Nguvu ya msamaha katika mahusiano/mapenzi

Nguvu ya msamaha katika mahusiano/mapenzi

Kuomba msamaha ni ishara ya kustaarabika na kujitambua Hasa kama unakuwa unaomba msamaha huo kwa dhati ya moyo wako na sio kushinikizwa.

Mimi mwenyewe na utata wangu wote ila kuna muda huwa ninaomba msamaha Hasa nikitambua kuwa nilichemka kwenye jambo husika (kiwe la kifamilia, mahusiano ya mapenzi, kikazi au la kisela tu na wana)

Hii huwa ina kufanya nijisikie mwepesi na mwenye jamani tele moyoni mwangu , na maisha kuyaona mswano kama kawa. Life goes on as usual as planned.

Hii huwa ni tiba s
Dah, mkuu huwa unawezaje kuomba msamaha marafiki?? Au hujawahi?
 
Tumejijengea ivo,kuomba msamah ni ishara ya udhaifu,lakin ukweli upo tofauti,MTU akiomba msamah ni ishara ya ukomavu kiakili,..unamsadia yule ulimkosea kukusamee na wewe kujifunza kutoka katika lile kosa,..
Well said mkuu, sema kumuomba msamaha mtu mnayelingana umri au mdogo kwako inakuwa ishu kweli
 
kuomba msamaha sio ishara ya udhaifu kama umekosea huna budi kumuomba msamaha uliyemkosea

kuomba msamaha kutoka moyoni
kunaweza kurudisha uhusiano uliovunjika

me ni mwepesi sana kuomba msamaha iwapo nimekukosea
 
Waungwana tu na wenye busara ndio huomba msamaha..

Na unapoomba msamaha haimaanishi wewe ni dhaifu hata kidogo, kwanza unapata amani ya moyo na kingine unakuwa umeimarisha mahusiano yako na uliyemkosea...

Hata kama mtu huna malengo haina maana ukimkosea ndo upotezee, hapana!!, ishi kwa amani na watu wote, hamna anaeijua kesho...

Kwangu mie msamaha huwa ni mwepesi sana kuomba!!!!
 
Kwa mstaarabu na muungwana yeyote yule anapojua amekosea basi hatasita kuomba samahani kwa kosa lake, lakini wale washenzi washenzi huwa hawajui/ hawataki kufanya hivyo.



Unajua Mapenzi ni kitu flani ambacho ni kigumu sana kudeal nacho.
Kwenye thread iliyopita yale watu waliocomment ,
kwa kiasi kikubwa ndio uhalisia wa jinsi watu wanavyoyatatua matatizo yao,

Niseme tu leo nimejaribu kumalizia utafiti nilioufanya kuanzia mitaani mpaka kwenye mitandao ya kijamii (ikihusisha familia,marafiki na wapenzi),

Nimegundua ukweli mchungu sana ambao wanaume lazima tukubaliane nao tu.
Kusema kweli wanaume bado tupo nyuma sana kwenye suala la kuyafanyia utabibu na kuyaponya mahusiano yetu yaliyovunjika(au yanayosuasua)

Na ndomana unakuta mwanamke akikukosea ni rahisi sana mahusiano yenu kurudi kwenye mstari kwasababu ni wepesi wa kutaka usuluhisho
lakini sisi vidume vya mbegu ndio tunajifanya kukaza usoni lakini moyoni tunateketea zaidi ya moto wa mabua!

Jambo hilo ni baya sana kwa afya kwasababu inasababisha wanaume tunaishi maisha mafupi sana.
Sijui kwa upande wa wanawake wanalichukuliaje hili suala ila

Naomba nieleweke kwamba hapa sizungumzii 'manungayembe'
bali nazungumzia yale mahusiano yaliyokuwa serious au wale walio ndoani.
.
Hebu tuambie wewe kwa upande wako unalichukuliaje suala la kuomba msamaha kuanzia kwenye ngazi ya familia, marafiki mpaka kwa wapenzi.
'Je, ni watu gani ambao hutokuja kuwaomba msamaha?'
 
Ukiona umeweza kuomba msamaha bila kung'ang'ania kuendelea kuwa mgumu, jua wewe ni mtu mungwana. Na mtu ambaye hawezi kusamehe mwache
Well said mkuu, hiyo ni njia moja wapo ya kuepusha magonjwa ya moyo,
sema uswazi tumezoea kuwekeana mtimanyongo
 
Hmmmmm! Umeingia kichwani mwangu weye! Lol!

Waungwana tu na wenye busara ndio huomba msamaha..

Na unapoomba msamaha haimaanishi wewe ni dhaifu hata kidogo, kwanza unapata amani ya moyo na kingine unakuwa umeimarisha mahusiano yako na uliyemkosea...

Hata kama mtu huna malengo haina maana ukimkosea ndo upotezee, hapana!!, ishi kwa amani na watu wote, hamna anaeijua kesho...

Kwangu mie msamaha huwa ni mwepesi sana kuomba!!!!
 
kuomba msamaha sio ishara ya udhaifu kama umekosea huna budi kumuomba msamaha uliyemkosea

kuomba msamaha kutoka moyoni
kunaweza kurudisha uhusiano uliovunjika

me ni mwepesi sana kuomba msamaha iwapo nimekukosea
Ulishawahi kuomba msamaha kwa kupiga magoti? Ulishawahi kumuomba msamaha rafiki yako?
 
hata siku moja simuombi msamaha mke wangu... nitajirekebisha mwenyewe kimya kimya... ila neno samahani asahau... akideka sana.. kwaooooooo!!!!!!!!
 
Hhahaha... Familia huwa zina drama sana...
Ulishawahi kuitwa kikao wewe na mwenzako kwaajili ya kuombana misamaha?

Bwana ehh ni hatari,..sasa acha uyo mi nshawai mtetea mdogo wangu wa kike asomeshwe boarding si akatoroka shule,..!?ase mpaka Leo nalaumiwa mim yaan,..
 
Back
Top Bottom