SoC03 Nguvu iliyofichwa yenye kuweza kuinua uchumi, wako, ari na hali nyingine za kimaisha

Stories of Change - 2023 Competition
Dec 10, 2020
15
14
Kila mtu katika ardhi ana uwezo wake wa kutoa msaada. Msaada unatofautiana kulingana na mtu hadi mtu na uwezo wa kutoa msaada huo. Kuna mafanikio makubwa sana yaliyojificha katika kutoa msaada. Unaweza kujiuliza kwa nini walio wengi hutoa msaada? Kwa nini imeandikwa katika maandiko matakatifu kuwa toa kile ulichonacho kwa asiyenacho?

Leo utapata kufahamu nguvu iliyofichwa katika msaada na nguvu hii huwainua wengi hata wale wenye uchumi mbaya huweza kujikuta wanapata uwezo hata wa kifedha na hata uchumi wao huinuka zaidi kutokana na nguvu hii.

Kwanza kabisa inakubidi kutambua kuwa, nguvu hii imefichwa kimafumbo na haionekani, kila mmoja anaweza kuihisi mara pale tu atakapoitambua. Matajiri wengi huitambua nguvu hii pale wanapopata faida kubwa kuliko hata biashara wanayofanya ndipo nguvu hii inakuwa pamoja nao na utaona kila mara utajiri wake unaongezeka. Nguvu hii imewekwa pamoja na neema iliyo njema ni nguvu ya ajabu na ina mafanikio makubwa.

Atakaye kufanikiwa kwa nguvu hii mara nyingi huambatana na heri kuu ambayo yeyote ambaye hana nguvu hii hawezi kuihisi isipokuwa tu yule aliyenayo nguvu hii anaweza kuihisi na ikamfanya kufanikiwa sana. Huu si uchawi wala si ushirikina wa aina yoyote ile. Ni kama muujiza unaotembea.

Kabla ya kuipata nguvu hii unapaswa kuijua namna ilivyo na inavyopatikana kwa maana ni rahisi sana kuipoteza hivyo usipokuwa makini unaweza kuipata na kwa muda tu ikapotea. Hivyo kuifahamu kwake ndivyo utakavyoweza kuitunza na kupata mafanikio yake makubwa.

Kama nilivyosema awali kwamba nguvu hii kila mmoja anayo na kila mmoja ana nafasi yake ya kuweza kuipata. Wengine watadhani ni matajiri tu au wenye mali nyingi ndio wanaoipata nguvu hii, ndiyo maana nikasema imefichwa. Imefichwa katika fumbo kubwa ambalo ni gumu kulitatua kwani linahitaji hisia ya hali ya juu na iliyo halali kabisa.

Nguvu hii ipo kwa kila mtu lakini haifanyi kazi kwa kila mtu na inaweza kufanya kazi kwa kila mtu anayeweza kulitatua fumbo lake. Nguvu hii inaweza kukusaidia kuinua hali ya uchumi kwa kuwa ina karama zilizo ndani yake, inaweza kuinua ari, inaweza kuondoa masaibu mengi ambayo yangeweza kukupata pasipo kutarajia.
Leo nitakupa nguvu hii ili uweze kuitumia na kumbuka kuwa tayari unayo nguvu hii lakini fumbo lake limefichwa. Kama hata leo hujawahi kulifumbua fumbo la nguvu hii ya ajabu fahamu ina uwezo wa kufanya kazi na mwili wako na roho yako kwa pamoja ikakufanya kuishi kwa amani kuu mno ambayo hata utakapofumbua fumbo lake muda huo huo utaiona na kuihisi ipo na itaanza kufanya kazi na wewe.

Ili uweze kuipata nguvu hii na iweze kifanya kazi kwako ni lazima uifungue mwenyewe, hakuna mtu anayeweza kukufungulia kwani kila mtu ana ufunguo wake yeye mwenyewe. Hata kama utaifahamu lakini usipotumia ufunguo wako mwenyewe huwezi kuifungua. Kwa wenye bahati huweza kuifungua bila kuijua na akishaifungua akiijua papo hapo hubadilisha maisha yake.

Mabadiliko hayo humpeleka kwenye wema na kufanikiwa kwake kunakuwa ni rahisi mno kuliko hata anayajituma kufanya kazi kwa nguvu nyingi huku akipata masononeko ya kazi yake. Tofauti na aliye na nguvu hii hata akifanya kazi ngumu wala hapati masononeko na faida yake ni kubwa mno huku akiwa na furaha iliyo na uhuru.

Nguvu hii iko katika msaada, sasa kila mtu anaweza akaona ni rahisi kutoa msaada na kuipata nguvu hii lakini si hivyo. Msaada huo unaotoa ni lazima uwe na utulivu na hauna dhamira yoyote ya kuweza kupata kitu kingine kufidia ulichotoa.

Lakini pia uwe umeinua furaha ya nafsi na kumfurahia yule unayempa msaada huo kuwa una manufaa na umetoa kilicho chema na unastahili kufanya hivyo. Na huyo mtu unayempa hatasononeka badala yake kila atakapoenda ndani ya nafsi yake atakuwa ana kumbukumbu ya kumjengea furaha kwa msaada uliompa na kupitia hiyo kumbukumbu nguvu hiyo inaanza kufanya kazi kwako.

