LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 15,254
- 27,547
- Thread starter
- #81
SawaMISERY LOVES COMPANY
Ndugu Likud naona una hali ngumu kifedha kwahiyo unataka watu wa kampani ya watu wenye majanga kama yako ili ufarijike. Nadhani ushauri wako ungejikita kwenye kuwasihi wasio na hela wasijilazimishe kufanya mambo yaliyo juu ya uwezo wao. Kusema kwamba Kayumba ni bora ni kujipa tu moyo kijinga. Mimi kama mdau wa elimu naweza kukuthibitishia kuwa Kayumba zenye ubora kwa Tanzania ni za kuhesabika. Kwa shule za msingi ni chache mno. Na kwa sekondari ni upate zile shule zinazoitwa za kitaifa. Hakuna namna unayoweza kumshawishi hata kichaa kwamba shule ya Sekondari Oljoro ambayo wanafunzi hupanda malori ya mchanga kwenda shule ni bora kuliko St Patrick au Arusha Modern. Hakuna bingwa wa malezi ila kwa asilimia kubwa tabia ya mtoto huanzia nyumbani na kwa kuiga wazazi wake. Ukiwa laissez faire lazima watoto watakuwa hovyo. Mkuu Likud kufulia ni sehemu ya maisha. Jitahidi kubeba msalaba wako bila kutaka kampani ya watu wengine.