Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,505
- 51,111
Kwa jinsi serikali inavyobehave huko Ngorongoro, huenda kuna makosa ya kutisha dhidi ya binadamu yanayofanyika huko. Hii nguvu ambayo serikali inatumia ili kuzuia ukweli inatoka wapi?
Hali hii inatia mashaka sana kwa sababu haiwezekani serikali iwageuze wananchi wake kama watumwa wasiostahiki haki yoyote katika nchi yao.
Inawezekana vipi uzuie wananchi wa eneo moja wasiwe na contact na wenzao?, unataka kuficha nini?
Kwa mujibu wa katiba ya nchi, wananchi wana haki ya kwenda mahali popote nchini. Sasa inakuwaje Serikali inazuia watu kwenda huko Ngorongoro, hii inakuwaje?
Hapa kuna kitu, huenda kuna crime against humanity ya kutisha sana huko ngorongoro, na ninapenda kuwaonya wote wanaohusika kwenye uhalifu huu kuwa hili jambo siyo dogo, na litawafikisha pabaya sana. Kama wasipokaa chini na kujitafakari, watapelekwa katika mahakama za kimataifa za uhalifu dhidi ya binadamu, wajitafakari sana.
1. Tunaambiwa bajeti ya kuhudumia wananchi wa Ngorngoro imesimamishwa
2. Wananchi wanawekewa vikwazo vikubwa vya kupata mahitaji yao msingi ikiwemo manunuzi ya msingi ambayo zamani walikuwa wakiyapata karatu.
3. Wanaume wamekimbia maboma yao kuogopa kukamatwa, wanawake ndo wanalea maboma yao.
Huu ukatili huu, rais Samia unawezaje kuuvumilia?.
Nakushauri rais Samia. Mama acha, acha kabisa, hili ishu ni kaa la moto. achana nayo kabisa. Kama mwarabu katoa pesa ili ajimilikishe ngorongoro rudisheni hizo pesa. Zitakutokeeni puani, Hizo pesa hazina maslahi kwa Taifa.
Hakuna pesa duniani zenye thamani kuliko maisha ya wananchi. Hivi ni heshima gani mbele ya huyo mwarabu mnaipata kwa kuuza wananchi wenu kwa vipande vya fedha?
Taarifa zilizopo ni kuwa wamasai wanachomewa nyumba zao, mazao yao, mifugo yao imewahi kupewa chumvi ya sumu, mnawaharrass viongozi wao!. Huu ni uhalifu mkubwa sana wa kibinadamu.
Dunia inaona, na tunadocument, huko mbeleni wahusika wa udhalimu huu wakifikishwa the hague tusije tukalaumiana!