Ngoma za mashetani

Ngoma za mashetani

Bora umeuliza jirani, unakufaham kwa mwananyange?? Halaf naskia ukipita karibu kamauna jini kichwani waweza jiunganao kwenye ngoma yao, hapo itakua tukwa kibao
Wewe mdigo pia. Hebu tuambie kwa kina.
 
Ni mambo yanachanganya sana dada. Mimi hua sielewi kama shetani ndio jini au ni vipi!

Hicho kifudu simchezo maana wanakua kama ngoma ya Mfalme Mswati anachagua mke, na pia matusi nje! Tena hapo wamechanganyika mama, watoto, kaka, dada.shangazi n.k

kwa vigezo vyote hiyo ni shirki tu dada. Na ni makabila na koo nyingi wanayo haya mambo ila hutofautiana namna ya kufanya
Wengi hata kimaendeleo wako nyuma sana,hilo kabila kwa Tanga ndo liko nyuma sana kiuchumi kielimu pia sababu ya shirki.
 
imani kaka, imani n kitu cha ajabu sana

Nakumbuka wakat niko vanga, kuna babu mmoja na yeye ni mganga, alikuja mdada siku ya kwanza akasema usiku anaota ndoto za ajabu ajabu kaja kutafta tiba ndoto zil zikate, akaambiwa aje siku inayofatia, sasa yule babu ni tapeli si mganga halisi, kulipokucha dada wa watu akaja wakat huo babu alishasahau kama kuna mtu atafata dawa alichokifanya akamwagiza mtoto wa mkewe wa kwanza et akamletee dawa, sasa me nilikua uwani na bibi huyo mke wa huyo babu, akaja yule kaka akachukua rangi za ukili najua wazijua akadondoshea kidogo kwneye maji ya lita moja akayachanganya aakanifanyia ishara ya kua kimya nikabaki nasikitika na kucheka akapewa jinsi ya kutumia kombe hilo feki baada ya siku tatu akaleta mrejesho ndoto zimekata asee nilicheka sana
Umenichekesha kweli dada, inamaana kapewa dawa fekilakini tatizo lake likaisha!

Huoni ni mambo ya saikolojia tu hayo? Waganga wanapiga hela balaa na wateja hawaishi maana wajinga wapo wa kutosha

Lakini pia kuna dawa za mitishamba za magonjwa ya kawaida kama chango la watoto, vidonda vya tumbo, kuumwa kichwa n.k
Hizi zipo na wanafanya watu ambao wala hawajiusishi na ushirikina
 
Hizo ngoma ni matawi ya Freemasonry na wote hao ni Freemasonry, sawa na ngoma za vodoo za west Africa.
Inawezekana kabisa mkuu, sio Afrika tu hata Caribbean kama Haiti na Dominica ambapo ngozi nyeusi ipo kwa wingi hizi mambo zipo
 
hahahaha sasa unataka kuyaona maziwa ya dada zako,mashangazi zako bibi zako utapofuka
Vijijini kwenye unyago,au kwenye mila zinazotahiri vifua wazi viko vingi tu kama mswati,utamaduni wa kuvaa nguo tumeletewa na wazungu.Aibu ni baada ya kuishi mjini vijijini sehemu zingine kuwa uchi ni kitu cha kawaida wala hakuna ashangae,mtoni mnaoga wote,hakuna anaejali.
 
Kwani mkuu usomi kunakufanya MTU kusahau mila na utamaduni wako??
Hapana usomi haukufanyi usahau au upuuze mila Beef Lasagna

Kinachogomba hapa ni mila zisizofaa kama kutembea matiti wazi kwa wanawake tena wakiwa wamechanganyika dada, kaka, shangazi, mjomba n.k, kutukana matusi ya nguoni mbele ya watu wako unaowaheshimu, na mengi mengine yanayokera
 
utajitaftia laana shaur zako
Tanga wanazicheza sana
Wakati niko mdogo palikuwepo na babu basi walikuja watu wanaopandisha sisi tunaita (Majini) kumtibu mtu huyo ngoma zilikuwa zikipigwa na kufanya sherehe (Chano) na kafara (hapo utaaguliwa na kuchanjwa chale mwilini) kisha watakiweka dawa tena huwa wanafanya pale yule jini anapopataka mfano chini ya mti,njia panda au hata kwenye vile vijumba vya waganga ambavyo hujengwa maeneo maalumu kwa mujibu ya ndoto zao.

