Ngoja tuongelee Uasherati na Uzinzi kidogo

Ngoja tuongelee Uasherati na Uzinzi kidogo

Bueno

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
34,610
Reaction score
59,577
Wakuu, naona watu wanachanganya mafaili kidogo kuhusu haya masuala mawili ya kingono. Yaani Uasherati na Uzinzi. Uasherati ni nini na uzinzi ni nini?

Uasherati ni kitendo cha kufanya ngono au kujamiiana kwa hiari na mtu ambae sio mkeo na wala sio mumeo yaan hamjaoana na hii inaingiza uzinzi humo humo yaani ndani ya uasherati kuna uzinzi ndani yake.

Uzinzi ni kitendo cha mwanamke ambae ameolewa kisha anafanya mapenzi au ngono yaan anajamiiana kwa hiari na mtu mwingine ambae sio mume wake halali. Huyu ni Mzinzi.

Uzinzi ni kitendo cha mwanaume ambae ameoa kisha anafanya mapenzi au ngono yaan anajamiiana kwa hiari na mtu mwingine ambae sio mke wake halali. Huyu ni Mzinzi.

Huu ni uzinzi na ndani ya uzinzi hakuna uasherati ila ndani ya uasherati kuna uzinzi.

Mathayo 19 : 9
9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

Warumi 7 : 2-3
2 Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali yule mume akifa, amefunguliwa ile sheria ya mume.

3 Basi wakati mumewe awapo hai, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine.

Leo nalala mapema sana. Kumbe ni saa sita hii.
 
Back
Top Bottom