Wakati ikianza kufanya kazi kwako, inakuwa inaunganisha furaha yenu wawili kati ya aliyesaidiwa na aliyetoa msaada. Na inakuwa inaongeza baraka ya tumaini kwa aliyesaidiwa na huku ikimjaza baraka aliyetoa na kumpa mafanikio yaliyo na amani.

Nguvu hii inaweza kupotea pale utakapohitajika kutoa msaada na una uwezo wa kufanya hivyo lakini ukajikataza kwa maksudi kutoa msaada huo. Taratibu itaanza kuyeyuka na kurejesha hali ya kutaka kujilaumu kwa kutokusaidia.

Tambua msaada unaoweza kuutoa, kiukweli kama nilivyosema kila mtu ana nafasi na kila nafasi ni kubwa kulingana na uwezo wako na yule anayehitaji. Kuna watu wanaohitaji zaidi msaada wa kifedha ukiwa na fedha toa hiyo fedha utafanikiwa, kuna wale wanaohitaji msaada wa kimwili mfano mtu aliyeumwa ama ameumia hajiwezi na uko pale una uwezo wa kutoa msaada.

Ukikuta hali kama hiyo kwa msukumo wote hata kama ulikuwa na jambo kubwa mno ahirisha na utoe msaada kwa kujitoa tu kumsaidia mtu huyo mfano kumbeba kumpeleka hospitali au huduma ya kwanza hii itakufanya ufanikiwe na kujisikia amani wakati wote ikiwa hautaivunja nguvu hii kwa ukaidi wa kutokutoa msaada.

Kuna wengine wana matatizo na yanahitaji msaada sahihi wa kimawazo. Mtu huyo utakuta anaumia sana na hajui lolote la kufanya ukiwa na wazo kuhusu suala lake mpe wazo hilo kwa moyo mmoja bila kumpotosha. Basi utafungua nguvu yako papo hapo.

Kuna wale wenye uhitaji wa chakula mfano umemkuta mtoto, mama, kaka dada, au mzee ambaye anahangaika kwa kukosa chakula na hana uwezo na wewe una uwezo wa kumsaidia hata kidogo basi kwa moyo wako msaidie na dhamira iwe ile ile kutokudhamiria kurejeshewa basi utafungua nguvu hii yenye mafanikio makubwa.

Mahitaji ni mengi na hayalingani kulingana na msaada unaohitajika na kila mtu ana uwezo wake kulingana na kile kinachohitajika kwa mtu husika anayehitaji msaada. Hivyo utaoji wako tu wa msaada huo ndio ufunguo wako wa mafanikio yako. Kumbuka kutoa msaada bila kutaraji kurejeshewa na msaada unaoutoa uwe wa moyo wako wote na wa upendo kwa unayempa msaada. Wanaofanikiwa zaidi ni wale wanaojitoa mara nyingi kila wanapoona wana uwezo wa kutoa msaada kwa wanaohitaji.

Uliwahi kujiuliza ni kwa nini watu wengi wakianza kufanikiwa hata kiuchumi huanza mara huanza kutoa misaada mingi? Hii ni kwa sababu walishaiona hiyo nguvu na walishaifungua hapo mwanzo na wanapotoa inawapa furaha zaidi na amani zaidi. Furaha hii ni ya kipekee sana si kila mtu anaweza kuipata isipokuwa anayetoa kwa moyo tu. Hivyo ili ufanikiwe hata wewe ndugu yangu jifunze kutoa misaada kwa wahitaji.
 
Juzi nmeamka nkajiandaa kuingia mzigoni kama kawaida tu

Nkatoka nje nataka kwenda kazini nkamuangalia mtoto mmoja wa jirani nkamuita nkampa andazi moja
(Jirani hupika)
Akachukua akaenda anakula huku anaruka ruka
Nkatoa 500 tu nkaongeza ma nne nkampa mama yake nkaendaga zangu

Nafika mbele huko nkakutana na mwalimu mmja ameharibikiwa na TV na amplifier yake
Vyote anavitumia sehemu ya biashara yake
Akidai alikua ananitafuta nkamuangalizie ina shida gani
Tv ni nch55 samsung ya mtumba
(Note me hua sitengenezi tv ila sound system pekee)
Nkaifungua nkakuta capacitor 2 zimevimba nkazibadili nkaiwasha ikawaka vizuri
Nkafungua ile amplifier nkakuta imeharibu just resistor tu! Nkaibadili ikafanya kazi vizuri

Jamaa kaja amefurah maana alijua tu mziki wa kuitengeneza ingekua ghali sana au isiwake
Nkamwambia jumla ya vifaa na ufundi ni elfu 57
Jamaa kaingia mfukoni kanikunjulia nkaendaga
Imagine 500 tu inanipa elf hamsini na kidogo

Hu ni mfano mmja tu kati ya 100 ila unapotoa nafsi ya yule unaempa ikifurahi basi kwako ni zaidi ya zawadi
 
Back
Top Bottom