Mwishowe mtu anapona
(Chano inatumika pia pale mama mzazi anapoenda kwa babu na kuaguliwa kwa lengo la kumkinga mtoto na wanga au watu wenye vijicho ili asipigwe "zongo" na "visimo" tena vya kizeia

"Nakumbuka yule aliyeniibia shilingi 4,000,000 milioni nne na kwenda kwa yule babu yangu na baada ya siku nne yule mwizi alikuja kwangu na kiasi cha zile pesa hazijapungua na aliniomba msamaha eti nimsamehe alikosea"

Anyaway nilishaondoka kijijini kwa sasa niko mjini na haya mambo hayana nafasi tena kwangu
 
Umenichekesha kweli dada, inamaana kapewa dawa fekilakini tatizo lake likaisha!

Huoni ni mambo ya saikolojia tu hayo? Waganga wanapiga hela balaa na wateja hawaishi maana wajinga wapo wa kutosha

Lakini pia kuna dawa za mitishamba za magonjwa ya kawaida kama chango la watoto, vidonda vya tumbo, kuumwa kichwa n.k
Hizi zipo na wanafanya watu ambao wala hawajiusishi na ushirikina
ndio mana nikakwambia imani kaka, mtu akiamini hua, yan nilicheka sana ile siku nikagundua waganga wengi sio wa kweli,
 
Tanga wanazicheza sana
Wakati niko mdogo palikuwepo na babu basi walikuja watu wanaopandisha sisi tunaita (Majini) kumtibu mtu huyo ngoma zilikuwa zikipigwa na kufanya sherehe (Chano) na kafara (hapo utaaguliwa na kuchanjwa chale mwilini) kisha watakiweka dawa tena huwa wanafanya pale yule jini anapopataka mfano chini ya mti,njia panda au hata kwenye vile vijumba vya waganga ambavyo hujengwa maeneo maalumu kwa mujibu ya ndoto zao.

Mwishowe mtu anapona
(Chano inatumika pia pale mama mzazi anapoenda kwa babu na kuaguliwa kwa lengo la kumkinga mtoto na wanga au watu wenye vijicho ili asipigwe "zongo" na "visimo" tena vya kizeia

"Nakumbuka yule aliyeniibia shilingi 4,000,000 milioni nne na kwenda kwa yule babu yangu na baada ya siku nne yule mwizi alikuja kwangu na kiasi cha zile pesa hazijapungua na aliniomba msamaha eti nimsamehe alikosea"

Anyaway nilishaondoka kijijini kwa sasa niko mjini na haya mambo hayana nafasi tena kwangu
kuna ile shetani anataja jina nayo inakuaje?? Mimi haya mambo mekuja yaona huku tanga, karibu waganga wengi hufanya hivi hizi ngoma huku n maarufu sana na zile nai zikipulizwa mm zinanikera sana saa zingine hakuja kucha unazisikia ni kazi jaman mambo mengine
 
Mshana Jr Hapa mtaani kwa ndugu zangu wadigo leo ni siku ya tatu wanacheza ngoma za mashetani. Watu wamejaa, wengi. Magari huwezi amini wingi wake. Mbuzi, kondoo, kuku vinachinjwa , damu mbichi zinanyweka etc. Ebu tufahamishe ngoma za mashetani ndiyo kitu gani? Umuhimu wake ni upi?
Dogoli, waathirika wengi ni kina mama wasio na elimu. Ni mara chache sana kukuta wababa na kina mama wasomi.
 
"Nakumbuka yule aliyeniibia shilingi 4,000,000 milioni nne na kwenda kwa yule babu yangu na baada ya siku nne yule mwizi alikuja kwangu na kiasi cha zile pesa hazijapunahagua na aliniomba msamaha eti nimsamehe alikosea"
Dah! Milion nne ikarudi nzima nzima mkuu, hahahaa si mchezo aisee

Inabidi Serikali watumie watu kama hao ili kudhibiti ufisadi😀😀😀

Mtu akipiga hela ya uma anajikuta anaingiwa na pepo la kuzirudisha yeye mwenyewe kama alivofanyaga Ngeleja zile za mgao wake wa Escrow 😎😎😎
 
Hapo kwenye unyago pia ni kwa nn mwari akichachezwa hutandikwa bakora hasa akiwa mjeuri??? Wanasema pia unyago una mizungu kiasi kupelekea wanaoicheza wengi kua washirikina kuna ukwelu?

Back
Top Bottom