Ngara kwalipuka risasi zapigwa usiku kucha!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,977
20,243
Mpaka wa tanzania rwanda na burundi si salama kwa sasa kwa tangu juzi mapigano makali yanaendelea mpakani ambapo vikundi vya wapiganaji vimejichimbia eneo hilo!
Taarifa za awali zinasema ni mapigano kati ya waasi wa burundi na serikali ya burundi, taarifa zinazidi kuchanganya baada ya kubainika kuwa majeshi ya tz yapo mpakani yakijibu mapigo!

Hali hiyo imepelekea wakazi wengi waishio mpakani kuyakimbia makazi yao.
Mgodi maarufu wa Kabanga Nikel nao umesitisha shughuli zao kufuatia mapigano hayo ambayo yamekuwa kama siri vile!

Habari zaidi zitaendelea kutolewa hapahapa jf chanzo kikuu cha habari za lugha ya kiswahili duniani hususani tz!
 
Majeshi ya tz wanajibu mashambulizi kwani wameingia kwenye ardi yetu?
 
Majeshi ya Tanzania waache kiherehere. Tuna matatizo mengi, hatuna muda wa kuingia vitani.
 
matatizo haya ukiongeza na vita na manunda wa burundi,rwanda,somali,. sijui........
 
Vita tuliyonayo inatutosha tumeshajifia kitambo mfumko wa bei,ubabaishaji mikopo wanafunzi elimu ya juu,ufisadi na hili eeeeh! tutaoza sasa wana JF.
 
Mpaka wa tanzania rwanda na burundi si salama kwa sasa kwa tangu juzi mapigano makali yanaendelea mpakani ambapo vikundi vya wapiganaji vimejichimbia eneo hilo!
Taarifa za awali zinasema ni mapigano kati ya waasi wa burundi na serikali ya burundi, taarifa zinazidi kuchanganya baada ya kubainika kuwa majeshi ya tz yapo mpakani yakijibu mapigo!

Hali hiyo imepelekea wakazi wengi waishio mpakani kuyakimbia makazi yao.
Mgodi maarufu wa Kabanga Nikel nao umesitisha shughuli zao kufuatia mapigano hayo ambayo yamekuwa kama siri vile!

Habari zaidi zitaendelea kutolewa hapahapa jf chanzo kikuu cha habari za lugha ya kiswahili duniani hususani tz!
hizi taarifa ni za kweli?mmm ngoja ni ulize maana huko ni kwa wakwe na sijajua lolote
 
Majeshi ya tz wanajibu mashambulizi kwani wameingia kwenye ardi yetu?

Ww acha kuwa juha! Jeshi la tz liache kimbembele wakati wao ndo wamekuja kupigania kwenye ardhi yetu, na je unazijua vizuri kazi za hili jeshi? Kama hujui kitu its better ukawa kimya.
 
Ingetakiwa wafike hapo Dar then Arusha na watingishe mahala muhimu ya chama tawala.
 
Majeshi ya Tanzania waache kiherehere. Tuna matatizo mengi, hatuna muda wa kuingia vitani.

Kazi ya jeshi ni kulinda nchi dhidi ya uchokozi wa aina yoyote toka nje. JWTZ wako sahihi kabisa kama wameanza kujibu mapigo...istoshe hapo patafaa kuyatumia mabomu yalioxpaya makambini kuliko kuyahifadhi na baadae yanauwa watz wa mbagala na g'mboto.
 
wanajeshi wetu tafadhalini msiruhusu hao waasi waje huku malizaneni nao huko huko.Nalog off
 
Una laana ya kwenu wewe! Ama ndiyo wale wale kiuno wewe!

wewe pumbavu unafikiria kwa kutumia makalio nadhani.
Kwa hiyo kama kuna jambo kama hilo JWTZ watazame tu?
Hebu simama pengine akili zitafunguka kinyesi wewe!
 
tatizo wale waasi wanapigana kutokea tanzania.na wanapozidiwa wanakimbilia tanzania kama wakimbizi.kwa mfano pale muluvyagira na mkikomero ngara mpaka wa burundi na Tanzania waliweka vijisiment kama mipaka ya nyumba na nyumba pengine ni miti imepandwa so waasi wanapopigana wanashindwa kujua kama wapo Tanzania kiasi kwamba mapigano unakuta yanafanyikia Tanzania. So hawa JWTZ wanapo ona hivyo wanaanza kupiga risasi ili kuwarudisha nyuma kitu kinachofanya askali wa burundi wawaone kama waasi.mia
 
Duh umenikumbusha mbali sana...enzi za kunywa primus pale Mugoma mitaa ya kati.......bhite shaa amakuru yawe?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom