-apologize, ndio kbs!
Namtakia all the best ktk maisha yake!
SIJAMSAMEHE!
Msamehe tu kwa faida yako jamani. Kuwa na uchungu na kinyongo huwa kunaathiri akili, mwili na roho hivyo nikiskia kuna mtu hafanikiwi kwa sababu kambeba mtu sishangai sana ingawa kasi ya mafanikio inaweza kushangaza wengi. Niliwahi kuwa muathirika wa uchoyo wa msamaha baada ya kumbeba moyoni "mchumba" tuliyeachana baada ya "uchumba sugu" wa miaka 5. Kwa miaka miwili maisha yalisimama (waliowahi kukolea wakaachwa wanaweza kuelewa vizuri). Siku nilipoamua kumsamehe na kumuachia aisee sijui nguvu zilitoka wapi. Ndani ya miaka miwili nilifanya mambo makubwa sana kwangu mpaka nikajuta muda nilioupoteza kwenye kulia lia na kumuombea mtu mabaya wakati yeye analala fofofo.
Kisa kingine ni cha mimi baba yangu mzazi. Nilikuwa namchukia sana lakini nilikuwa nimefanikiwa kimaisha (digrii nyingi, kazi, mtoto na mali kadhaa na bado nina ari ya kuendelea kujiongeza) Huyu baba alinitelekeza nikiwa na mwaka mmoja. Sikuwahi kumuona na hata nilipojua aliko sikuwahi kufikiria kumfata. Sijui alipata wapi namba yangu ya simu nikiwa chuo kikuu akaanza kunipigia pigia na kugawa namba yangu kwa ndugu zake huku dar wanataka kuniona eti mtoto wao sijui ndugu yao! Basi yule baba akipiga nikiona namba yake natetemeka kwa hasira, na sipokei. Siku nikijiskia kupokea hawezi kuongea zaidi ya maneno mawili maana alikuwa anahisi hasira zangu.
Injili za msamaha nilikuwa nimeshazisoma sana na kuziskia kwenye mahubiri ya wachungaji na wanasaikolojia lakini kutekeleza ilikuwa ngumu. Nilikuwa naona nikimsamehe atafaidi sana. Yaani mwenzie (mama yangu) na babu na bibi wahangaike mpaka nimefika hapa halafu yeye ajilete kirahisi tu, na mimi nianze kuita baba uzeeni wakati wenzangu walijifunzia utotoni! Thubutu! Injili ya mwisho niliyosoma ni kitabu cha mch. kagya -
nafsi iliyojeruhiwa hutafuta kulipiza kisasi (kuna mtu hapa pia amesema alikisoma). nilikisoma, nikakiweka kwenye
shubaka kama miaka miwili hivi. siku 1 nikaonana nae laiv nikajadiliana nae kuhusu kitabu chake na nikampa stori yangu. Akaniambia nilimalize lile swala siku ile ile, pale pale. Akaniambia nimaanishe kutoka moyoni nikasema maneno pale wee....baba...natangaza nimekusamehe.......kuanzia leo nimekuachia....bla bla bla... Nikamuuliza sasa nimpigie simu nimwambie nimemsamehe? akaniambia huna haja ya kumpigia simu wala kumfata huko aliko. Cha msingi wewe umemwachia.
Akanipa kisa cha binti mmoja aliyetelekezwa na babake. Binti alipokuwa mkubwa wa kujitegemea akamtafuta babake bila mamake kujua, akaja dar akaenda mpaka ofisini kwa babake. Baba akamkumbatia kwa furaha na baada ya kazi akaenda nae nyumbani kwake (nyumbani kulikuwa na mke na watoto). Mara usiku binti anaskia mtu anagonga chumbani kwake, akafikiri anaota, akahakikisha haoti, kuuliza nani baba kajibu, kwa hofu binti akafungua. Vuuup! baba ndani ya taulo kajiongeza ndani , kamkamata binti anataka kumbaka. Kukuru kakara binti kachomoka. Binti akajuuuuuuuuuuuuuuuuuta kumfahamu babake! Nikamwelewa mchungaji yule.
Siku hiyo nikalala mwenye amani kweli kweli, mwili mwepesiii. Kumbu kumbu za baba zikinijia nikawa sishikwi na hasira kama mwanzo. Siku moja akanipigia nikashangaa nimepokea bila kusita na nikamsalimia vizuri na maongezi yakachukua kama dakika 3. Sina mpango wa kumtafuta lakini sina tena mzigo wa chuki dhidi yake. Na nimeshajifunza kutokumuweka mtu kiporo kwenye moyo.
Kisa kingine nilikisoma kwenye kitabu kinaitwa "joy comes in the morning" cha hopolang phororo. Kama mafanikio ni elimu na kazi basi huyu mama amefanikiwa sana. Wakati anaandika kile kitabu alikuwa country director wa shirika la kazi duniani hapa tz. katembelea sana dunia. huyu alibakwa sijui niseme kunajisiwa mara kadhaa akiwa mtoto wa miaka 10 hivi. akakaa kimyaa kwa miaka 30 ila moyoni anaskia kufa kufa. staki kuwachosha zaidi kusoma gazeti langu lakini huyu mama alihangaika sana kujikubali uwezo wake, alikuwa anajiona hafai, hakuweza kuanzisha mahusiano na wakaka, na yakianza hayadumu. Aliteseka na siri yake mpaka alipofikisha miaka ya 30 ndo akaamua kufunguka na hatua mojawapo ilikuwa kumsamehe yule baba. Hakuwa anajua yuko wapi, hai au mfu, alimtaja tu jina fulani huko uliko nimekusamehe.......kisha akaendelea na mchakato wa kupona. Alikuja kupenda na kukubali kupendwa akiwa kati kati ya miaka ya 40. Sasa hivi ni mtu mwenye furaha sana. Mpaka anaandika kitabu hakuwa ameolewa lakini walau moyo ulikuwa wazi kupokea upendo na kufurahia maisha. Hiyo ni nguvu ya msamaha. Na wale mnaoshinda kutwa kucha kutafuta threads za kuwaandama wanawake waliochelewa kuolewa mjuage kuna vitu kama hivi, na kama kuna aliyetelekezwa na mama yake achukue hatua ya kusamehe. Samahanini kwa gazeti na wikiendi njema.